Waandishi wa Habari wampa RC Hapi siku 7 awaombe radhi baada ya kiwataka wawe na vitambulisho vya wamachinga

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa wamempa siku saba mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi kuwaomba radhi baada ya kuwataka nao kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

Hapi alitoa kauli hiyo jana Jumatatu Mei 27, 2019 wakati akizungumza na watendaji wa Serikali kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara.

Aliwataja waandishi wa habari kama wafanyabiashara na vibarua wasio rasmi, huku akianisha makundi 53 yanayostahili kupata vitambulisho hivyo.

“Wafanyabiashara ni wengi kuna wapiga debe, wauza nyanya, mchicha, wachoma mahindi na hata waandishi wa habari na wapiga picha wote wanatakiwa kuwa na vitambulisho ili kuchangia kodi kutokana na kazi wanazofanya,” amesema Hapi.

Akizungumza leo Jumanne Mei 28, 2019 mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa, Frank Leornald amesema kauli ya Hapi inadhalilisha taaluma ya habari.

Leornald amesema waandishi wa habari mkoani humo wamefanya majadiliano na kuazimia mambo sita watakayoyawasilisha katika ofisi ya mkuu huyo wa Mkoa, na kutaka majibu ya haraka.

“Tumesikitishwa kuwekwa katika kundi moja linalolinganisha taaluma ya habari na wafanyabiashara. Katika maazimio hayo sita tumemuomba Hapi kutoa tafsiri rasmi anayoijua yeye kuhusu waandishi rasmi na wasio rasmi.”

“Tunaamini taaluma ya habari ni kama taaluma nyingine za sheria, udaktari na ualimu hivyo kuingiza wanahabari katika kundi la wafanyabiashara wanaotakiwa kuwa na hivyo vitambulisho ni kuidhalilisha taaluma yetu,” amesema Leornald.

Amebainisha kuwa Hapi anapaswa kuomba radhi kutokana na kauli yake hiyo.

“Mengine tutayatolea uamuzi baada ya Hapi kujibu barua yetu tuliyomuandikia,” amesema Leornald.

Leo mchana Mwananchi lilizungumza na Hapi kuhusu kauli yake hiyo na kufafanua kuwa aliwalenga wapiga picha wa mitaani akiwatolea mfano wanaopiga picha watu mbalimbali katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam, pamoja na wanaopiga picha katika sherehe mbalimbali.
 
Waache mambo ya ajabu wabebe vitambulisho hvyo vya kodi.Siku hizi waandishi binafsi wamejaa kibao na wanafanya biashara ya habar,kupiga picha watu,kuziuza,wengine picha za maharusi/sherehe n.k lakini hamna anayewafuatilia kulipa kodi.Hebu walipe hyo kodi ambayo wanafurahia kuona muuza mahindi anatoa
 
Waache mambo ya ajabu wabebe vitambulisho hvyo vya kodi.Siku hizi waandishi binafsi wamejaa kibao na wanafanya biashara ya habar,kupiga picha watu,kuziuza,wengine picha za maharusi/sherehe n.k lakini hamna anayewafuatilia kulipa kodi.Hebu walipe hyo kodi ambayo wanafurahia kuona muuza mahindi anatoa
kabisa mkuu
 
Yule faza alisemaga Wakimaliza kwetu, wataenda kufanya kwa nani vile!?
 
Hawa waandishi wasituletee uchuro. Eti amedhalilisha taaluma? Shit, kwa habari gani watu wa Iringa mnazoandika kama sio kusifu na kuabudu?
Kateni vitambulisho vya machinga hanna dili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom