Waandishi wa habari TZ hii inakuwaje?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Nimeshuhudia baadhi ya waandishi wa habari wanaokuja wilaya ya Tandahimba wakilipwa Posho na Halmashauri ya Wilaya hiyo. Tena hupewa posho zaidi pale wanapotaka kubalance story ambazo zinawagusa watendaji wa Halmashauri. Tumeshuhudia ukandamizaji mkubwa kwa wakulima wa korosho ambao wameanzisha Umoja wao, katika kipindi hicho kulikuwa na utitiri wa waandishi ambao walikuwa wanazunguka huku na huko na kuchukua posho kila walikoenda. Walipoenda kwenye Umoja wa wakulima walipewa pesa na walipoenda Halmashauri pia walilipwa. Pia katika kumbukumbu zangu inaonyesha kuwa mwandishi mmoja anayeripoti katika vyombo vinavyomilikiwa na ndugu R. Mengi anaongoza kwa kupewa posho na Halmashauri. (kaanza siku nyingi)

Naomba ufafanuzi hapa, hii ni Takrima au kitu gani? Na mnaruhusiwa kufanya hivyo?
Kwanini Halmashauri itoe Posho kwa waandishi?
 
Navyojua mimi, waandishi huwa wanalipwa posho kwenye either semina au mikutano na muhsuika kama ahsante tu kwa ajili ya kuripoti hayo matukio, kwa hilo lako sina hakika.
 
Mambo mengine uchune GAZETI unataka tukale wapi? Tusipochangamka huku chini ndio basi tena, pale ndio inapoishia kamba yetu. Dah hizi post nyingine zitatuharibia ulaji!
 
Usilee Ugonjwa. kama unaogopa kutaja majina ya waandishi hao basi angalau taja magazeti/redio/tv wanavyofanyia kazi. Zaidi ya hivyo mchango wako huu muhimu utaishia kuonekana ni Udaku tu. Dare to talk openly.
 
Usilee Ugonjwa. kama unaogopa kutaja majina ya waandishi hao basi angalau taja magazeti/redio/tv wanavyofanyia kazi. Zaidi ya hivyo mchango wako huu muhimu utaishia kuonekana ni Udaku tu. Dare to talk openly.

Mimi nilitaka ufafanuzi hapo lakini kwa kuwa umetaka saaana kufahamu si mbaya nikikutajia huyu mmoja ambaye anaripoti sana Radio one - Rashidi Kanga. Ninachohitaji ni ufafanuzi wa jambo lenyewe hilo!
 
Back
Top Bottom