Waandishi wa habari wajikaanga kwa mafuta yao, wasifiwa na jeshi la polisi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari wajikaanga kwa mafuta yao, wasifiwa na jeshi la polisi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Sep 22, 2012.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Maandamano yaliyofanywa na waandishi wa habari hivi karibuni, yamegeuka kuwa kejeli kutoka kwa jeshi la polisi,

  Polisi wamewasifu sana waandishi wa habari eti "kwa kuandamana kwa amani"
  polisi hao kwa kuonyesha wana ajenda mahsusi, wameenda mbali zaidi katika mwendelezo wa sifa zao, wamewaweka kundi moja na waandamanaji wa kiislamu, ambao japo walizuiwa na polisi, kwa kufanania zuio la nyololo, eti nao "waliandamana kwa amani"

  Nilitegemea kwenye maandamano ya waandishi wa habari, hotuba zao zingelenga kushinikiza kamuhanda afikishwe mahakamani kwa ushahidi walio nao, na wangeueleza umma kuwa wako tayari kutoa ushahidi kumuhusu kamanda kamuhanda alivyoshiriki kuuwa,
  kinyume chake "wameandamana kwa amani"

  Walijaribu kuonyesha hasira kidogo tu nchimbi alipojumuika kwenye maandamano yao bila kualikwa, nchimbi akajivika uso wa mbuzi, wakafanya mahojiano naye, dhumuni la jumuiko lake likakamilika kwa kuwafikishia ujumbe jonalisti pale jangwani.

  Jipangeni upya nawashauri, na mara hii mtake sio "muombe" Kamuhanda apandishwe kizimbani, mkisubiri ripoti ya kamati iliyoundwa ndio mjue kulindana kutakuwa wazi pasi na kificho, na kila ukijaribu kusema utaambiwa tume imechunguza kwa kina, na imebaini . . . . . .
  Kamuhanda hahusi...
  Pasco au ushahidi mzito kwa kamanda kamuhanda nyinyi waandishi wa habari hamna, na zile picha ni za photoshop?
  Waandishi mmejikaanga kwa mafuta yenu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tume sidhani kama italeta majibu ambayo watanzania wanataka, yatakuja yale yale amepigwa na kitu kizito.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa Smartboy,
  kwa majibu ya kamuhanda aliyoyatoa alipohojiwa na redio na kusisitiza hajiuzulu kwani alikuwa katika kutekeleza majukumu yake, inaonyesha ni nini tume imeenda kutuandalia "huko jikoni"
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. M

  MKALIMOTTO Senior Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha uchochezi mleta uzi. halafu nyie chama cha domokaya na maandamano msipende kutumia watu kwa maslahi yenu pum.........baaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaf@@2&
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kwenye red ulimaanisha Lipumba au? Manake nakumbuka aliwahi kumpa jk ilani ya uchaguzi ya cuf nadhani leo unaikumbushia, halafu mandojo na domokaya simsikii siku hizi, tupe habari zake!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,528
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jogi, kuhusu hili la waandishi na polisi, nilishatoa maoni yangu haya huko nyuma!


  [​IMG] By Pasco [​IMG]

  1. Waandishi wa habari waajiriwa, hawana jeuri ya kususia habari za kipolisi kwa sababu ni watumwa, huko kususa, ni hasira za uchungu, zikipoa, wataendelea kuandika!, Maggid yuko right!.

  2.Waandishi wa kujitegemea, tuko wa aina mbili, aina ya kwanza ni "freelance journalist", hawa wanaandika na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, newsroom nyingi zinalipa 3,000, 5,000 kwa habari moja itakayotoka, na labda 10,000 kama habari itakuwa ndio lead story!, huyu mwandishi akifanikiwa ku file story 1 tuu kwa siku na ikatoka, mwisho wa mwezi atavuta 90,000 tuu!. Waandishi wa kada hii ndio hutegemea "bahasha" to survive!.

  3. Kada ya pili ni "independent journalists", kada hii ndiko mimi niliko, inahusisha kuandika just for the love of it, wengi wa kada hii tunazo shughuli zetu za kufanya to make our living, hivyo hatutegemei malipo yoyote kwa stories tunazotuma, mfano mimi silipwi hata senti tano kwa stories ninazofile kwenye media. Kundi hili ndio kundi kama la kina Mjengwa, Mzee Mwanakijiji etc, etc, enzi zile Mwanakijiji akitoa kile kijarida cha Cheche, alikitoa bure nasi tulikitawanya bure!. Kwa sasa Mjengwa, Mwanakijiji na wengine, ni waandishi wa makala mbalimbali kwenye magazeti mbalimbali. Kwa kawaida magazeti yanapaswa kuwalipa, sidhani kama wanaandika ili kujipatia hivyo vijisenti na I doubt hata kama wanachukua!. Kundi hili ndilo hatutumwi na mtu na hatumtumikii mtu zaidi ya jamii!.

  5. Mwisho bado naendelea kulia na tatizo kubwa humu jukwaani, watu wengi humu tuna tatizo la kuukubali ukweli halisi baina ya "is" and "ought". Mjengwa ni mkweli wa "is" and so do I, wengi humu ukweli wenu mnaoukubali ni "ought" ambao sio ukweli halisi!. Nikukumnbushe mifano michache.


  • Habari za kipolisi ni habari za jamii, kuzisusia ni kuinyima jamii haki ya kupata habari, mwandishi makini, anaweza kwenda polisi na kuripoti habari za kipolisi kwa angle ya jamii bila kuwapa promo polisi, na bado kuitumikia jamii. Habari za kipolisi ni ukweli wa "is" na kususia ni "ought"!.


  Pasco.  Pia niliongelea kwa kirefu, kwa nini waandishi hawawezi kususia habari za kipolisi!.

  [​IMG] By Pasco [​IMG]

  1. Kisuso cha waandishi, sio kisuso cha kweli, ni kisuso cha hasira na uchungu wa kufiwa, siku zikipita, uchungu utapungua, hasira zitapungua na kwa RPC waandishi wataripoti!.

  2. Wengi wa waandishi ni watumwa tuu, hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kwa utashi wa editor na edotors ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki "he who pays the piper may call the tune"!.

  ila mimi kama Pasco wa JF, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, kama ni gazeti, huamua gazeti gani nipeleke, au kama ni kwenye TV na redio, mimi mwenyewe ndio huamua pa kuipeleka!, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli kweli!, hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote sio za kipolisi tuu, ni wale tuu ambao sio "watumwa" yaani wale waandishi wanaojitegemea na sio hawa "watumwa" wanaotegemea vyombo vya habari!.

   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Pasco, nashukuru kwa response na nukuu uliyoiweka, ni msimamo unaoungika mkono. Ambacho sijafanikiwa kukiona kwenye nukuu yako ni kile nichokigusia kwenye maelezo ya uzi huu.

  Malengo ya maandamano yamekwenda harijojo, kulaani ulikuwa ni wajibu wa kwanza, lakini mlikuwa na cha zaidi kama wanafamilia ya wanahabari, ushahidi dhidi ya kaumuhanda mnao, kwa umoja wenu pale jangwani mngepaaza sauti zenu ili, kwa ushahidi mlionao, kamuhanda avuliwe vyeo, apandishwe kizimbani kujibu shitaka la mauaji ya mwangosi sambamba na wale askari wengine wanaoonekana dhahiri kwenye picha mnato na video.

  Hapo namaanisha tuhuma za jamii kwa kamuhanda & co. Ingebidi serikali izisikilize kwa uzito wa pekee kilio hiki na ingepunguza kama si kuondoa kabisa pilikapilika za kumsafisha kamuhanda & co.

  Ndiyo maana waandishi wa habari mmekuwa sehemu ya propaganda ya ccm kupitia jeshi la polisi kwamba wanaoweza kuandamana kwa amani ni
  1. Wanahabari.
  2. Waislamu.
  3. ccm

  Na kutoa nafasi kwa jeshi la polisi kutetea mauaji wanayoyafanya kwa kusingizia kutekeleza uhifadhi wa amani ingawa ni kwa kuvunja katiba.
  Paazeni sauti zenu kitaaluma muieleze jamii ni kwa jinsi gani haki yao ya kuishi ilivyo hatarini mikononi mwa polisi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. MLUGURU

  MLUGURU JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 818
  Likes Received: 385
  Trophy Points: 80
  wajumbe wa mct aka baraza la habari lapata safari kwenda nje kujifunza zaid!!!!!!!:A S shade::A S shade::A S shade:
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  wanapelekwa na nani.
   
 10. MLUGURU

  MLUGURU JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 818
  Likes Received: 385
  Trophy Points: 80
  wizara ya habari ikishirikiana na mct mkuu
   
 11. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jogi tunakuteua uwe msimamizi wa waandishi wa habari. Jukumu lako liwe hilo uliloainisha kama kasoro. Tunakusubiri mzee.
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mkuu kazikubwa, wataniuliza vyeti vya Tsj, hapo nitakwama, lakini ikiwa utawauliza wakakuhakikishia kutoa ushirikiano, maandamano ya kwanza tutaandamana kwa amani kuanzia saa moja asubuhi kutokea makao makuu ya dstv tutakuja salender, united nation road, morogoro road hadi jangwani, njiani tutagawa vipeperushi kwa yeyote tutakayekutana naye, tutawahoji na kurusha live mpango mzima kabla ya kuhitimisha andamano kwa kumtaka mwendesha mashtaka kumuunganisha kamuhanda kwenye mashtaka ya mauaji ya mwangosi katika muda usiozidi siku saba. Kinyume chake tutaitisha maandamano ya "kelele" kujumlisha wananchi. Kelele lengo lake ni kuwa ikiwa igp + Feleshi masikio yao yameziba, basi kelele ziyazibue, kelele zitahusisha honi za magari, kugonganisha makopo, vijiko, nyuma, sahani za bati kupiga miluzi, kuzomea n.k kwa masaa matatu matakatifu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...