Waandishi wa habari wamhurumia magufuli

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
MTANZANIA TAR 8 MACHI 2011
Pole Magufuli, wachapakazi hawatakiwi Tanzania hii!

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amemzuia Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuendesha mpango wa bomoa bomoa ya nyumba na mabanda yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara.
Kwa kauli yake, Pinda amesema Magufuli ameonyesha kasi kubwa katika kushughulikia suala hilo. Kwa maneno mengine ni kwamba amemtaka apunguze kasi ya utendaji kazi!
Kwanza ieleweke wazi kwamba hatuungi mkono uonevu dhidi ya wananchi. Lakini pia hatuungi mkono uvunjaji wowote wa sheria za nchi ambao kwa sasa umekithiri.
Magufuli anajulikana kama mmoja wa viongozi makini katika nchi yetu. Pinda amekiri hilo kwa kusema pale walipoona wizara fulani inalegalega kiutendaji, Magufuli amepelekwa kama buldoza kwa ajili ya kuleta ufanisi.
Kwa bahati nzuri ni kwamba, Magufuli amekuwa kiongozi wa aina yake miongoni mwa Baraza la Mawaziri. Mara zote amesimamia sheria. Ndio maana akiwa Wizara ya Ardhi, alibaini wananchi wa Luguruni, Dar es Salaam wameonewa, na akaamua walipwe fidia maradufu kulingana na sheria.
Tangu atoe agizo la kuwaondoa wavamizi ndani ya hifadhi ya barabara wengi walikuwa wameanza kuitikia. Wapo wanaojua wazi kuwa wamejenga nyumba za kuishi au za biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa, na kwa sababu hiyo wakawa wameanza kujiondoa wenyewe. Wapo waliolalamika kuwa wapo maeneo husika kihalali, na yeye akasema wanaostahili fidia kwa mujibu wa sheria, watalipwa. Hatukuona ubaya wowote kwa uamuzi huo.
Agizo la Pinda linalowalinda wavamizi wa hifadhi ya barabara si tu kwamba limemdhalilisha Magufuli, lakini limethibitisha kuwa viongozi wachapakazi katika nchi hii hawatakiwi. Viongozi wenye kasi ya kutekeleza wajibu wao nao hawatakiwi. Watatakiwa viongozi aina ya “njoo kesho, njoo keshokutwa.”
Mbaya zaidi, Pinda amekwenda kulizungumza suala hili nyumbani kwa Magufuli mjini Chato. Katika hali ya kawaida Pinda angeweza kutumia vikao halali, vikiwamo vya Baraza la Mawaziri kumtaka asiwabughudhi wavamizi. Kwa kumpinga hadharani, ni kwamba Pinda amesaidia kujenga utamaduni wa watu kutoheshimu sheria katika nchi hii.
Uamuzi huu hautashia hapo. Tutarajie wavamizi zaidi kwenye hifadhi za barabara na maeneo yote ya wazi maana Waziri Mkuu amezuia wasiondolewe. Baada ya uvamizi kuongezeka, Pinda anaweza kupindisha kauli yake kwa kusema “alinukuliwa vibaya!”
Kama Pinda anadhani kwamba bomoa bomoa inapunguza upendo wa wananchi kwa CCM, anajidanganya. Hata huko Libya ambako wananchi wanapata huduma zote bure, hata kulipwa mishahara bila kufanya kazi, bado wameuchukia utawala.
Kwa kudhalilishwa kiasi hiki, ingekuwa vema Magufuli atangaze kujiuzulu kwani kibinadamu hatakuwa na moyo wala kasi ya kuendelea na wajibu wake wa kulinda sheria kama alivyoapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WAMEKUWA WAKIONYESHA MASIKITIKO MAKUBWA KWA UAMUZI ULICHUKULIWA NA WAZRI MKUU MHE MIZENGO PINDA KUSIMAMISHA BOMOA BOMOA YA MAGUFULI ALIYOTANGAZA NCHI NZIMA.NI UKWELI ULIO DHAHIRI KUWA MHE JOHN MAGUFULI AMEKUWA AKIFANYA KAZI ZAIDI NA VYOMBO VYA HABARAI KULIKO ANAVYOFANYA KAZI NA VIONGOZI WENZAKE, MABSI WAKE NA SERIKALI KWA UJUMLA WAKE. HIVYO HAISHANGAZI KUONA BAADHI YAO WAKIMSIKITIKIA.

KATIKA TAHARIRI YA GAZETI LA MTANZANIA YA JUMANNE TA 08 MACHI 2011 MHARIRI WA MTANZANIA MHARIRI AMEDIRIKI KUMTAFUITI MAGUFULI HURUMA YA UMMA NA KUMSAFISHA KWA KUDAI KUWA MAGUFULI ALISEMA KUWA WANAOSTAHILI FIDIA WATALIPWA, JAMBO AMBALO SIO LA KWELI HATA KIDOGO. KILA MTU ALIMSIKIA MAGUFULI AKIDAI KUWA WATAKAOBOMOLEWA HAWATALIPWA FIDIA.

KATIK AYA YA TANO YA TAHARIRI HIYO MHARIRI ANADAI "KUTOKANA NA MAGUFULI KUWA MTU ANAYEFUATA SHERIA ALIAMUA WAATHRIKA WA LUGURUNI KULIPWA FIDIA MARADFU".

ASICHOJUA MHARIRI NI MAZINGIRA YALIYOPELEKEA MAGUFULI KUTOA MAAMUZI HAYO. AWALI WATENDAJI WA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WALIKUWA WAKIDAI KUWA MWAKA 1993 RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALILITWAA ENEO LA ARDHI YENYE UKUBWA WA KILOMITA 2 PANDE ZOTE MBILI ZA BARABARA KUU YA MOROGORO KATIKA ENEO LA LUGURUNI KWA AJILI YA SHUGHULI ZA SERIKALI, HIVYO WAATHIRIKA HAWAKUSTAHILI FIDIA HATA KIDOGO KWA KUWA WENGI WAO WALINUNUA NA KUENDELEZA ARDHI HIYO BAADA YA RAIS KUITWAA. ENEO HILO LINAFIKA MPAKA KWEMBE, MSAKUZI N.K

WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU NDIO WALIFANIKIWA KUMSHAWISHI MAGUFULI KUWA HATA KAMA ENEO HILO LILITWALIWA NA RAIS 1993, HAKUNA TAARIFA ZOZOTE ZILIZOTOLEWA KWA WANANCHI AU KUWEPO ZUIO LA AINA YOYOTE KWA WATU KUUZA NA KUNUNUA ADHI HUSIKA NA KUIENDELEZA HADI MWAKA 2007, HIVYO KWA MUJIBU WA HAKI ZA BINADAMU WATU WOTE WALIONUNUA ARDHI HIYO KATI YA 1993 HADI 2007 WANA HAKI YA KULIPWA FIDIA.

NA KWA UDHAIFU WA MAGUFULI KUPENDA UMATI MKUBWA WA WATU NA WAANDISHI WA HABARI, WANAHARAKATI HAO WALIHAKIKISHA MKUTANO WA MAGUFULI SIKU HIYO UNAHUDHIRIWA NA UMATI MKUBWA SANA WA WATU NA IDIADI KUBWA YA WAANDISHI WA HABARI. HALI HIYO ILIMFANYA MHE JOHN MAGUFULI KULAZIMIKA KUUTOSA MSIMAMO WA KATIBU MKUU WAKE, WATENDAJI NA WIZARA NA KUKUBALINA NA WANAHARAKATI HIVYO AKAKUBALI KUWAPA HAKI WANANCHI YA KULIPWA FIDIA.

MAZINGIRA NI HAYO HAYO KATIA HIFADHI ZA BARABARA, TOKEA 1967 HAKUNA MAMLAKA YOYOTE ILIYOWAARIFU AU KUWAZUIA WANANCHI KUJENGA KATIKA HIFADHI YA BARABARA; AIDHA SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA KATIKA OPERESHENI VIJIJI ILIWAGAWIA WANANCHI ARDHI ISIYOHUSIKA NA UPANUZI WA BARABARA YAANI ILIYOKO NJE YA FUTI 75 KILA UPANDE WA BARABARA, AMBAYO LEO HII MAGUFULI ANATAKA WATU KUBOMOA NYUMBA ZAO BILA FIDIA.

KAMA AMBAVYO MAGUFULI ALIAMUA KUWA WANANCHI WA LUGURUNI, KWEMBE N.K WANA HAKI YA KULIPWA FIDIA KAMILIFU KATIKA ARDHI ILIYOTWALIWA NA RAIS MWAKA 1993 VIVYO HIVYO WANANCHI WALIOKUWA WANAVIJIJI WA VIJIJI VILIVYOKUWA KANDO KANDO YA BARABARA YA MOROGORO WANA HAKI YA KULIPWA FIDIA KAMILIFU KAMA MAGUFULI NATAKA KUWAONDOA KATIKA ENEO ANALOLIITA HIFIDHA YA BARABARA.

WAHENGA WALITUFUNZA "MKUKI MZUIRI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU" ARDHI ILIYOTWALIWA NA RAIS NA HIFADHI ZA BARABARA ZOTE NI ARDHI ZA SERIKALI, HIVYO SIO BUSARA KUMSHABIKIA MAGUFULI KUWABOMOLEA NYUMBA WALIOKO KATIKA HIFADHI ZA BARABARA KWANI AKIMALIZA HAPO ATAKUJA KUWABOMOLEA WALE WANAOISHI KATIKA ARDHI ILIYOTWALIWA NA RAIS MWAKA 1993. TANZANIA ITAWABOMOLEA WANGAPI?
 
Pinda nilishasema hafai kuwa waziri mkuu toka day one anachaguliwa na mkwere....hajuagi anaongea nini na anamaanisha nini.....ni waziri mkuu wa hovyo kabisa kupata kutokea....
 
pinda nilishasema hafai kuwa waziri mkuu toka day one anachaguliwa na mkwere....hajuagi anaongea nini na anamaanisha nini.....ni waziri mkuu wa hovyo kabisa kupata kutokea....

hayo ni maoni yako, ila katika hilo alifanya maamuzi ya busara na hekima kubwa sana.
 
Hakufanya maamuzi ya busara hata kidoga: Kama uamuzi ulikuwa kusitisha zoezi la Magufuli, busara ilikuwa PM kumwita na kumwambia madhara ya hilo zoezi kwa sasa, na Magufuli mwenyewe angetangaza kusitisha zoezi hilo, kuliko WM kutangaza hadharani tena nyumbani kwa Magufuli kwamba zoezi hilo lisimame na aelekeze kasi hiyo kwenye Kilimo. Ina maana Pinda hajui kama kuna waziri wa Kilimo??

Kimsingi Magufuli amedhalilishwa sana tena mbele ya wapiga kura wake wakiwamo ndugu zake wa karibu, watoto wake, wazazi wake nk. Kwa mtindo huu si sahihi. Namshauri MH Magufuli achukue maamuzi magumu ili kulinda heshima aliyojijengea mbele ya jamii ya waTZ. Vinginevyo tunalazimika kuamini kuwa alijua zoezi hilo halikuwa na baraka za baraza la mawaziri na kwamba ilikuwa kinyume na sheria.
 
Mkuu Jatropha,

Jaribu kuandika kwa kuchanganya herufi kubwa na ndogo kwa kadri ya sentensi (badala ya kutumia herufi kubwa tupu!). Inakuwa rahisi zaidi kwa sie wasomaji wako kusoma ulichoandika.
 
Tunakukaribisha magufuli njoo cdm umashuhuri wako hautapwaya kama ilivyokuwa kwa mrema. Kuhusu pinda aaaaarrrghh just kilaza aliyebahatika kukaa madarakani kwa miongo kadhaa na ataondoka bila kuacha lolote.
 
hayo ni maoni yako, ila katika hilo alifanya maamuzi ya busara na hekima kubwa sana.
tangia lini Pinda akawa na busara?Angekuwa na busara angelidanganya bunge na watanzania?Pinda ni mtu wa kukurupuka na ni mtu wakuogopwa sana kwa unafiki,na ndio mana akizidiwa anatoa machozi.
"Waziri mkuu kivuli anetetea maslahi ya mafisadi"
 
Pinda ana wivu sana huyo na hana ubinadamu.Pinda ndiye aliyeshabikia wafugaji wa kisukuma/kimasai kufanyiziwa na wakulima huko kilosa.Pinda ana chuki na Wakulima/wafugaji wa kisukuma kwa sababu wameshika maeneo makubwa huko kwao Rukwa .Anamchukia Magufuri kwa sababu ni ana damu ya kisukuma.Pinda aliwahi kukosana na mzee Mapesa a.k.a Cheyo Mamose bungeni kwa kushabikia wafugaji wa kisukuma na kimasai kuhamishwa kilosa, hadi kufikia ng'ombe zao kuuzwa kwa shs30,000 per head.TOKA MAGUFURI WASIKUBABAISHE hebu fanya maamuzi MAGUMU KAMA WALIVYOFANYA WENZAKO SHINYANGA NA MWANZA, ACHANA NA CCM KARIBU CDM ujumuike na jirani yako DR.MBASSA
 
Mkuu una ungonjwa mbaya sana wa ukabila.
Ugonjwa ambao ni mbaya kuliko ukoma-kuendelea kujadili mada hii kwa misingi ya ukabila ni upofu wa kiakili.
Sitashangaa kama mkuu huyu atataka nchi ya kisukuma.
 
Wote wahuni tu..............................si Pinda aliyepinda wala si Magufuli aliyegafilika.......................................

Hapo napata picha kuwa mawaziri wengi hawaelewani, PM inawezekana alikuwa anavizia jinsi ya kumueleza J Pombe Magufuli lakini ndo hivyo nafasi/hesabu zilikuwa zinagoma. PM kapata kaupenyo kidogo, ndo hayo tumeyasikia.
 
Tunakukaribisha magufuli njoo cdm umashuhuri wako hautapwaya kama ilivyokuwa kwa mrema. Kuhusu pinda aaaaarrrghh just kilaza aliyebahatika kukaa madarakani kwa miongo kadhaa na ataondoka bila kuacha lolote.

Mlimkaribisha kabisa ahamie chadema ili aje akinukishe kwenye uchaguzi mkuu wa 2015! Basi mkubali tu kushirikiana naye.
 
MTANZANIA TAR 8 MACHI 2011
Pole Magufuli, wachapakazi hawatakiwi Tanzania hii!

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amemzuia Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuendesha mpango wa bomoa bomoa ya nyumba na mabanda yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara.
Kwa kauli yake, Pinda amesema Magufuli ameonyesha kasi kubwa katika kushughulikia suala hilo. Kwa maneno mengine ni kwamba amemtaka apunguze kasi ya utendaji kazi!
Kwanza ieleweke wazi kwamba hatuungi mkono uonevu dhidi ya wananchi. Lakini pia hatuungi mkono uvunjaji wowote wa sheria za nchi ambao kwa sasa umekithiri.
Magufuli anajulikana kama mmoja wa viongozi makini katika nchi yetu. Pinda amekiri hilo kwa kusema pale walipoona wizara fulani inalegalega kiutendaji, Magufuli amepelekwa kama buldoza kwa ajili ya kuleta ufanisi.
Kwa bahati nzuri ni kwamba, Magufuli amekuwa kiongozi wa aina yake miongoni mwa Baraza la Mawaziri. Mara zote amesimamia sheria. Ndio maana akiwa Wizara ya Ardhi, alibaini wananchi wa Luguruni, Dar es Salaam wameonewa, na akaamua walipwe fidia maradufu kulingana na sheria.
Tangu atoe agizo la kuwaondoa wavamizi ndani ya hifadhi ya barabara wengi walikuwa wameanza kuitikia. Wapo wanaojua wazi kuwa wamejenga nyumba za kuishi au za biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa, na kwa sababu hiyo wakawa wameanza kujiondoa wenyewe. Wapo waliolalamika kuwa wapo maeneo husika kihalali, na yeye akasema wanaostahili fidia kwa mujibu wa sheria, watalipwa. Hatukuona ubaya wowote kwa uamuzi huo.
Agizo la Pinda linalowalinda wavamizi wa hifadhi ya barabara si tu kwamba limemdhalilisha Magufuli, lakini limethibitisha kuwa viongozi wachapakazi katika nchi hii hawatakiwi. Viongozi wenye kasi ya kutekeleza wajibu wao nao hawatakiwi. Watatakiwa viongozi aina ya njoo kesho, njoo keshokutwa.
Mbaya zaidi, Pinda amekwenda kulizungumza suala hili nyumbani kwa Magufuli mjini Chato. Katika hali ya kawaida Pinda angeweza kutumia vikao halali, vikiwamo vya Baraza la Mawaziri kumtaka asiwabughudhi wavamizi. Kwa kumpinga hadharani, ni kwamba Pinda amesaidia kujenga utamaduni wa watu kutoheshimu sheria katika nchi hii.
Uamuzi huu hautashia hapo. Tutarajie wavamizi zaidi kwenye hifadhi za barabara na maeneo yote ya wazi maana Waziri Mkuu amezuia wasiondolewe. Baada ya uvamizi kuongezeka, Pinda anaweza kupindisha kauli yake kwa kusema alinukuliwa vibaya!
Kama Pinda anadhani kwamba bomoa bomoa inapunguza upendo wa wananchi kwa CCM, anajidanganya. Hata huko Libya ambako wananchi wanapata huduma zote bure, hata kulipwa mishahara bila kufanya kazi, bado wameuchukia utawala.
Kwa kudhalilishwa kiasi hiki, ingekuwa vema Magufuli atangaze kujiuzulu kwani kibinadamu hatakuwa na moyo wala kasi ya kuendelea na wajibu wake wa kulinda sheria kama alivyoapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WAMEKUWA WAKIONYESHA MASIKITIKO MAKUBWA KWA UAMUZI ULICHUKULIWA NA WAZRI MKUU MHE MIZENGO PINDA KUSIMAMISHA BOMOA BOMOA YA MAGUFULI ALIYOTANGAZA NCHI NZIMA.NI UKWELI ULIO DHAHIRI KUWA MHE JOHN MAGUFULI AMEKUWA AKIFANYA KAZI ZAIDI NA VYOMBO VYA HABARAI KULIKO ANAVYOFANYA KAZI NA VIONGOZI WENZAKE, MABSI WAKE NA SERIKALI KWA UJUMLA WAKE. HIVYO HAISHANGAZI KUONA BAADHI YAO WAKIMSIKITIKIA.

KATIKA TAHARIRI YA GAZETI LA MTANZANIA YA JUMANNE TA 08 MACHI 2011 MHARIRI WA MTANZANIA MHARIRI AMEDIRIKI KUMTAFUITI MAGUFULI HURUMA YA UMMA NA KUMSAFISHA KWA KUDAI KUWA MAGUFULI ALISEMA KUWA WANAOSTAHILI FIDIA WATALIPWA, JAMBO AMBALO SIO LA KWELI HATA KIDOGO. KILA MTU ALIMSIKIA MAGUFULI AKIDAI KUWA WATAKAOBOMOLEWA HAWATALIPWA FIDIA.

KATIK AYA YA TANO YA TAHARIRI HIYO MHARIRI ANADAI "KUTOKANA NA MAGUFULI KUWA MTU ANAYEFUATA SHERIA ALIAMUA WAATHRIKA WA LUGURUNI KULIPWA FIDIA MARADFU".

ASICHOJUA MHARIRI NI MAZINGIRA YALIYOPELEKEA MAGUFULI KUTOA MAAMUZI HAYO. AWALI WATENDAJI WA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WALIKUWA WAKIDAI KUWA MWAKA 1993 RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALILITWAA ENEO LA ARDHI YENYE UKUBWA WA KILOMITA 2 PANDE ZOTE MBILI ZA BARABARA KUU YA MOROGORO KATIKA ENEO LA LUGURUNI KWA AJILI YA SHUGHULI ZA SERIKALI, HIVYO WAATHIRIKA HAWAKUSTAHILI FIDIA HATA KIDOGO KWA KUWA WENGI WAO WALINUNUA NA KUENDELEZA ARDHI HIYO BAADA YA RAIS KUITWAA. ENEO HILO LINAFIKA MPAKA KWEMBE, MSAKUZI N.K

WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU NDIO WALIFANIKIWA KUMSHAWISHI MAGUFULI KUWA HATA KAMA ENEO HILO LILITWALIWA NA RAIS 1993, HAKUNA TAARIFA ZOZOTE ZILIZOTOLEWA KWA WANANCHI AU KUWEPO ZUIO LA AINA YOYOTE KWA WATU KUUZA NA KUNUNUA ADHI HUSIKA NA KUIENDELEZA HADI MWAKA 2007, HIVYO KWA MUJIBU WA HAKI ZA BINADAMU WATU WOTE WALIONUNUA ARDHI HIYO KATI YA 1993 HADI 2007 WANA HAKI YA KULIPWA FIDIA.

NA KWA UDHAIFU WA MAGUFULI KUPENDA UMATI MKUBWA WA WATU NA WAANDISHI WA HABARI, WANAHARAKATI HAO WALIHAKIKISHA MKUTANO WA MAGUFULI SIKU HIYO UNAHUDHIRIWA NA UMATI MKUBWA SANA WA WATU NA IDIADI KUBWA YA WAANDISHI WA HABARI. HALI HIYO ILIMFANYA MHE JOHN MAGUFULI KULAZIMIKA KUUTOSA MSIMAMO WA KATIBU MKUU WAKE, WATENDAJI NA WIZARA NA KUKUBALINA NA WANAHARAKATI HIVYO AKAKUBALI KUWAPA HAKI WANANCHI YA KULIPWA FIDIA.

MAZINGIRA NI HAYO HAYO KATIA HIFADHI ZA BARABARA, TOKEA 1967 HAKUNA MAMLAKA YOYOTE ILIYOWAARIFU AU KUWAZUIA WANANCHI KUJENGA KATIKA HIFADHI YA BARABARA; AIDHA SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA KATIKA OPERESHENI VIJIJI ILIWAGAWIA WANANCHI ARDHI ISIYOHUSIKA NA UPANUZI WA BARABARA YAANI ILIYOKO NJE YA FUTI 75 KILA UPANDE WA BARABARA, AMBAYO LEO HII MAGUFULI ANATAKA WATU KUBOMOA NYUMBA ZAO BILA FIDIA.

KAMA AMBAVYO MAGUFULI ALIAMUA KUWA WANANCHI WA LUGURUNI, KWEMBE N.K WANA HAKI YA KULIPWA FIDIA KAMILIFU KATIKA ARDHI ILIYOTWALIWA NA RAIS MWAKA 1993 VIVYO HIVYO WANANCHI WALIOKUWA WANAVIJIJI WA VIJIJI VILIVYOKUWA KANDO KANDO YA BARABARA YA MOROGORO WANA HAKI YA KULIPWA FIDIA KAMILIFU KAMA MAGUFULI NATAKA KUWAONDOA KATIKA ENEO ANALOLIITA HIFIDHA YA BARABARA.

WAHENGA WALITUFUNZA "MKUKI MZUIRI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU" ARDHI ILIYOTWALIWA NA RAIS NA HIFADHI ZA BARABARA ZOTE NI ARDHI ZA SERIKALI, HIVYO SIO BUSARA KUMSHABIKIA MAGUFULI KUWABOMOLEA NYUMBA WALIOKO KATIKA HIFADHI ZA BARABARA KWANI AKIMALIZA HAPO ATAKUJA KUWABOMOLEA WALE WANAOISHI KATIKA ARDHI ILIYOTWALIWA NA RAIS MWAKA 1993. TANZANIA ITAWABOMOLEA WANGAPI?
Kumbe Raisi Magufuli anasifika kwa Utendaji ulitukuka kabla hata hajawa Raisi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani jitu lina visasi hili ,sasa lilivyopata urais likarudia kuwabomolea walewale aliokatazwa kuwabomolea na pinda , ndio akili hiyo .
 
Back
Top Bottom