Waandishi wa habari wa namna hii kweli mnazingatia taaluma yenu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari wa namna hii kweli mnazingatia taaluma yenu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nyabibuye, Jan 21, 2012.

 1. nyabibuye

  nyabibuye Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nimeshindwa kufahamu kama hii taaluma ya habari nayo imevamiwa awali nilifahamu kuwa mhimili huu wa habari kama ambavo binafsi napenda kuutambua uanaowadau waliobobea katika taaluma zao lakini kumbe sasa naanzakuona mambo sivo.

  Gazeti la Tanzania Daima mwanzoni mwa wikii hii lilichapisha habari iliyosomeka "WALIOFUKUZWA UDSM WAMEVUNA KILICHOPANDWA" sinashida na kutolewa kwa habari ile lakini je mwandishi ulifanyia uchunguzi habari uliyoandika au uliandika kwa vile ulisukumwa na msukumo fulani!, hivi ni kweli ulishindwa haata kuzitafuta hizo taratibu na sheria unazodai viongozi wa serikali ya daruso wamekiuka? Binafsi ninajua unayoelimu ya taaluma lakinikwa hili umeidhalilisha taaluma yako wewe binafsi na mwajiri wako kwa vile sina hakika kama ulitumia maadili yanayokuongoza kufanya vile !

  Kwa kifupi kilichofanywa na serilkali ya wanafunzi wa DARUSO ni jambo halali na uhalali huo unatoka kwenye katiba ya wanafunzi wenyewe, kwanza ili kikao cha bunge la wanafunzi kiwe halali ni lazima mambo yafuatayo yakamilike : mosi, kikao kiwe kwenye kalenda ya chuo na ilikiua hivo, pili, bunge la daruso lipate kibali kutoka utawala wa chuo na kibari hicho kilitolewa na makamu mkuu wa chuo anayeshughulikia utawala (nakala ipo nadhani mwandishi ungeomba kujiridhisha na hini kabla hujaandika chochote) tatu, ni lazima tupewe mwakilishi kutoka hukohuko utawala wa chuo naye pia tulipatiwa,nne ulinzi ambao nao pia tulipatiwa.

  Idadi ya wabunge ambao wanatakiwa kuhudhulia ili kikao kiweze kuanza ni theluthi moja ya wabunge wote nao pia walitimia. kwa ujumla taratibu zote zilifuatwa na kikao kilikuwa ni halali sasa kosa la hawa viongozi wa DARUSO NI NINI na kwanini baadhi ya waandishi mnashindwa kutafuta hizi habari badala yake mnazipotosha mchango wenu katika jamii ni nini haswa.

  Daruso inayo katiba, imepitishwa na watawala hawahawa leo unataka serikali yao itetee maslahi yako mtawala wakati unajua ni kinyume? mbona na hawa wanaotoa hizi habari hawafuatili matatizo katika jamii kwa makini mkaifahamisha jamii uozo huu bali mnakua ni sehemu ya kuendeleza uozo huu?

  Je kanuni za wizara ya elimu zinatoa adhabu gani kama serikali ya wanafunzi wa elimu ya juu imekiuka sheria ya nchi au sheria yeyote? hili jambo ni la kufaanya utafiti ukasoma na kuelewa kinachotakiwa ni nini na haya ni mambo ya kisheria hayawezi kuendeshwa kisiasa, mwisho wa siku mwandishi kama huyu anajionaje anavofanya upuuzi katika taaluma yake we ungekua ni Dakitari si ungepasuaa mgonjwa kicwa badala ya mguu unaonaje kama elimu yako inawalakini ukaachana na hii kazi kwa sababu huna uwezo wa KUTAFUTA HABARI au hukuelewa maana ya kutafuta habari na kuzifanyia uchunguzi.

  KIMSINGI UMEBOA NA HIZI SIASA UNAZOTUMIWA NAZO NI CHAFU NINGEKUONA MTUU WA MAANA KAMA UNGEMWAMBIA BOSI WAKO AKATATUA MATATIZO BADALA YA KUUNGANA NAYE KATIKA VISINGIZIO KUMBUKA HII TANZANIA SIYO ILE YA MIAKA HAMSINI ILIYOPITA. jirekebisheni na muombe radhi tutakutafuta tukuhakikishie kwamba ulichoandika hakimo kwenye maadili ya kazi yako na wala hukufanya uchunguzi wowote ulikulupuka, ushahidi tutakupatia na hii DARUSO si jui utafanya nini nao! Asante kwa kutokua makini.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wewe mwenyewe una matatizo makubwa zaidi ya hao waandishi unaweza kusema ukasikilizwa ? Hebu angalia ulicho andika kweli unajua kuandika au umetokea shule za kata ?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Halafu yake hiyo habari anayolalamikiwa ilikuwa na makala tu ya maoni binafsi ya Happyness Katabazi na siyo stori ya habari ya ya Gazeti.
   
 4. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu alienzisha Topic hii amefanya makusudi au alikuwa hajui kuwa hilo gazeti analolikosoa linamilikiwa na chama cha wanajeshi walioasi kambi(wavaa magandwa wa uraiani).Kwa taarifa yako hawa watu hawajui neno kukosea na wanapenda kusifiwa tu.Haya bwana umewachokoza subiri mashambulizi.Kuwa mvumilivu usikimbilie kwa JF MODERATOR.
   
 5. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hee! Wenyewe saa hizi wapo kwenye mchaka mchaka, subiri wamalize shughuli utawaona hapa. Utakula mabuti na matusi juu! Hawa ni zaidi ya mgambo wa jiji. Waulize FFU na JKT wa kule Mbeya walivyopigishwa kwata usiku kucha na magwanda mpaka wakasalimu amri..
   
Loading...