waandishi wa habari Tz wanaipeleka nchi pabaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

waandishi wa habari Tz wanaipeleka nchi pabaya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Barubaru, Jul 23, 2009.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hakika kwa takriban wiki mbili nimekuwa naangali vichwa mbali mbali vya habari vinavyotawala magazeti mbalimbali ya huko Tanzania na kuona vichwa vingi vinavyotawala ni OIC, Mahakama ya kadhi na waraka wa kanisa katoliki.

  katika fani ya uandishi hivi ni visa vinavyogusa imani na hisia kubwa sana katika jamii. Hususan kwa watanzania ambapo kuna dini kuu mbili yaani Ukristu na Uislamu. Hii ni sawa sawa na mpira Simba na Yanga. Kwani kama wewe ni mshabiki wa mpira huko tanzania ni lazima uwe mshabiki wa yanga au Simba kisha ukawa wa timu nyingine kama malindi au miembeni n.k.

  Kwa kifupi Dhumuni kuu na ndio msingi mkuu wa waandishi wa habari ni KUIPASHA JAMII, KUIELIMISHA JAMII na KUIBURUDISHA JAMII. Nikiwa kama Mwandishi wa habari kitaaluma na mwanasheria kitaaluma pia naona WAHARIRI wa tanzania sasa wanaipeleka nchi pabaya.

  Waandishi wengi huko Tanzania sasa wameweka mbele maslahi ya pesa pamoja na hisia zao binafsi na kuamua kuachana na maadili ya uandishi. Utaona Mwandishi anaandika kitu kwa matakwa yake na vile yeye anavyotaka kiwe kiasi cha kuibabaisha jamii na kuiweka jamii katika malumbano makali.

  Mwandishi hatakiwi kuwa upande wowote wa shilingi. yeye anatakiwa kuripoti kitu vile kilivyo na kuiachia jamii iamue. sasa unapomwona mwandishi anaripoti kitu na kisha ku conclude yeye mwenyewe ni kinyume cha kanuni za uandishi na vile vile kinyume cha sheria kwani kwani kazi yake ni kupasha habari na sio kuiamulia jamii ifanye nini.

  Siku zote tunaamini kuwa KALAMU YA MWANDISHI ina ushawishi mkubwa sana katika kuleta mtafaruku katika jamii. Kwani sana waandishi wa huko wameamua kufatilia na kuingilia mambo ya Dini na kuyaripoti vile wanavyotaka wao, kuwahoji baadhi ya mabalozi na hata kuandika kashfa kwa watu ambao wanakuwa kinyume cha matarajio yao.

  Huu kiuandishi ni mwiba mkali sana katika jamii ya ndugu zetu huko Tanzania. naishauri Serikali kuthibiti mambo hayo kwani yanaweza kuvunja amani iliyopo japo ni ya woga (hata ukiangalia humu barzani hoja za kidini zimechukua sura tofauti kiasi cha watu kuanza kukashifiana na kubezana katika iimani zao).

  Kuna mambo mengi huko Tanzania ambayo inabidi yaandikwe kama mauji ya albino, uchaguzi wa serikali za mitaa, vifo vya mama na watoto, ugonjwa wa ukimwi, malaria n.k ambapo waandishi wanatakiwa wafanye tafiti nyingi na kuandika makala nyingi za kuielimisha jamii.hayo ndio mambo yatakayoleta tija kwa jamii na kuimarisha usalama wa nchi.

  Namaliza kwa kusema.

  WAANDISHI NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI HUKO TANZANIA TAMAA YENU YA PESA MTAIZAMISHA TANZANIA KATIKA BALAA KUBWA LA VITA VYA KIDINI.

  Ni Mimi.
  Nasriyah Saleh Al- Nahdi.
  Qatar Petrolium Ltd
  Umm Hays
  Doha. Qatar
   
 2. S

  Shamu JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio Waandishi wa habari, bali ni FREEDOM. Sasa hivi tunayo Freedom, na kila mtu anasema au kuandika vile anavyopenda mwenyewe. Wakati wa Nyerere waandishi walitakiwa kuandika habari za Nyerere na CCM tu. Udini ulikuwepo siku nyingi sana; lakini waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuandika hizo habari. Sasa hivi Tanzania kuna mvutano wa Kidini kwa sababu kila dini inataka kutetea maslahi yake. Lete mvutano wa Kidini uendelee ili hayo matatizo yatatuliwe.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kisheria tunasema hakuna uhuru usio na mipaka. Ili kitu kiwe huru ni lazima kiwe kimewekewa mipaka yake kiutendaji.

  sasa katika fani ya habari kuna mipaka iliyobainishwa yaani kazi zao zitahusiana na kuelimisha, kupasha na kuburudisha jamii.

  Vile vile katika katiba ya Tanzania kuna freedom of speech, yaani inabainisha wazi kwa kusema kila mtu ana haki na yupo huru kutoa mawazo yake kwa jamii lakini maoni hayo hayatakiwi kuvunja sheria za nchi.

  sasa ukipitia kitaalamu sana hizo mada zao unaona wazi waandishi haa na wahariri wao wameamua kuweka pesa mbele na kusahau maslahi ya taifa.

  Au labda hawajawahi kuona vita za kidini wanazozichochea. hakika ni mbaya sana na wengi wataathirika sana na kupoteza sifa za Tanzania kama kisiwa cha amani duniani.

  Ijumaa mubarak

  Nasriyah Saleh Al-Nahdi
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  sio siri mzee toka haya mambo ya oic,mahakama ya kadhi na waraka wa kanisa kuna waandishi ambao mimi binafsi wameniboa vibaya kwa kuwa mstali wa mbele kuegemea upande flani badala ya maslahi ya taifa,kwa muda mrefu wale niliokuwa naamini kuwa waandishi makini lakini walioongoza kuniboa ni Saed Kubenea na M.M.Mwanakijiji makala zao zimeniboa kinoma kwani muda wote wanatetea uislamu,kutokana na kichefuchefu nilichopata kutokana na tungo zao za hovyohovyo hata magazeti yao nategemea kutoyanunua niliyokuwa nayaamini
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jile79.

  Hakika uliyonena ni muhimu lakini nakusihi unapoandika jaribu sana kupunguza jazba na kutumia majina ya watu. Kwani kisheria unaweza kuzua matatizo kama watakuuliza ushahidi ulionao.

  Kwa kweli takriban magazeti yote ya kila siku na yale ya weekly ya huko Tanzania YAMEEGEMEA UPANDE MMOJA NA KULETA MSUGUANO MKUBWA KWA JAMII NA KULETA CHUKI ZA KIDINI ZILIZOKUWA ZIMEJIFICHA.

  nasema sasa tanzania imejiweka vibaya sana na kama waaandishi hawa wataendelea hivi nafikiri majibu mtayapata si zaidi ya miaka mitatu. Amani itavunjika na watu kwa imani zao wataanza kupigana.

  Allah awanusuru kwa hilo
   
 6. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #6
  Jul 27, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njia pekee ya kutibu ugonjwa uliopo kwebye newsroom nyingi hapa nyumbani ni Kwa kuweka na kuheshimu viwango, kuanzia vyuo vinavyotoa masomo mbali mbali ya uandishi as habari. Vyuo hivi ni lazima viwe-regulated kuhakikisha elimu inayotolewa ni inayistahili na ya daraja la kimataifa. Tukifanikiwa kwenye ngazi hiyo, basi tutaweza kuhamia upande tasisi ya Maelezo.

  Tasisi hi ndiyo yenye mamlaka pekee ya kutoa vitambulisho vya waandishi wa habari. Kwa nafasi hiyo, Maelezo ikiwa makini inayo uwezo as kuchuja grade ya waandishi Kwa kutumia vitambulidsho maalum kulingana na uwezo, kisomo na uzeofu wa mwandishi wa habari. Baada ya hilo makampuni mbali mbali na tasisi zitashauriwa kualika waandishi kulingana na uzito wa issue. Hili litaweza kurudisha heshma kwebye fani hii ambayo ni kichicheo kikubwa Kwa maendeleo na demokrasia.

  La tatu na la muhimu zaidi ni wamiliki wa vyombo vya habari na serikali. Wawekezaji kwenye media wasaidiwe ili waweze kuboresha employment conditions. Jamani tuondokane na hili wazo kwamba media inweza kuendeshwa kwa cheap labour...hili ndilo linalopeleka nchi pabaya. Tunabitaji kujenga media yenye maadili na msimamo kama nanga yake. Lakini kama tutaendelea kutengeneza ajira zisizoendeleza watu au kuwainia kimaisha basi milele watakuwa wanaingiliwa na watafuna nchi na kuendeleza agenda zao. Sekta ya media itengenezewe viwango vya 'employment conditions'. Itoe muongozo wa mshahara, benefits, training na professional accreditation (viwango vya taaluma).

  Hayo ndiyo maeneo ninayoona yataleta tija kwa kuanzia. Tukishajenga msingi huo, ndipo tunapoweza kuelekeza nguvu kwenye 'specialization' - hili nitalizungumzia Kwa kina baadaye kidogo.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Gold Digger,

  hakika kwa upande wangu sina wasiwasi na viwango vya elimu na taaluma za waandishi wengi hususan wahariri. wana viwango vizuri sana na vyenye kutambulika ila nafikiri ni tamaa tu inawafikisha huko katika kuvunja maadili ya habari.

  Mimi naona suala la WAHARIRI kuingiliwa kikazi na wamiliki wa vyombo vya habari. Utaona wamiliki wengi wa vyombo vya habari vya huko Tanzania wanaona kuwa vyombo vya habari ni biashara na sio sehemu kubwa ni huduma kwa jamii biashara ni ndogo sana.

  Sasa naona waharir wameamua kuacha maadili na kuangalia pesa na kuandika habari zile zinazochochea jamii ikiwa pamoja na kuleta mitafaruku ili jamii zifarakane na wao wauze habari zao. hakika hii ni hatari kubwa inayyoeza isababishia nchi vita.

  Vile vile ni vizuri Serikali ya Tanzania kuangalia viwango vya mishahara pamoja na elimu kwa waandishi ikiwa pamoja na semina, warsha na mafunzo mengine kwa waandishi.

  Vile vile waandishi au wamiliki wa vyombo vya habari ikiwa pamoja na wanahabari kujikita zaidi katika kuandika makala za kitafiti na sio kukimbilia habari za matukio.

  Nasriyah Saleh Al-Nahdi
   
 8. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasriyah,

  Sikatai kwamba baadhi ya wahariri wana kisomo kizuri na wenye taaluma, lakini hawatoshi! Ninakubaliana na wewe fika kwamba mazingira magumu ya kazi na imani potofu ya baadhi ya wawekezaji kwenye sekta hii imeruhusu virusi kuingilia kazi na kufuta heshima ya fani yetu.

  Lakini pia ni lazma tukubali kwamba nchi yetu sasa imefikia hatua ambayo sasa tunahitaji wapasha habari wawe na uewelewa kuliko yule mtu wa kawaida, haswa kwenye eneo ambayo wanawapasha habari.

  Kwa mfano, ni aibu kwamba kwenye Tanzania ya leo kuna mwandishi wa habari anatumwa kuripoti habari za michezo leo alafu wiki inayofuata anatumwa kuripoti habari kuhusu sera mpya, programu za miundombinu au uchumi wa nishati...hivi kweli hapo tunatarajia kupata habari ya kina?

  Kuna haja ya kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa na angalu diploma kwenye somo moja nje ya fani yao. Kwenye nchi nyingi huwa vyuo vikuu havitoi digrii ya uandishi wa habari mpaka umalize diploma au digrii kwenye somo mojawapo kama biashara, sheria, lugha, maendeleo ya jamii, siasa, michezo na mengineyo. Hivyo wanahakikisha kwamba mwandishi wa habari anapoingia kwenye ajira anao uwezo wa kuchambua na kuelewa kwa kina masuala mbali mbali na kuweza kuchagua kubobes kwenye eneo lake. Hili pia husaidia waaandishi kuweza kujiendeleza pale watakapo taka kuachana nu uandishi wa habari. Na mwisho ya siku matunda ya utaratibu huu ni pale jamii inaponufaika kwa kuelewesha na kupasha habari za uhakika.

  Hili ni suala muhimu sana kama kweli tunataka kuendeleza taifa na kurudisha heshma ya fani hii kwenye nchi yetu.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Gold Digger,

  Hakika uliyosema ni sawia kabisaa hakuna hata chembe ya ubishi. Sio Tanzania tu bali siku zote waandishi ni lazima wahudhurie kozi mbalimbali za kitaaluma ikiwa pamoja na washa zitakazo wawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

  Na utaona wengi wa wahandishi siku hizi wanapenda sana kuandika (kuripoti)habari za matukio zaidi na kuacha kujikita katika kuandika makala zenye tafiti na uchambuzi wa masuala ya kijamii. Hii yote inajitokeza kutokana na kukosa taaluma sahihi za mabo ya kijamii.

  Lingine naona huko Tanzania, taaluma ya habari imevamiwa na watu wasiokuwa na taaluma ya uandishi, wao wanakuwa repoter tu na baadae kuanza kuandika habari.

  hakika wengi wa hawa wanakuwa hawajui ethics za uandishi ndio maana wanakimbilia kuandika habari nyingi za kichochezi na zile zinazogonganisha jamii.Hawajui madhara ya KALAMU ZAO kwa jamii.

  Lakini msingi mkubwa ni kuwa wahariri wengi wamekua na tamaa kiasi cha kuachia magazeti yao yatekwe na kuandika habari za kufarakanisha jamii kwa nia ya kupata thamani ndogo ya pesa lakini wakijua fika wanalichimbia kabuli Taifa.

  Nasriyah
   
Loading...