Waandishi wa habari walivyo dhalilishwa na ikulu ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari walivyo dhalilishwa na ikulu ya Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Aug 23, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ikulu, huu ni udhalilishaji

  Na Salehe Mohamed

  UKWELI daima humuweka huru mtu, na husaidia kurekebisha mambo pale yanapokwenda tofauti ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, nami nimeamua kuwa mkweli.

  Kwanza napenda kuishukuru Ikulu, kwa kulialika gazeti la Tanzania Daima kuwamo kwenye ziara ya siku nne ya Rais Jakaya Kikwete, katika mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Pwani, lengo kuu likiwa ni kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa baadhi ya barabara na nyingine kuzifungua.

  Nimeamua kuipongeza Ikulu, kwa hatua yao hiyo, kwa kuwa kwa muda mrefu gazeti hili halikupata fursa hiyo, kwa kile kinachodaiwa kuandika vibaya habari za serikali na wakati mwingine kumgusa rais kwa mambo yanayodaiwa kuwa na lengo la ama kumchafua au kumdhalilisha.

  Pongezi hizi nazitoa si kwa kujipendekeza kwa kuwa nilikuwamo katika safari hiyo, bali ni kwa ajili ya mwamko na kufumbuka macho kwa watendaji wa Ikulu na kujua nini maana ya uhuru wa vyombo vya habari pamoja na kuheshimu demokrasia ya kutoa na kupokea habari.

  Pamoja na pongezi hizo, lakini si vibaya nikaweka bayana yale yaliyonikera, ambayo mimi pamoja na wenzangu tuliona ni ya kutudhalilisha na yasiyopaswa kufanywa na watendaji makini wenye kufanya kazi katika taasisi nyeti kama Ikulu.

  Kwanza, ni pale maofisa waliposhindwa kutuweka katika orodha ya watu waliomo kwenye msafara wa rais, jambo ambalo lilitufanya tupate shida ya kupata malazi tulipofika Ikwiriri, mkoani Pwani, ambapo ilitulazimu kuhangaika sana mpaka ilipotimu majira ya saa tano usiku.

  Katika kuhangaika huko, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alilazimika kutoa fedha kutoka mfukoni mwake ili tutafute malazi, huku akituhakikishia kuwa siku ya pili tusingepata tabu kama hiyo na kumpa majina yetu ofisa usalama tuliyemjua kwa jina moja la Bomba, ambaye hakuweza kutimiza ahadi yake kama alivyotuahidi.

  Cha kusikitisha zaidi, siku ya pili tulilala mkoani Lindi, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi, kwani wageni walikuwa wengi na nyumba nyingi za kulala wageni zilikuwa zimejaa, hali iliyotulazimu kuzunguka mji mzima kutafuta sehemu ya kulala, ambapo tuliipata saa sita, lakini mazingira yake hayafai kuzungumzia mbele ya jamii ya kistaarabu na hasa kwa ujumbe ambao unaongozana na rais.

  Siku ya tatu tulilala wilayani Masasi, huko hali ilikuwa ni ile ile, tuliendelea kuwa mashuhuda wa majina ya wenzetu kama ilivyokuwa siku zilizotangulia, lakini safari hii tulikuwa werevu na tulianza kutafuta sehemu ya kulala mapema na kwa bahati nzuri tuliipata kwenye majira ya saa mbili usiku, huku mazingira yake nayo yakiwa hayaridhishi.

  Siwezi kusahau siku ya mwisho ya ziara hiyo ambapo tulidhalilika kiasi cha kutosha kwa kushushwa kwenye ndege huku tukiwa tayari tumekaa kwenye viti na kufunga mikanda tayari kwa safari.

  Siku hiyo rais alikuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Masasi kwenda Mangaka, ambapo katika sherehe hizo tulitangaziwa kuwa watu waliopo kwenye msafara wa rais watapaswa kwenda Katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara ili warejee Dar es Salaam kwa kuwa rais ana shughuli nyingine.

  Kibaya zaidi, baada ya kushushwa kwenye ndege tuliulizwa maswali yasiyo ya kiiungwana na wanausalama, ambao waliongozwa na mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Joachim, ambaye alionyesha kushangazwa na kukasirishwa na uzamiaji tulioufanya.

  Joachim, na timu yake baada ya kutuuliza maswali ya hapa na pale yasiyo na mantiki kwetu, alituahidi kuyafanyia kazi zaidi majina yetu ili kujiridhisha kama si watu wabaya ‘magaidi’ na kuturuhusu kuendelea na utaratibu wetu wa safari kwa njia ya barabara.

  Hivi kweli katika mazingira ya kawaida ni mtu gani ambaye anaweza kujichomeka katika msafara wa rais, tena kupanda ndege moja na rais na watu wa usalama wakamuangalia tu? Hilo haliwezekani hata kidogo, watu wa usalama walituacha tuingie kwenye ndege kwa kuwa walijua sisi tupo pamoja nao, kwa sababu safari yetu ilianza pamoja, tena mwanzo mwa makazi ya rais (Ikulu) na hata katika ziara nzima tulijumuika nao kuhakikisha kile kinachosemwa au kufanywa na rais, jamii inakijua.

  Kama Ikulu inaweza kuwasahau kwenye orodha yao waandishi waliowapigia simu na kuwagharimia, je, umakini wa watendaji waliokuwa wakishughulikia suala hilo upo wapi?

  Nilidhani taasisi hiyo ndiyo inapaswa kuwa kinara wa kufanya mambo yake kwa usahihi, kwa kuwa ina watendaji ambao naamini hawakupewa nafasi walizonazo kwa upendeleo.

  Ikulu ina waandishi na wapiga picha wake ambao kwa kipindi chote hicho walipata malazi bora na hata wakati wa kurejea Dar es Salaam walikuwamo kwenye ndege, kwa nini haikuwafanyia vitendo hivyo wao?

  Kama iliona haina shida na waandishi wengine, basi isingewaalika ili kukwepa kuwadhalilisha kuliko vitendo ilivyowafanyia. Watendaji wake wangeweza kutuambia waandishi mapema kuwa tusiende Mtwara.

  Tungeambiwa mapema tusingepata aibu hiyo, kwa kuwa tulikuwa na gari ambalo tulipewa kabla ya kuondoka Dar es Salaam na tulikuwa na maamuzi nalo, hivyo tungeweza kumwambia dereva turejee makwetu, naye akatutii bila matatizo.

  Kama watendaji wangetaka kutuambia hatumo kwenye orodha ya msafara wa rais wa kurejea, walikuwa na nafasi nzuri ya kufanya hivyo, kwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano niliongea naye wakati tunaondoka Masasi, akiwa analalamikia kichwa cha habari kilichoandikwa na gazeti langu.

  Nimeamua kuandika mambo haya, si kwa nia mbaya, bali kuwarekebisha watendaji waliozoea kufanya mambo kwa mazoea na kuwapuuza wajumbe wengine wanaoambatana na msafara wa rais kwa kudhani kuwa si wa muhimu kama walivyo wao.

  Binafsi nilitarajia baada ya kadhia ile Mkurugenzi wa Mawasiliano baada ya kufika Dar es Salaam angetupigia simu kujua mambo yalivyokwenda, baada ya kutuacha pale Mtwara, lakini hakufanya hivyo hadi jana asubuhi alipofanya hivyo, tena baada ya kusikia kutoka kwa baadhi ya watu jinsi tulivyotendewa na hatua tulizopanga kuchukua kuhusu udhalilishwaji ule.

  Lakini ningependa kumshukuru Katibu wa rais niliyemfahamu kwa jina la Jairo, ambaye alilazimika kushuka kwenye ndege na kutukimbilia tulipokuwa tunatoka kwa aibu kiwanjani na kutukabidhi kwa dereva wake kuwa ahakikishe anatufikisha Dar es Salaam.

  Binafsi naona katibu huyo alijisikia vibaya kuhusu kushushwa kwetu, tena rais akiwa amekwisha kuingia ndani ya ndege, jambo ambalo ni kinyume cha itifaki.

  Kwa kutumia kalamu yangu, nimeamua kutolinyamazia jambo hili hata kama watendaji wa Ikulu watachukia na kuamua kutolialika gazeti hili katika ziara za rais, naamini hatukualikwa kwa kuogopwa, bali ni kwa kuthamini mchango wetu ndani ya jamii.

  Nasi tuliona fahari kuwamo katika msafara, lakini hatutafumbia macho tabia ya kushusha hadhi na utu wa mtu, hata kama wanaofanya vitendo hivyo wana uwezo wa kifedha au kidola.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwa kweli inasikitisha sana.hii kitu andika na huko ikulu kwa bwana rweyemamu na eleza malalamiko haya.poleni sana ndugu waandishi wa habari
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama waandishi mlisahaulika, vipi madereva?
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  Poleni, ni communication breakdown on part of insignificance, thank God angalau mlialikwa, mafreelance ndio usiseme kabisa they are totally ignored.
  This country bwana...
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  poleni sana wanahabari, hii ndo bongo na huyo ndo raisi wetu, kama watu wote wanaomzunguka raisi ndo hivyo walivyo yeye mwenyewe yukoje,
  HUWEZI KUCHUMA TINI KWENYE MIIBA
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  kweli mwamba ngoma huvutia kwake....! badala ya kuandika kilio cha wananchi hususani UJAMBAZI au kuandika na kupasha umma juu ya kile alichoitiwa,mtu kwa ubinafsi na matakwa yake anaamua kuandika historia yake ya siku moja mahali paitwapo ikwiriri badala ya 'coverage'.
  Pia tunaona mtu huyu "mzamiaji" wa ndege ambaye kanuni na taratibu za "usalama wa kianga" unataka wasafiri wote wawe kwenye "manifesto" ya rubani. Kama wewe jina lako halikuwemo ni dhahiri hutapanda ndege. wewe ulikwenda kwa usafiri murua wa gari zuri, kisha utake kurudi kwa ndege........!

  EBOOO...! wewe uliambiwa ziara yako utapanda ndege?

  Mwandishi unalilia kupada ndege..........!!!!! kwi kwi kwi ....MWANDISHI WA GAZETI HILI BWANA........!

  HIVI UNAANDIKIA GAZETI GANI VILE......?
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  eti kwenye gazeti lenu la mwishoni mwa wiki hii ndo mnaandika na kuripoti nini kilijiri kwenye ziara hiyo.

  INA MAANA GANI KUTOHABARISHA KWA WAKATI ULE? badala yake mkawa mnasimulia habari ya kushushwa kwenye NDEGE MLIYODANDIA BILA IDHINI...! MLIAMBIWA NDEGE NI DALADALA....! UKIITWA UNAINGIA TU..... EBOOO!

  LABDA ULIITWA NA TEJA MPIGA DEBE AMBAYE YEYE HATA KAMA IMEJAA UTASIKIA ......."YAKUKAA HIYOOOO...BADO WAWILI....."
   
 8. J

  John10 JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini msiwe na usafiri wenu? msipende kutumia hela ya bure ya serikali kila wakati. sometimes mnatakiwa muwe independent ili mlete habari za kweli.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hi hi hi ,ha ha ha ha ha tuache utani hii habari inachekesha ingawa inasikitisha.mkome kujipendekeza kwa rais.........ina maana nyinyi magazeti yenu yote yana ofisi dar tu????????huko mliposema hakuna hadhi na kugumu kupata malazi ni tanzania pia ambapo watu wanahitaji waandishi wa habari ili waeleze matatizo yao yasikike......sasa nyinyi kwa akili fupi
  mkajiona na nynyi ni wahashemiwa...........ha ha ha shame on u??
  Hivi nani awafundishe kuwa priority yenu ya kwanza ni wananchi wanaopata tabu na sio hao wahashemiwa??????
  Mpande ndege kurudi dar ili iweje?????mkitumia basi si ndio vizuri zaidi mpate kuona mengi yanayowasibu watanzania?aliowatimua amewasaidia sana hamjui tu...............
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,216
  Likes Received: 5,615
  Trophy Points: 280
  Nilijua wanaodharaulika ni walimu kumbe na nyie wamo

  mh mwaya wenzenu tushawazoea hao..............
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,216
  Likes Received: 5,615
  Trophy Points: 280
  Siku nyingine msikimbizane nae hiyo ndio dawa ya mwihso kwa hawa mafisadi wa ikulu wanaohisi wamekamata maisha kushinda ikulu kuangalia tausi
   
 12. PoliteMsemakweli

  PoliteMsemakweli Member

  #12
  Sep 6, 2009
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mimi ninao ushauri...usilaumu Ikulu kwa hili... Msafara wa Rais sio mchezo bwana.. Kuna kuwa na watu kibao hasa huko Mikoani.. Nyie kama waandishi wa habari msitegemee kubebwa ama mtanunuliwa muandike habari za yule ambaye anawalipia.. Lazima muelewe kuwa sharti mjitegemeze wenyewe na msingojea fadhila za IKULU. IKULU ina kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa kuna usalama wa Rais na mambo ya kujua wandishi watalala wapi hilo kwao si priority..Wandishi jaribuni kujitegemea na amini kuwa katika uzoefu wenu mtaweza kuyathibiti mazingira ya safari ili mtuletee habari mbivu na sio za kupikwa!!!
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  1. Naungana na Phapo juu kuhusu waandishi wa habari kulinda objectivity kwa kuhakikisha wanajilipia, he who pays the piper, calls the tune.

  2. Waandishi hawajaanndika habari core iliyowapeleka, wameishia selfishly kuandika squabbles zao na Ikulu. Not to be a Kikwete apologist, lakini kwa nchi kama Tanzania waandishi hawa wameonyesha lack of prioritization.
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Sep 6, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mi nashindwa kuelewa hapa. Kwani ukiitwa kuandika matukio anayepaswa kugharamia safari yako ni nani? Kampuni yako ya habari iliyo kuhajiri au yule ambaye ametoa nafasi kwa waandishi kuwepo kwenye huo msafara?

  Kwa upeo wangu naona kuwa ukiwa wewe ni Mwandishi wa Habari na matukio na umehajiriwa kwa kazi ya kutafuta habari na matukio ili uje kuitaaarifu (kuuza habari kwa...) jamii husika... Je kampuni yako au shirika lako si ndio lenye kugharamia hiyo safari, tena basi naona kama wamepatiwa tip kwa kujuzwa kuwa kuna taarifa za kuandika maala fulani. Kwa hali hiyo walipaswa wao kwa njia moja ama nyingine kuchangia hiyo safari kwa kuwapatia masurufu ya safari hao wafanyakazi wao na si Ikulu kuwagharamia.

  Maofisa wa ilkulu wajibu wao ni kuhakikisha kuwa kuna waandishi wa mashirika binafsi na wanaruhusiwa kuandika kile kinacho jiri na si kuwagharamia malazi na chakula na mshiko wa gharama za kujikimu.

  Pili haya mashirika ya habari inabidi ifikie wakati wawatumia waandishi wawakilishi wa mikoani (kama wapo) kuwawakilisha na si kuwatumia wale wa makao makuu tu.... Waache ukiritimba.
   
 15. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Mahesabu unaonyesha jinsi gani ulivyokuwa huna akili... Eti unataka manifesto ya wasafiri katika msafara wa rais awe nayo rubani? unataka kuniambia rubani ndiye aliyewashusha hao waandishi baada ya kukosa majina yao? swali la pili, mahesabu unakumbuka kwamba hawa walikuwa wamefuatana na Raisi, ambaye alikwenda huko na gari, unauliza waandishi walikwenda na ndege mpaka warudi na ndege, je rais alienda na ndege?

  Inaonyesha Rais Kikwete amezunguukwa na watu wasioweza kufikiria hata itifaki ya wiki moja ya shughuri za rais ndani ya miaka minne sasa?

  Kuna mtu anatakiwa kuwajibika hapa.
   
 16. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Waandishi wa bongo wengi hua wanashangaza sana. Inaonesha baazi yao wanapenda hiyo kazi kwa kuzamia vitrip na pesa inayotolewa kwa style ya brown envelope tu,hakuna kingine. Wewe unafanya kazi shirika X leo umepewa tip kua kuna story mahali fulani,iweje source ya ile story akulipe? Kwa style hiyo utakua objective kweli? Si atakua kishakununua? Labda wengine hatuijui hiyo fani vizuri lakini huo ndio mwanzo wenu wa kudharaulika na jamii(including sources). Kuna kisa kimoja nilikiona pale Peakock hotel. Tulienda kwenye workshop fulani na waandishi wakapata tip huko wakaja kucover lile tukio. From no where muda wa msosi ilikuja tim ya waandishi kugombania sambusa mpaka wahusika wakuu wa ile workshop wakabaki pembeni wamedua wanashangaa kulikoni. Jamaa wako bize kula misosi badala ya kuandika. Mtindo huu umeshazoweleka sasa wanaona kama ni haki yao. Ndio maana wakifanyiwa inavyotakiwa wanaona wananyanyaswa. Wewe ulipwe na serikali kwani ni mwandishi wao? Kama unapenda such government trips fanya kwao, napo watakulipa endapo una umuhimu wa kwenda kwenye safari hiyo. Sometimes wanatumia waandishi wao wa mikoani kupunguza gharama. Kuwa na waandishi wa mikoani kuna maana gani kama nyie wa makao makuu mnaenda kwenye kila tukio ? Hizo night na perdiem ndizo zinazowaharibia heshima yenu. Achaneni na mambo ya brown envelope na favours zisizo za msingi kama kweli mnataka kua reliable reporters. Period!
   
 17. m

  mkulu Member

  #17
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  he he heeeh ..... wao wanalalamika mazingira mabovu ambayo wamekaa kwa siku moja tu, its funny ... hao wakazi wa huko je?wao ndio walipaswa kuripoti ugumu wa mazingira ya huko unavyowaathiri wananchi (wao wangejitolea mfano jinsi walivyopata tabu sio kuja hapa kulalamika ktk thread nzima) ila wao wanalalamika kuwekwa kwa mazingira hayo eti wamedhalilishwa. Je hao wanaokaa huko wamefanywa nini?Wanastahili?
  Kwa staili hii kama wangepewa kila kitu (na usafiri wa ndege,maana yaonesha walichukia kweli kufungua mikanda ya ndege ..) wangeandika lolote baya lile ambalo lingetokea huko?

  Ni mtazamo tu!......
   
 18. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #18
  Sep 7, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Get the story first and distance yourself from the people you cover. Some basic journalistic principles are lacking from this journalist. Unang'ang'ania kuandika yakwako kabla ya kutupa issues za kule ulikoenda kuandika story. The main problem here in TZ is that when journalists get a trip to cover some issue they call it a Vacation. That's why they put their personal interests at the forefront: posing for photos and spending in lucrative hotels. Is that responsible journalism? Nobody is warning them. They are emulating this from their brother(Michuzi) who brags going overseas and to various places within the country(posing with hands across peoples shoulders,including ladies). This has been a trend todate in this country. Now you should open eyes and rethink about your profession.
   
 19. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuniita jina zuri kama hilo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.....!
  hebu weka bayana unachotaka kuhalalisha.....!
   
 20. K

  Kaka Mdogo Member

  #20
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi siyo Mwandishi wa habari lakini kuna mchangiaji kaongea suala la msingi ambalo mtoa hoja angepaswa kujiuliza kwanza kabla ya kutoa hoja. Chombo cha habari kikipewa mwaliko kwa ajili ya ku cover shughuli fulani ina kinatakiwa kilipiwe gharama zake za hiyo coverage? This is the main issue. Kama Ikulu ilitakiwa kuwalipia, kuwapa chakula, malazi na usafiri, basi walidhalilishwa, kama Ikulu haikutakiwa basi wamejidhalilisha! period. Lakini cha msingi ni independence ya hawa waandishi wa habari au hicho chombo cha habari. Mkianza kulipiwa na kupanda ndege ya rais basi mnatakiwa kuwa subservient kwa serikali na rais wake.
  Lakini vilevile usalama wenu kama waandishi wa habari ni kwa kuuzingatia. Ni lazima mfanye mambo yenu kwa umakini. Mnaindika serikali na kuipinga wazi wazi lazima muwe makini kwamba hawatafanya lolote la kuwadhuru including kuwabambikia kesi za ajabu ajabu. Lingetokea tatizo kwenye ndege na wewe raia mwandishi wa habari umo huchelewi kuwa prime suspect kwa makusudi tu. Watch your actions and movements!
   
Loading...