Waandishi wa Habari ni nguzo muhimu, walindwe

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100
Tasnia ya habari imekuwepo kwa vizazi na vizazi, Tasnia hii imechangia kufanikisha mambo mengi sana ikiwamo, maendeleo, kukuza lugha, kutoa elimu mbalimbali, kuonesha sehemu zenye fursa za kiuchumi na kufichua ubadhilifu katika mambo mbalimbali ikiwemo kwa watumishi wa Umma nk.

Tasnia ya habari inazidi kukua sana hasa kwa nyakati hizi za sayansi ya Teknolojia ambapo kwa sasa taarifa husafiri kwa haraka na kufikia watu wengi sana kwa muda mfupi. Vyombo vya habari Televisheni, Magazeti, Redio, Mitandao ya kijamii vinafanya kazi kubwa sana kuhakikisha taarifa zinawafikiwa watu kwa wakati.

Katika kuhahakisha uwepo wa tasnia hii kuna watu ambao ni wana habari, watu hawa wanaweza kuwa waajiriwa katika taasisi mbalimbali za habari, makampuni au asasi zinazoshughulika kwanamna namna au nyingine na habari au taarifa. Tasna hii haiwezi kuendelea wala kuwepo bila uwepo wa wana habari au wachapishaji wa maudhui, watu hawa hufanya kazi muhimu sana na wakati mwingine hufanya katika mazingira magumu na hatarishi katika kuhakikisha jamii inapata habari au taarifa muhimu zinazohitajika. Katika kuzingatia umuhimu wao watu hawa walipaswa kulindwa au kwani ni tunu moja muhimu sana.

Pamoja na umuhumi wao watu hawa wanakabiriwa na changamoto nyingi sana ambazo ninakuwa kikwazo katika kuhahakisha upatikaji wa taarifa muhimu au habari za kiuchunguzi ambazo kimsingi zinahitahika sana ili kuibua mambo mengi ambayo yamefichichwa.

Baadhi ya changamoto zinazowakabili:

1. Uwepo wa Sera na sheria ambazo zinanyima uhuru wa hasa anapotaka kuandika habari za kiuchunguzi, mfano
  • Sheria ya takwimu haimruhusu mwanahabari kuandika bila kupata taarifa kutoka vyanzo vya serikali,
  • Sheria ya habari inataka mwanahari asajiliwe
  • Sheria ya mitandao.
  • Sheria inayoipa Mamlaka ya Mawasiliano kufungia vyombo vya habari inawapa hofu wana habari ya kukosa ajira
2.Changamoto ya kupanda kwa gharama za vifurushi vya mitandao (Internet) Hii inawaathiri zaidi waandishi ambao ni raia wa kimtandao, ambao mara nyingi huwa ni wa kujitegemea ambao huweza kushuhudia jambo na kulichapisha mtandaoni ikiwa ni sehemu ya kutoa taarifa kwa jamii.

3. Hofu ya usalama wao, kulikuwa na uwepo wa matukio ya kupigwa na kunyang'anywa vifaa vya kazi kwa wana habari, hali hii inafanya watu kuwa na hofu wa kufanya kazi kwa weledi na wengine kuacha kabisa kwa kuhofia maisha yao mfano, Kuuawa kwa baadhi ya wanahabari kama Mwangosi, kupigwa kwa mwandishi wa habari Zanzibar nk.

4. Mishahara midogo, Kukosekana kwa maslahi katika kazi zao huwafanya washinde kuwa wabunifu, wawe watu wa kupenda 'vibahasha'hivyo kuandika mambo ambayo anayataka anayewapa bahasha hata kama hayana tija.

5. Kukosekana kwa vifaa vya kisasa katika hasa kwa kutokuwa na mitaji ya kutosha hivyo kushindwa kufikia malengo ya kazi zao.

Kutokana na changamoto hizo jamii amba ndio walaji wa maudhui yanayotengenezwa na wana habari inakosa habari na taarifa zenye tija. Wana habari wamejikita katika kutoa taarifa kulingana na matukio ya kila siku na kutafiti na kuchunguza kuhusu mambo muhimu yalijificha katika jamii, Serikali nk.

Serikali, Wadau mbalimbali hakikisheni mnawalinda wana habari wajione wako salama katika kutekeleza majukumu yao, Sheria na sera kandamizi zifanyiwe marekebisho ili jamii inufaike na kazi zao.
 
Back
Top Bottom