Waandishi wa Habari waaibishwa kutoripoti uwanja wa ndege wa Katavi kuota nyasi na mmliki wa ambulance zilizokamatwa bandarini

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
296
507
Uandishi wa uhakika huwezi kuwa rafiki na Mamlaka, Kuna siku moja Trump alikuwa anaishambulia CNN kwa Twitter kuwa badala ya kuitangaza vizuri Marekani na miradi yake ya kiuchumi chombo hicho kimekazana kupambana na Utendaji wa Rais na proganda zingine.

Muda huo huo CNN wakamjibu Tena kwa kumtag kwenye Twitter (Sio kazi yetu kuitangaza vizuri Marekani Duniani hiyo ni kazi ya Rais na serikali yake kazi yetu ni kuripoti na kuandika UKWELI TU)

Tanzania Tundu Lissu alidanganya Umma kuwa Katavi Ndege haziji na uwanja umeota nyasi badala ya Wandishi kwenda uwanjani kuripoti, walisubiri mpaka Mkuu wa mkoa alipoenda.

Rais wa Tanzania Hayati Magufuli katika mapambano ya ufisadi Kuna viambulensi vilikamatwa Bandari ya Dar, baadaye tukaanza kupishana navyo halmashauri hakuna aliye hoji kulikoni? Vilikuwa vya Nani Kama vimetaifishwa sawa kutoka kwa Nani? Leo nimeangalia TBC taarifa ya habari sukari guru imekamatwa ni yatangu 2019 kontena tano je Nani ana miliki?

Kwanini Sukari imekaa tangu 2019 bandarini mpaka imeharibika Nini kilitokea?
 
Tanzania kwa kipindi hiki hakuna waandishi wa habari, kuna waimba mapambio tu, hivi mtu kama Musiba ndio anajiita eti muandishi wa Habari, are you seriuos? hakuna analysis hakuna uchambuzi na udadavuzi wa kina wamebaki kusifiana tu ili mradi mkono uende kinywani, taaluma hii imelawitiwa sana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, believe me.
 
Hiyo habari ya kuwa kontena mwenye nazo hajulikani hajitokeze ni uongo.

Kontena kabla ya kusafirishwa melini lilipotoka walitengeneza Bill of Lading (Risiti ya mzigo) ambayo inaonyesha mzigo umetoka wapi,tarehe ya kupakia,mzigo unapoenda, idadi ya mzigo, mmiliki wa mzigo na nani atakayepokea kwa niaba ya mmiliki(notify part ambapo anakuwa ni clearing agent mwenye mzigo na address yake inawekwa).

Hapo mwenye kontena anajulikana direct wamfuate wamwambie afanye taratibu zake.
 
Njaa, njaa, njaaaa, achana na media houses ambazo ziliamua kupuliza moto ili mapishi yawahi kuiva ila waandishi ni njaa 'narudia' njaa.

Huwezi kumuandika vibaya anayekupa mkate, mwandishi amebaki kupambana na mwandishi na kuacha kufanya/kuandika habari kama hizo.

Tasnia imekosa wenye weledi japokuwa uandishi wa Tanzania ni wa hofu ila hofu isiwe sababu ya kushidwa kusema ukweli, wachache wanaelewa na wengi ni njaa kali.
 
Taifa letu bado halijawa na uhuru walionao wamarekani, huku tunalazimishwa kuwa wazalendo lazima uisifie CCM, japo ni kweli waandishi wetu wengi ni makanjanja.
Mkuu, ungeelezea nini kifanyike ili kuondokana na hii Mambo.
 
Tanzania kwa kipindi hiki hakuna waandishi wa habari, kuna waimba mapambio tu, hivi mtu kama Musiba ndio anajiita eti muandishi wa Habari, are you seriuos? hakuna analysis hakuna uchambuzi na udadavuzi wa kina wamebaki kusifiana tu ili mradi mkono uende kinywani, taaluma hii imelawitiwa sana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, believe me.
Duh...!.
P
 
Na siyo waandishi wa habari tu, ebu fuatailia kinachoendelea BASATA na wasanii.

Yaani ubunifu kwasasa katika utendaji fanyia chumbani kwako huku nje tunataka kile TUNACHOKIONA kipo sawa na SIYO kutuambia sisi na elimu zetu hatujui.

Hii nchi bado tuna safari ndefu Mungu saidia.
 
Uandishi wa uhakika huwezi kuwa rafiki na Mamlaka, Kuna siku moja Trump alikuwa anaishambulia CNN kwa Twitter kuwa badala ya kuitangaza vizuri Marekani na miradi yake ya kiuchumi chombo hicho kimekazana kupambana na Utendaji wa Rais na proganda zingine.

Muda huo huo CNN wakamjibu Tena kwa kumtag kwenye Twitter (Sio kazi yetu kuitangaza vizuri Marekani Duniani hiyo ni kazi ya Rais na serikali yake kazi yetu ni kuripoti na kuandika UKWELI TU)

Tanzania Tundu Lissu alidanganya Umma kuwa Katavi Ndege haziji na uwanja umeota nyasi badala ya Wandishi kwenda uwanjani kuripoti, walisubiri mpaka Mkuu wa mkoa alipoenda.

Rais wa Tanzania Hayati Magufuli katika mapambano ya ufisadi Kuna viambulensi vilikamatwa Bandari ya Dar, baadaye tukaanza kupishana navyo halmashauri hakuna aliye hoji kulikoni? Vilikuwa vya Nani Kama vimetaifishwa sawa kutoka kwa Nani? Leo nimeangalia TBC taarifa ya habari sukari guru imekamatwa ni yatangu 2019 kontena tano je Nani ana miliki?

Kwanini Sukari imekaa tangu 2019 bandarini mpaka imeharibika Nini kilitokea?
Siyo contena 5 mkuu. Ni 500 kwa mujibu wa bwana Jaffo. Usisahau magari yaliyowahi kukamatwa hapo bandarini kwenye container sijui yalikuwa ya nani?
Mtu mweusi haishiwi vitimbwi!?
 
Na siyo waandishi wa habari tu, ebu fuatailia kinachoendelea BASATA na wasanii.

Yaani ubunifu kwasasa katika utendaji fanyia chumbani kwako huku nje tunataka kile TUNACHOKIONA kipo sawa na SIYO kutuambia sisi na elimu zetu hatujui.

Hii nchi bado tuna safari ndefu Mungu saidia.
Kabisa
 
Uandishi wa uhakika huwezi kuwa rafiki na Mamlaka, Kuna siku moja Trump alikuwa anaishambulia CNN kwa Twitter kuwa badala ya kuitangaza vizuri Marekani na miradi yake ya kiuchumi chombo hicho kimekazana kupambana na Utendaji wa Rais na proganda zingine.

Muda huo huo CNN wakamjibu Tena kwa kumtag kwenye Twitter (Sio kazi yetu kuitangaza vizuri Marekani Duniani hiyo ni kazi ya Rais na serikali yake kazi yetu ni kuripoti na kuandika UKWELI TU)

Tanzania Tundu Lissu alidanganya Umma kuwa Katavi Ndege haziji na uwanja umeota nyasi badala ya Wandishi kwenda uwanjani kuripoti, walisubiri mpaka Mkuu wa mkoa alipoenda.

Rais wa Tanzania Hayati Magufuli katika mapambano ya ufisadi Kuna viambulensi vilikamatwa Bandari ya Dar, baadaye tukaanza kupishana navyo halmashauri hakuna aliye hoji kulikoni? Vilikuwa vya Nani Kama vimetaifishwa sawa kutoka kwa Nani? Leo nimeangalia TBC taarifa ya habari sukari guru imekamatwa ni yatangu 2019 kontena tano je Nani ana miliki?

Kwanini Sukari imekaa tangu 2019 bandarini mpaka imeharibika Nini kilitokea?
Mabaki ya utawala dhalimu uliopita mtasikia mengi.
 
Kati ya tasnia zilizokosa kabisa weledi, mojawapo ni uandishi wa habari wa Tanzania. Kuke wamejaa waganga njaa. Aheri uje JF utapata habari za uhakika kuliko kununua gazeti au kuangalua TV.

Kutokana na ukanjanja, ndiyo maana, mara nyingi viongozi wa Serikali wamekuwa wakiwachezesha kama wanavyotaka, kwa sababu wanaujua udhaifu wao.

Ukiwa na bahasha iliyoshiba, unaweza kuwaita na ukawaambia cha kuandika au kutangaza.
 
Back
Top Bottom