Waandishi wa habari vs wamiliki wa habari

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,910
5,082
Ukijaribu kuvaa viatu vya wanahabari utahisi visivyokuwa vya kawaida ila wao wamelala hawana Habari.

Ukiangalia miondo ya vyama na malengo ya vyama vya wafanyakazi utaona kuwa ni ngumu sana wamiliki na wafanyakazi wao kuwa na mtizamo mmoja. wafanyakazi kwa umoja wao huungana kudai masilahi bora na mazingira bora ya kazi, kwa upande wa wamiliki vitu hivo hawavikubali kwa hiari Mara nyingi.

Waandishi wa Habari kwa upande wao naamini wana matatizo ya masilahi na mazingira ya kazi kama zilivyo kada zingine za ajira, lakini katika maajabu sijawahi kuwasikia wakidai masilahi yao!! Je hii ina maana gani?

1. Wanaishi kwa kutegemea bahasha kutoka huku na huko?
2. Hawajiamini au niwaoga wakupindukia?
3. Elimu feki au vyeti feki.

Waandishi/wanahabari wamekuwa wa kwanza kurukia vitu vinavyowahusu wamiliki! je huku sio kujipendekeza ilihali wao nao wana matatizo yao?

Kikulacho kinguoni mwako. tatizo hapa linaonekana liko kwa vyama vyao.
wito.

Waziri wa Habari tunakuomba sana ushughulikie hili suala vinginevyo watumiaji wa Habari tutalishwa sumu na tutakufa.
chondechonde MWAKYEMBE.
 
Ni ni hatari kazi hii zamani nayo ilikuwa WITO kama ualimu.SIKU HIZI LETE BAHASHA NIKUPIKIE HABARI TAAAAAAAAAAAAAAAAAAAMU
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Ni ni hatari kazi hii zamani nayo ilikuwa WITO kama ualimu.SIKU HIZI LETE BAHASHA NIKUPIKIE HABARI TAAAAAAAAAAAAAAAAAAAMU
yani maisha ya ujanjaujanja yanaanzia kwa wanahabari
 
Back
Top Bottom