Waandishi wa habari wanafanya kazi kwa uhuru Tanzania

Besta Mlagila

Member
May 29, 2018
96
150
Serikali ya Tanzania inaendelea kuheshimu na kulinda tasnia ya habari na wanahabari kuweka misingi imara ya sheria inayofanya watendaji wake kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na mhimili mwingine wa Nchi.

Tasnia na wanatasnia wa Tanzania wapo huru na wanaendelea kulindwa na kuheshimiwa, ili kuwahakikishia watanzania uhuru huo, Serikali ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Rais Dkt JOHN POMBE MAGUFULI imeweka vipaumbele kwenye tasnia ya habari ambavyo ni pamoja na ulinzi na usalama na maendeleo ya kiuchumi kwa wanahabari. Aidha, sheria ya wanahabari ya mwaka 2016 nayo imelenga kutambua kuwa uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine.

Sheria iliundwa ili kuwafanya waandishi wa habari wanufaike na maslahi ya kazi zao kwani inawataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwalipa wanahabari mishahara mizuri ili wafurahie kazi zao. Bima za Afya kwa waandishi wa habari zimeainishwa kwenye sheria hii, huku pia ikiwataka wamiliki kuwaingiza wanahabari kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kama NSSF ili wanapostaafu wanufaike na mafao ya uzeeni.

Rais Magufuli anawaheshimu sana waandishi wa habari na taaluma yao kwa ujumla anawezesha kutambulika kwa kuwafanya wao wajiongezee maarifa ya elimu ili wao wawe na ueledi wa kutosha kwa kuandika mambo mengi ya kijamii. Uhuru wa habari unaozingatia maadili ndio nguzo aliyoiweka Rais Magufuli tangu Novemba 2015, alipoingia madarakani, waandishi wameendelea kuheshimika.
 

Attachments

  • File size
    2.5 MB
    Views
    0

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,599
2,000
Aliwapiga mikwara ITV kuonyesha habari za vita za wafugaji kule Moro,na hapo nikathibitisha kweli uhuru wa Media umeongezeka chini ya awamu ya 5.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom