Waandishi wa habari uhuru gani zaidi ya huu??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari uhuru gani zaidi ya huu???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpunumpunyenye, Sep 12, 2012.

 1. m

  mpunumpunyenye Senior Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Nasikitishwa sana na mfumo wa waandishi wa habari wa tanzania kwa vitendo vyao viovu vya kupiga makelele kudai uhuru wa kupata na kutoa habari, swali nauliza ni uhuru gani mnaodai zaidi ya huu mlionao??
  Nauliza hivyo kwa sababu waandishi wa habari wa tanzania wapo huru kuandika habari kuliko nchi zote duniani, nasema hivyo nnayo sababu, maana tanzania kwenye magazeti wanaandika hadi habari za ikulu, usalama wa taifa, za watu binafsi, akaunti za watu mwasasiliano binafsi ya watu siri za serikali kwenye magazeti yao ambavyo ni kinyume na maadili ya uandishi wa habari,
  imefikia mpaka mtu anaandika habari yoyote kwa maslahi anayoyajua yeye mwenyewe bila kuangalia madhara yake kwa jamii. Mjitafakuri kwanza na mjipime.
   

  Attached Files:

 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  awali una swali la kujiuliza kwa nini kuna mvutano wa sheria mpya ya vyombo vya habari ??

  hapa waandishi walalamikia mauaji ya mwandishi mwenzao kwamba kwa mauaji hayo ni sawa na kuwaziba mdomo ili wawe na hofu kubwa ktk kuripoti habari hasa za siasa na hususani CHADEMA

  KI UKWELI AWAMU HII INA UHURU MKUBWA SANA WA UPATIKANAJI WA HABARI pamoja na hilo tunalo elekea kunaonesha wakubwa wameishiwa uvumilivu ndiyo maana 1. Mwanahalisi limefungiwa 2. Daudi Mwangosi kauawa
   
 3. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  "waandishi wa habari wa tanzania wapo huru kuandika habari kuliko nchi zote duniani". Sina uhakika na utafiti wako! Kama wana uhuru huo, kwanini wananyanyaswa na kuuwawa na polisi kama ilivyotokea kwa Mwangosi! Taarifa nyingi wanazopata waandishi ni zile ambazo wenye taarifa hizo hupenda kuzitoa kwa kuitisha kitu kinachoitwa "press conference". Waandishi wengi hawapati taarifa kwa visingizio vya "nipo kwenye kikao"; "nipigie baadaye"; "nipo safari waulize waliopo ofisini" n.k. Kwa hali hiyo hauwezi kusema kuwa wana uhuru wa kupata habari. Kwenye Katiba mpya tutapendekeza utoaji wa habari usiwe hiyari bali ni haki kwa kila mtanzania kuzipata.
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Kweli wewe mpunyenye we wakuliwa tu.
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Uhuru ulipita kiwango ndo unapelekea wanapata kibano cha POLISI, hawataki tu kujitambua, waende RWANDA wakajionee , kila baada ya mita 500 unakutana askari zaidi ya watano wakiwa wamevalia kivita kusubiri chokochoko yoyote dhidi ya Serikali. Hawa wanahabari wetu wakienda nchi kama za kenya, Rwanda na Uganda hawawezi kufanyakazi kabisa.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hakika , hata waandishi wa habari wanatakiwa na wao kujitafakari kama wanafanyakazi kwa maslahi vyama vya siasa au kwa maslahi ya Taifa.
   
 7. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  una maanisha nini kusema “waandishi wa habari na vitendo vyao VIOVU?”
  Kama wapo huru lipo wapi gazeti la mwanahalisi?
   
 8. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  fafanua kidogo mkuu

  wao wanaandika habari zote hata siasa na hawapaswi kuchakachua hata kidogo ila sema wanapokuwa too bias
   
 9. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Mamaisara»kuandika ama kutoandika kitu fulani kwa maamuzi binafsi pia ni tawi la uhuru wa waandishi,ukitaka wawe huru na hapohapo ukitaka waandike habari zitakazowapendeza wakubwa zako tu,utakuwa unawaonyesha uhuru ndani ya kioo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni wazo lako na ni potofu pia.
   
 11. m

  mpunumpunyenye Senior Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  uhuru gani usio na mipaka?? upotoshaji hauna haki ktk uhuru wa habari!
   
 12. lusubilo lucas

  lusubilo lucas Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  unaweza kutoa sababu kwanini gazeti la mwanahalisi limefungiwa?hadi mwandishi wa habari anauliwa kinyama wewe ulioni hilo. unamatatizo makuba sana kwenye ubongo wako wewe
   
 13. melxkb

  melxkb JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmmmmm!! Dont reckon there is any reasonable Great Thinking in this..........!!!!!

  1. Uhuru wa habari maana yake ni mtu kuandika habari za mtu binafsi?,....tafakari kama ni kwa njia huru kw vyombo vya habari....??
  .
  2. Uhuru wa habari unapoona akaunti za watu zimeandikwa?..........tafakari kama ni kwa njia huru kwa vyombo vya habari....??

  3. Uhuru wa habari ni kuandika habari za Ikulu? Je unajua hizo habari zinapatikana vipi,....tafakari kama ni kwa njia huru kwa vyombo vya habari....??
  4. Je, kipimo cha uhuru wa vyombo vya habari ni pale vinapoandika habari za ikulu, usalama wa taifa, akaunti za watu, watu binafsi?......tafakari kama ni kwa njia huru kwa vyombo vya habari......??
  5. Je, kwa mjibu wako, uhuru kwa vyombo vya habari umekuwepo mkubwa na wa kupitiliza kwa hiyo magazeti yafungiwe kama adhabu ya kuukiuka huo uhuru na waandishi wanaouawa ni wale waliokiuka huo uhuru? Na jukumu hilo la kutekeleza hiyo hukumu liko mikononi mwa polisi wanpokuwa mitaani kwa kutumia risasi na mabomu?
  6. Mwisho naomba unisaidie takwimu zinazoonyesha kwamba Tanzania kuna uhuru wa vyombo vya habari uliopitiliza kuliko nchi nyingine duniani. Nitakushukuru kwa hilo.

  Ushauri:- Gharika imefika, hata wewe umo ndani ya chombo, endeleen kutumia RISASI na MIZINGA lakini kumbuka hakuna risasi au silaha iliyo imara zaidi ya mabadiliko ya kifikra na kimtazamo katika jamii - Hii imeshinda zote na haijawahi kuangushwa, kumbuka wakati wa Hittler, kumbuka Apartheid system ya SA, kumbuka utumwa wa babu zetu kwa vipigo na minyororo, kumbuka...kumbuka...kumbuka....kumbuka....mtatuua wachache, wengi watashinda, mkiuua mmoja wanazaliwa mia moja. Hata bila vyombo vya habari tayari dhoruba imesha chafua bahari na chombo chako kimekwisha toboka sharti maji yakizamishe na hatukubali kuzama, zameni peke yenu, TUTAPAMBANA....

   
Loading...