Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
Kwa takriban siku mbili nipo Tanzania na napata fursa kubwa kusoma magazeti ya nchi hii na pia kusikiliza radio na kuona TV mbalimbali za Tanzania hususan Bara naona kweli Maadili ya Uandishi wa Habari sio tu wa magazeti lakin pia hata Radio na TV umekosa uzalendo.
Waandishi wengi sana wamejikita katika USHABIKI na kupenda kufanya BIASHARA ya habari zao na kusahau kabisa miiko na Sharia na kaanun za Uandishi wa habari. Tukumbuke mwiko mkubwa kwa mwandishi yoyote wa habari ni USHABIKI. Mwandishi anatakiwa kutoa ripoti ya kile anachokiona bila kuongeza jambo lake lolote na kama anataka kuripoti tukio ni lazima ahakikishe anatenda haki kwa kila upande kwa kupata maoni na rai zao. Kwani siku zote habari inakuwa na sehemu mbili (mlalamika na mlalamikiwa).
Inatakiwa ifahamike kuwa kazi ya Mwandishi wa habari ni KUELIMISHA JAMII, KUBURUDISHA JAMII na Kuijuza au KUIPASHA HABARI JAMII. Kwa mantiki hii utaona Kalamu ya mwandishi ni sumu au bomu baya sana kuliko lile la nyuklia. Mwandishi siku zote anatakiwa kutumia busara sana katika kazi zake ikiwemo na kuweka uzalendo wa nchi yake mbele kwa kutoa habari zilizo sahihi zisizo na hata chembe ya ushabiki kwa jamii kwani jamii inataraji kupata habari zilizo sahihi na zisizo na upendeleo wa upande wowote.
Ukipitia Sharia za Tanzania inaozungumzia Uhuru wa maoni sharia namba 15 ibara ya 6 ya mwaka 1984, kifungu cha 18
.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru

kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wamawasiliano yake kutoingiliwa kati.(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimukwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.Kwa hicho nilichobainisha Juu utaona karibu kila chombo cha habari tanzania kimekosa uzalendo. Chukulia habari ndogo tu jinsi wanavyoripoti mambo kutoka Bungeni. Waandishi hawa hawana umakini na hawajui kuwa kuna sharia maalum za uandishi wa habari za Bunge na Mahakama. Wao wanajaza ushabiki miongoni mwa jamii za Kitanzania na kuigombanisha Serikali na raia wake kwa manufaa yao ya kibiashara na kisiasa na kusahau Amani ya nchi hiyo.
Jana nilikuwa napitia habari za Kiongozi wa madaktari Dr Mkopi kufikishwa mahakama ya kisutu. Utaona kila gazeti limeripoti linavyofahamu na kwa mtu makini kama atasoma unaona kabisa waandishi hawa wana nia kubwa ya kuigombanisha Serikali na Madaktari bila kufahamu kuwa watakao umia ni wananchi. Wameshindwa kabisa kujua kuwa Dr Mkopi ameshitakiwa na mahakama kwa kudharau amri halali ya mahakama na sio Serikali.
Ukisoma kwa kina wanashindwa kabisa kuofautisha Mahakama, Serikali na Bunge. Kwao wao kila kitu ni sawa. Nasikitika sana kuona Baraza la Habari Tz limekaa kimya na hata wizara ya habari Tz zimekaa kimya bila kukemea haya. Kwa tunaamini kuwa msipoziba Ufa basi kifo kitawaumbua.
nawasihi muwe wazalendo kwa nchi yenu na ondoeni kabisa ushabiki wa Siasa au kidini kwani mnaiangamiza nchi yenu.
Haya ni maoni yangu kwenu
Dr Hamza Yousuf Al naamaniy (Barubaru)
Mwanza Tarabu (Muta) na Nkurukumbi
Omwana nikalikwela,ina shani ommano,
Lutiluti nanda maiza, omoyo tigindi munda.
Owenfundo nyamilinga, lugayo olwo nakubone,
ijamawe kinyalyana, lugayo ongalule moyo
Nkurukumbi 2
hay