Waandishi wa Habari wa sasa wamekosa Weledi na Ufanisi katika kazi yao ya Uandishi

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,180
12,651
Sitoweza kutengua kauli yangu hiyo hata niwekewe upanga shingoni kutokana na habari zinazoandikwa nakurushwa ili watu wasome nakusikia.

A.Alykum wananzengo hakika Kristo ni tumaini letu na Mwenyezimungu atupe nguvu na pumzi yakupambania majukumu yetu yakutafuta mkate wa kila siku.

Naam, twende moja kwa moja kwenye pointi kama kichwa habari kinavyojieleza nisikuchoshe.

Kuna habari imekuwa ikizagaa sana kwenye mitandao pamoja na vyombo vikubwa vya online tv na kwenye magazeti yenye kichwa cha habari kinachosema nanukuu; "Aliyekuwa mchezaji wa Yanga zamani anauza mishikaki."

Kiukweli nilishangazwa sana na hii habari na nikapata maswali mengi kichwani lakini majibu yake ni kuwa waandishi wamekosa weledi katika kazi yao.

Nini lengo lakuandika hii habari? Sasa kama alicheza Yanga au Simba asifanye biashara? Je, mnataka afanye nini baada yakustaafu mpira, ajifiche ndani au? Kwani hiyo biashara ya mishikaki wachezaji waliostaafu hawatakiwi kufanya?

Nimefuatilia habari kuisikiliza nakuisoma sikuona conclusion yoyote inayotolewa na waandishi mwisho wa siku ikaja kuwa ni suala la ushabiki wa Simba na Yanga.

Enyi waandishi tafakarini hizo habari kabla yakuzipeleka kwa wasomaji, siyo mnaandika taka taka zisizo na manufaa mwisho wa siku inakua kama kumdhalilisha mtu nakumfedhehesha kwani yeye ni wa kwanza kufanya hiyo biashara ya mishikaki na mbona hamkuwatafuta wauza mishikaki wengine mkawahoji ila mlipo sikia kachezea Yanga ndiyo ikawa ni habari kubwa kwenu?

Tumieni vizuri taaluma zenu ila mkitumia mihemuko ipo siku tutakuta mmeandika; "Shabiki wa Yanga akutwa akila ugali na maharage."
 
Screenshot_20230308-130935.jpg
 
Back
Top Bottom