Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari wanaJF,
Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu tunafuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye vyombo vya habari hasa magazeti kuhusu mkataba wa "Lugumi".
Mimi binafsi naona sakata hili linaweza kupoteza maana hata kama lina maana kubwa nyuma yake kutokana na jambo lenyewe linavyobeba sura ya propaganda hata kama haikuwa propaganda.
Hivi Waandishi wa habari mnashindwa nini kutuletea habari iliyo na vitu hivi juu ya huo mkataba?
1: Nyaraka zinazoonesha umiliki wa Kitwanga wa kampuni ya Infosys
2: Nyaraka zinazoonesha uhusika wa Infosys katika huo mkataba na hasa wao walitakiwa kufanya nini, na walipewa mkataba na nani? Je, kazi yao waliitimiza au hawakuitimiza?
3: Mkataba unasemaje juu ya muda wa kukamilika kazi yenyewe
Hapa najaribu kuwaza tu; Infosys inasemwa kumilikiwa na watu wawili, Mkurungenzi wa NIDA na Kitwanga. Mbona Kitwanga zaidi ndiye anayetajwa sana kuliko jamaa wa NIDA?!