Waandishi wa habari wa Tz nani kawaloga, hamuoni aibu?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari wa Tz nani kawaloga, hamuoni aibu??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by figganigga, Nov 30, 2011.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  Heshima yenu JF.Hadi sasa nashindwa kujua wandishi wa habari wa Tanzania wanawaza kwa kutumia nini. Waandishi wa habari wapo kila pembe ya nchi yetu lakini bado wanaogopa kuongea ukweli wa jamii inayo wazunguka. TUMETHUBUTU TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE KWELI..?? Vijijini hamna huduma muhimu, mali asili zinanufaisha wageni, Mafisadi wana nenepa sisi tunakonda, udini, ukabila, maradhi hamuoni? Kwanini hamuongei ukweli?. Amani Isiwe MRIJA wa kutunyonyea na kutupumbaza. Ongeeni ukweli. Miaka 50=5.Mia
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  hali ni mbaya,
  barabara kubwa kama ya kwenda arusha ni mbovu haifai
  vijumba vilivyoko kando kando ya barabara ni aibu unaona kabisa
  mtu anayeishi humo ndani ana njaa,
  je huko mikoa ya pembezoni kukoje.
  waandishi wa habari hakuna, kuna waganga njaa tu.
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwani waandishi wa habari ndiyo CCM? Naona mmeshindwa kuilaumu serikali mnaamua kuhamia kwa waandishi wa habari. Mwandishi ana makosa gani kuhusiana na barabara mbaya ya Arusha?
   
 4. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,223
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  wajinga sana wamerongwa na wamiliki wao

  tatizo uoga kaka!! kila mwandishi anategemea sh 150,000 anayolipwa kwa mwezi hana kipato kingine chochote so lazima aseme atavyoambiwa!!

  wengine umbea/upashkuna/ulimbukeni/ uongo/ ili waonekane marafiki wa serikali au marafiki wa kundi flan la watu

  a good example ni hawa CLAUD FM ambao hawana chamaana wanachofanya zaidi ya upashkuna na umbea

  sidhan kama kuna mtu mzima mwenye akili timamu anayesikiliza clauds

  amina
   
 5. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Hoja zenu ni nzuri lakini mmeziwasilisha vibaya kwa kutumia tuhuma bila kujua tatizo la msingi.
  Kumbuka nchi yetu ina tatizo la kimfumo kuanzia kwa nchi,wananchi wake nk wakiwemo nyinyi.
  Ebu nieleze FANI yako wewe imesaidiaje nchi katika kipindi hicho ili baadaye tuwajadili waandishi.

  Hatuwezi kukataa kumjadili aliyejisaidia ndani ya chumba na sababu za kufanya ivyo badala yake tutajili aliyekataa kusema kwamba kuna uchafu na aliyeshindwa kuondoa uchafu huo katika chumba .

  Mnapojadili jambo lolote,kwanza tafuta msingi wake.
  unaweza kukuta mtu anajadili umaskini wakati yeye mwenyewe anatumia zaidi ya sh 100,000 kuwekeza tumboni kwa kunywa tu bila kuwekeza jambo la maana.
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  waandishi wetu ni watu wa kitu kidogo,wao na Redio fulani hapa nchini wanafanana sana
  wapo wachache wenye kudhubutu na kusema lakini ni wachache sana ukilinganisha na uwingi wao

  hatuwezi kujapata waanahabari kama kina Jri Muro,Kubenea na wenzake

  nawapenda sana wanahabari wa Kenya hususani KTN, wao hawamwangalii nyani usoni

  kwenye ukweli watasema na kukupongeza na penye mapungufu watasema

  lakini hapa kwetu ni tofauti sana na hii inatokana na wanahabari wetu kufanya kazi hii kwa kuangalia kipato zaidi na sio hudumu
  hatukatai kutafuta pesa lakini sio kwa mtindo wa kutosema hata yale yanayokugusa mwenyewe
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mhhhhhhhhhhh
  hivi hawa jamaa hawana kioo cha kujiona? mbona kila mtu anawasema wao tu? bora ingekuwa unasemwa kwa mazuri basi
   
 8. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  Byabato, mimi nakubaliana na wewe, lakini kwanini munashindwa kuongea ukweli? mimi nawalaumu wandishi wa habari kwa sababu wao ndo wanasehemu ya kusemea maovu tofauti na sekta nyingine. CCM wanaona wameshindwa so wanatafuta maneno ya kuongea ili wapate uhalali wa kuendelea kututawala. TUMETHUBUTU TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE ni kauli yenye kupambwa ya kisiasa iliyo asisiwa na CCM kama chama tawala. sasa kwanini mnasimamia kauli za kisiasa kuliko hali halisi iliyopo? samahani lakini. naomba ufafanuzi. Mia
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  waandike waseme ili isikike,labda ipo siku mtasikia maana waswahili wanasema kimya cha mwandishi ni kabaya zaidi kuliko kelele za mama mwenye nyumba
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na ndio maana kuna mgawanyo wa kazi
  kwa sasa tupo na waandishi wa habari,kwanini mnashindwa kusema ukweli hata ktk kile kinacho wahusu? mbona hamtumii pen zenu kuwaeleza wakuu ukweli wa mambo ama hata sisi wananchi?

  Tena nisikilize na nisome vyema mkuu

  hivi huwa unaangalia KTN kuna habari inaitwa untouchable(jicho pevu) umeona ujasili wa wale waandishi?

  mbona mambo haya yapo hapa Tz tena pale Moro,lakini waaaaaaaaaapi hamtaki kuumbua watu

  inakuwaje mnafanya kazi kwa matakwa ya kuwalidhisha watu wakati hata nyinyi wenyewe kama waandishi mnaumia

  sija mwona mwandishi wa tz aliyekuja na habari za kiuchunguzi ukiachana na bwana muro

  tubadilike na tufanye kazi kama tasnia ya habari inavyotaka,tuache ukanjanja
   
 11. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni njaa. Mwandishi naye ana njaa, hata wewe ukimpa 'kishawishi' aandike figganigga ni chaguo la mungu 2015, ataandika tu!

  [​IMG]
  Il Gambino
   
 12. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  Wanapo fanya hivyo wanakuwa wanatunyima haki ya kusikika sisi wananchi. Mimi nawaomba wabadilike sababu nchi inako elekea lawama juu ya waandishi wa habari. Mia
   
 13. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #13
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Sikiliza mkuu
  Sitaki kuonekenana natetea waandishi wa TZ hapana.Lakini nataka kuelewesha kwamba tatizo unaloliona hapa likiwa tofauti na wenzetu kenya mfano yule mwandishi Mohamed Ally wa Jicho Pevu(natazama sana uchunguzi ule) ni kwamba kuna mambo mengi yanayosababisha uandishi wa hapa ukose mashiko.kuna mambo mengi sana ambayo ukweli hauwezi kufanya journalism kama unavyodai KTN,NTV au ALJAZEERA ya mashariki ya kati.naomba nikutajie tu kwa ufupi vitu 2,mengine siku nyingine.

  1.SHERIA
  Kama unafuatilia kipindi hicho cha JICHO PEVU utakubalina nami kuwa yule mwandishi anachunguza huku akishirikiana na vyombo vya dola kwa kuwa sehemu nyingine anakamata kabisa wahusika akiwa na polisi lakini katika makala zake anakuwa balanced.

  Kwa tz ni vigumu kufanyika.Mchoro wa kile kipindi(script) huwezi kukifanya hapa Bongo.Tazama Muro alikuwa na kipindi kizuri lakini nacho mchoro wake ulikuwa mbovu kwani huwezi kumchunguza mtu asubuhi jioni unamuta kwenye kipindi tena live,una-play tape na kumuuliza maswali(kama alivyofanya kwa Msika) wanaojua walijua kuwa kipindi hicho hakitadumu kwa TZ.

  2.UWEZO WA VYOMBO VYENYEWE.

  Elewa kuwa mtaji wa vyombo hivi vya habari TZ unatofautina,sana na Kenya Mfano KTN na Aljazeera pamoja na weledi,mifumo ya vyuo na sheria zinazofanya kupatikana kwa waandishi zinatofatiana sana.

  Hivi unajua kuwa asilimia 80 ya matangazo yanayoendesha vyombo hivi yanatoka Serikalini?.Hata magazeti unayoyaheshimu kwa sasa It is the matter of time ! hutayasikia tena.mitaji hawana.
  Je huyo mwandishi anayefanya uchunguzi mnaoutaka kama KTN ana bima? analipwa sh ngapi kwa mwezi ?akiongwa sh milioni 2 ili aache ataikataa ili kulinda heshima na maadili ?nk.

  Muro amesota zaidi ya mwaka mzima kwa kesi ya Uongo kisa alitetea maslahi ya wananchi mbona sijaona kikundi kinachoandamana kumtetea Muro.aliyofanya ilikuwa ni maslahi ya nani?,amepata nini?,Je atarudia tena? kwa faida ya nani(thawabu mbinguni ?) .Ebu tuume na kupuliza !
   
 14. MERCIFUL

  MERCIFUL JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,471
  Likes Received: 746
  Trophy Points: 280
  Mathias Byabato: Nimekusoma na kukuelewa fika. Lakini bado ukweli unabaki pale pale...waandishi wetu hawatutendei haki Watanzania. Pamoja na hayo yoote uliyoainisha, haimaanishi kuwa tukae kimya na kukubaliana na hio hali. Kwamba Polisi wetu ni hovyo basi na waandishi nao wana haki ya kuachiwa waharibu?!!! Wao ndio wana nafasi ya kusikika kuliko taaluma zingine zote; and YES, if they DARE, changes will happen....with/without the sophisticated technologies that others countries have. Hatuombi watuonyeshe hi-tech news..La Hasha....Watumie hizo hizo kalamu na peni zao kufikisha ujumbe na kwa jinsi ile ile wanavyo-cover habari ambazo mara nyingi hazina tija kwa watazamaji!!
   
 15. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  bravo mkuu!
   
Loading...