Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Wewe Pasco upo kundi lipi hapo?
Mkuu Mzalendo80, Pasco wa jf ni mwandishi wa kujitolea wa jf, silipwi chochote na yeyote!. Hata utetezi wangu kwa Lowassa, wale mnaoamini nalipwa, kutokana na uwezo wenu wa kufikiri, endeleeni kuamini hivyo maana huo ndio uwezo wa fikra zenu!. Lakini wanaofikiri kwa kutumia logic zaidi, nadhani watakubaliana na mimi kuwa namtetea Lowassa for a reason, na kupitia hiyo reason behind, Lowassa hawezi kunilipa mimi nimpigie debe humu jf!.
 
Mkuu BADILI TABIA, naungana na wewe mia kwa mia kuwa bahasha ni bahasha, hilo halina ubishi ila sio kila bahasha ni hongo au rishwa!.

Ndio maana kuna kuanzia bahasha ya posa, bahasha ya rambirambi, bahasha ya sadaka kanisani etc.

Hata hizi bahasha za waandishi, zipo bahasha za usafiri, bahasha za lunch, bahasha za masurufu, bahasha za maduhuli, bahasha za posho za vikao, bahasha za marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi, bahasha za usumbufu, bahasha za uwajibikaji, zote hizi ni bahasha halali ambazo waandishi wa habari wanapaswa kulipwa!. Hizi sio favours ni stahili zao ambazo wa wanastahili kulipwa!.

Usitubabaishe kwa maneno, hizo bahasha unalipwa na nani?
 
Iwe fedha ya usafiri, au malazi au chakula kama anakupa kwa kutaka umuandike, hiyo ni rushwa tu. Hauna ujanja hapo.

Dahh, mpokea rushwa na mgawa rushwa unataka kujitetea? nilikuwa sijui lakini leo umeweka wazi mwenyewe. Acha hiyo ni dhambi kubwa sana, si kidini tu hata ki uzalendo.

Kuanzia leo hii ni vita rasmi, mimi na wewe na sitokubali au kuamini chochote unachokiandika. Wewe unafanya dhulma kubwa sana kwa watanzania na kukiri kwako hapa inabidi uchukuliwe hatua kali sana za kisheria, iwe ni fundisho kwa wengine.

Kwa kuwa umekiri mwenyewe sasa tuelezee na vibahasha hivyo umeshapokea kutoka kwa nani na nani na umesha vigawa kwa nani na nani.

Kama inabidi utengeneze fedha kwa uandishi wako kuna njia nyingi sana za kutengeneza pesa za halali, kwa kuanzia unaweza kuwa muandishi wa scripts na si wa habari.

Nkusikitikia sana na hapo hapo nakushangaa sana tena na hapo hapo nakusifu kwa kueleza ukweli lakini ukweli haukuondelei dhambi ya kupokea na kugawa rushwa kama ulivyokiri mwenyewe hapo juu.
Dada yangu FaizaFoxy, hebu muulize Maalim wako Mohammed Said, aliwezaje kuyaandika hayo aliyoaandika na atawezaje kuya print na kuyasambnaza maandishgi yake bila kuwezeshwa?. Ili media zifanye kazi zake vyema ni lazima ziwezeshwe!. Huu uwezeshaji wa media zetu masikini ili zitimize wajibu wake nazo ni bahasha!.

Hivi unajua kwa nini shule la Islamic Seminaries zinafanya vibaya na ndizo shule zinazovuta mkia zikifuatiwa na shule za Wazazi?!. Jee unadhani watoto wa Kiislamu wanazaliwa na akili pungufu ya Wakikrito?!. Hapana!, wote wanazaliwa na akili zawa na wengine hata kuwazidi Wakristu, kwa nini sasa ndio wana end up failures?!. Tena tuna bahati hatujafanya sense walioko magerezani wengi ni wa dini gani, au idadi ya masikini wanaioshi katika umasikini uliotopea wengi ni wa dini gani?!, utashang'aa!. Sababu ni nini?, ni kiwango cha uwezeshaji!. Wenzenu Wakristu wanafanya uwezeshaji kwa taasisi zake huku wakisaidiwa na ile MOU ambayo nayo ni bahasha!.

Media zetu ni masikini za kutupwa bila kuwezeshwa, haziwezi!. Sasa kama uwezeshaji huu unaiuta rushwa!, hebu muulize Rais Kikwete huwa anawapa nini wale waandishi wa habari anao safiri nao?!. Kama kweli kila anaetoa bahasha kwa waandishi lazima aende jela, naomba tuanzie na Ikulu, nami jela nitajipeleka mwenyewe bila hata kusubiri kutafutwa!

Lengo la hii mada ni kuonyesha kuwa kweli bahasha zipo lakini sio kila bahasha ni rushwa!. Ziko bahasha safi za facilitation ambazo lengo lake ni uwezeshaji wa media, hizi sio rushwa!.
 
Mkuu Pasco nakubaliana nawe kabisa kuwa waandishi wa habari ni fani kama nyingine na wanadamu kama wengine. Kuna stahiki zao kama wengine na haki zao kama taaluma nyingine.

Nikutahadhirishe tu kuwa unapoweka mpaka wa hiki ni halali na hiki sio unaweza kujifunga na kamba yako mwenyewe.
Kuna kitu kinaitwa Law, halafu Regulations. Hivi ni vitu ni 'binding' ya kuwa mwandishi anapaswa kufanya ABC au hapaswi kufanya ABC.
Nadhani umesahau kitu kinaitwa 'ethics' ambacho ukikiangalia haki 'bind' moja kwa moja lakini kinaweza kuwa chachu ya kuumua mkate wakati Regulations na Law zinafanya kazi.

Waandishi mna ethics zenu kama alivyo mwanasheria au Daktari.
Nitashangaa kama utanikuta saa 6 mchana nipo mahali na Hakimu tunapata Lunch halafu saa nane anasikiliza kesi yangu.
Lunch ni haki ya hakimu kama mlo na hakuna mahali imesemwa itoke wapi.
Kinachomsuta hakimu ni ethics(maadili) , kwamba atatenda ilivyokusudiwa? Lunch imeleta kitu kingine kinaitwa conflict of interest kati ya mimi mshtakiwa anayenifahamu tukiwa katika lunch na sheria anazozijua na hiyo ime compromise integrity ya hakimu lakini haina maana kuwa ni haramu.

Nimetoa mfano huo ili kujenga hoja kuwa hizo bahasha unazosema ni halali ni kweli yaweza kuwa ni halali, lakini je huoni kuna ambazo zinaleta conflict of interest, zina violate principle, values and ethics za uandishi?

Labda pia nionyeshe wapi kamba inaweza kukufunga. Bahasa za usumbufu ni zipo hizo Pasco? nielimishe hapa.
Mkuu nguruvi3, the deviding line beween bahasha safi na bahasha chafu is very thin!. Kwa vile bado niko stage ya bahasha safi, acha nimalize, nitakuja bahasha chafu na hapo ndipo tutakapona hiyo conflict of interest, na kuna "pressures facing the news", ambapo suala la "he who pays the piper maya call the tune" itakuja!.
 
Da
Hivi unajua

Media zetu ni masikini za kutupwa bila kuwezeshwa, haziwezi!. Sasa kama uwezeshaji huu unaiuta rushwa!, hebu muulize Rais Kikwete huwa anawapa nini wale waandishi wa habari anao safiri nao?!. Kama kweli kila anaetoa bahasha kwa waandishi lazima aende jela, naomba tuanzie na Ikulu, nami jela nitajipeleka mwenyewekusubiri kutafutwa!

Pascal soma definition ya corruption inayopatikana kwenye Prevention and Combating of Corruption Act 2007, baada ya hapo angalia kwenye sheria yote utafute Kama shida ni defence, no no no. Hata ingekuwa na shida namna gani ukipokea hela kwa ajili ya kutimiliza kitu kwa niaba ya aliyekupa, na kitu hicho ukifanye kwa kutumia ofisi yako basi hiyo ni Rushwa. Usibishe.
 
Tunaendelea na bahasha safi. Hapa Tanzania huwa tunayo vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano, vyote hivyo hutengewa posho iitwayo sitting allowances, yaani posho za vikao. Hizi ni pesa halali ambazo zinalipwa kwa kila aliyealikwa. Waandishi wakialikwa kama wajumbe wa vikao hivyo, na wakahudhuria kama wajumbe wengine, mwisho wa siku hulipwa kama wengine na bahasha hizi pia ni halali na nazitetea kwa nguvu zangu zote!.

Kwa msio elewa, wakati wa kikao cha bunge, mtashuhudia vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano mengi yakifanyikia Dodoma siku za Jumamosi na Jumapili na Spika huwatangazia wabunge na kusisitiza "utaratibu " utafuatwa, anamaanisha kila atakayehudhuria, atalipwa ile sitting allowance ya bunge ambnayo ilikuwa 80,000 sasa ni 200,000!. Kwenye vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano haya, waandishi hualikwa lakini wao kwa vile sio wajumbe, huripoti tuu opening na kutoka nje, hapa sasa ndipo vile vibahasha vya ama transport ama lunch hutolewa na waandishi huishia zao. Posho hizi hazina uhusiano na kuimfluence reporting bali kuwawezesha waandishi watimize wajibu wao!. Hizi pia ni posho halali hivyo bahasha halali ambazo sio rushwa!. Mkiamua kuziita nazo ni rushwa, sawa, ila waanze kwanza hao wabunge watangulie gerezani nasi wanahabari tutawafuatia!.
 
Mkuu Pasco thanks kwa hili darasa la bahasha! Mi mwenyewe my ofc tulikuwa tuna lunch new products tuliita waandishi wakatoka na 15000@ sikuelewa 4 wht! Leo nimekusoma thanks mkuu.
 
FaizaFoxy, unaonaje kama tukianzia Ikulu lile fungu la kuwawezesha waandishi linalipwa na nani?, ndipo tuje kwenye media zetu zinalipwa na nani?

Tuambie Ikulu ni nani alikupa bahasha na ilikuwa na shillingi ngapi?

Usitueleze kuhusu mafungu ya Ikulu ya kuwezesha, Ikulu ina mafungu mengi sana ya kuwezesha, karibu kila sekta. Nimekuambia umeshafanya dhambi na bado unaitetea na kwa hilo huwezi kuchakachuwa, dhambi ni dhambi tu, ikiwa Ikulu wanafanya dhambi ya kugawa vibahasha vya rushwa inabidi kama mwandishi uelezee hapa kinaga ubaga.

Kama unategemea kwa kuitaja Ikulu ndio FaizaFoxy atatetea dhambi? hapo sahau, sinto itetea Ikulu au baba yangu au mama yangu au yeyote yule anaefanya dhambi ambayo hata Qur'an inaikataza.
 
Pascal soma definition ya corruption inayopatikana kwenye Prevention and Combating of Corruption Act 2007, baada ya hapo angalia kwenye sheria yote utafute Kama shida ni defence, no no no. Hata ingekuwa na shida namna gani ukipokea hela kwa ajili ya kutimiliza kitu kwa niaba ya aliyekupa, na kitu hicho ukifanye kwa kutumia ofisi yako basi hiyo ni Rushwa. Usibishe.
Mkuu Ngambo Ngali, kujua nini ni rushwa na nini sii rushwa hauhitaji kuisoma definition, rushwa ni fedha inaotolewa kwa malengo ya kuifluence the natural course of action, sasa hizi bahasha za usafiri, chakula au vikao, ni kwa lengo la kuwezesha, empowering na sio ku influence positive coverage!. Kama uwezeshaji wowote ni rushwa, then Tanzania yote tukula rushwa maana kufuati umasikini wetu, makusanyo yote hayatoshelezi uendeshaji wa nchi, hivyo kuna budget deficit ambayo inakuwa covered the general budget support fung inayotolewa na mataifa ya ulaya, hivyo nchi yetu nzima tunahongwa!.
 
najiuliza huyu pasco anejibu kwa ufasaha na kujiamini ni pasco yupi
tupe full name kaka kwani tunakufananisha na pasco m tunaemfahamu wengi
ingawa umesema sio yeye.we ni kioo cha jamii endelea kutujuza yote ulioulizwa
labda nkuulize una mkakati gani kurudi TBC na utaisaidiaje TBC iwe chombo cha umma badala ya chombo cha serikali
ili uendeshaji wake uratibiwe na umma na sio serikali? kama ilivo KBC BBC na wengineo.
kuhusu bahasha bado naziona sio haki yenu kupewa kwani mnalipwa mishahara na mnapaswa kuandika habari pasipo kutegema bahasha
kwani inaonekana wazi mnatoa habari na kuzipa kipaumbele kulingana na uzito wa bahasha.
hii dhambi itawatafuna milele na hata hadhi yenu inayumba sana itabidi tuwatungie sheria kali kuhusu hilo nami ntakuwa mstari wa mbele
kuandaa hiyo rasimu.
 
Pasco hata useme nini rushwa ni rushwa tu. Hao wazungu usituletee habari zao, hatuongeleai bajeti ya nchi hapa. Mada umeanzisha mwenyewe kuhusu vibahasha na kila unachokifanya hapa ni kutetea dhambi.
 
Tunaendelea na bahasha safi. Hapa Tanzania huwa tunayo vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano, vyote hivyo hutengewa posho iitwayo sitting allowances, yaani posho za vikao. Hizi ni pesa halali ambazo zinalipwa kwa kila aliyealikwa. Waandishi wakialikwa kama wajumbe wa vikao hivyo, na wakahudhuria kama wajumbe wengine, mwisho wa siku hulipwa kama wengine na bahasha hizi pia ni halali na nazitetea kwa nguvu zangu zote!.

Kwa msio elewa, wakati wa kikao cha bunge, mtashuhudia vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano mengi yakifanyikia Dodoma siku za Jumamosi na Jumapili na Spika huwatangazia wabunge na kusisitiza "utaratibu " utafuatwa, anamaanisha kila atakayehudhuria, atalipwa ile sitting allowance ya bunge ambnayo ilikuwa 80,000 sasa ni 200,000!. Kwenye vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano haya, waandishi hualikwa lakini wao kwa vile sio wajumbe, huripoti tuu opening na kutoka nje, hapa sasa ndipo vile vibahasha vya ama transport ama lunch hutolewa na waandishi huishia zao. Posho hizi hazina uhusiano na kuimfluence reporting bali kuwawezesha waandishi watimize wajibu wao!. Hizi pia ni posho halali hivyo bahasha halali ambazo sio rushwa!. Mkiamua kuziita nazo ni rushwa, sawa, ila waanze kwanza hao wabunge watangulie gerezani nasi wanahabari tutawafuatia!.

Huwezi kuhalalisha hizo na zikawa halali, wale wako kazini kwao na wanalipwa kutokana na kazi zao, nyinyi mlipwe kazini kwenu na si na hao mnaotakiwa kuwaandika. Hapo hakuna uhalali na hilo unalijuwa.

Wale waliokuwa wanasema wewe ni kanjanja mie nikakutetea naomba wanisamehe sana.

Wewe ni mla rushwa na mgawa rushwa, ni mtu hatari sana kwenye jamii. Husameheki hata kidogo kwani bado unajiona kuwa hufanyi dhambi na kuvipa majina tofauti vibahasha, hivi hata nafsi yako haikusuti kwa haya?
 
Kwani Pasco,source analazimika au anapaswa amlipe au amkirimie mambo gani mwandishi?
Una maana mi nikiwa Mtwara,nikitoa taarifa kwenye ofisi yako..sina budi kuandika pia kwamba,wakionyesha tiketi za ndege watarudishiwa nauli zao,na nitawalipa per diem sh kadhaa kwa siku?? Yaani ni wajibu wangu?
Haya umetaja TBC,na wao wakipokea barua ya namna hiyo wana act vipi?
Asante Pasco......
trachomatis, kama ulinisoma vizuri mwanzo, nilisema ni jukumu la vyombo vya habari kuwawezesha waandishi wake wafike popote na kutekeleza majukumu yao pasi kulipwa na source. Kufuatia ukata unaovikabili vyombo vyetu, havina uwezo wa kukuletea mwandishi huko Mtwara, unless TBC ina mwakilishi wake Mtwara!, ili habari yako itoke ITV itakubidi umgharimie huyo mwandishi usafiri, chakula, malazi na per diem ili aweze kufika Mtwara. Hozo zote ni bahasha safi!.
 
najiuliza huyu pasco anejibu kwa ufasaha na kujiamini ni pasco yupi
tupe full name kaka kwani tunakufananisha na pasco m tunaemfahamu wengi
ingawa umesema sio yeye.we ni kioo cha jamii endelea kutujuza yote ulioulizwa
labda nkuulize una mkakati gani kurudi TBC na utaisaidiaje TBC iwe chombo cha umma badala ya chombo cha serikali
ili uendeshaji wake uratibiwe na umma na sio serikali? kama ilivo KBC BBC na wengineo.
kuhusu bahasha bado naziona sio haki yenu kupewa kwani mnalipwa mishahara na mnapaswa kuandika habari pasipo kutegema bahasha
kwani inaonekana wazi mnatoa habari na kuzipa kipaumbele kulingana na uzito wa bahasha.
hii dhambi itawatafuna milele na hata hadhi yenu inayumba sana itabidi tuwatungie sheria kali kuhusu hilo nami ntakuwa mstari wa mbele
kuandaa hiyo rasimu.
Mkuu Lokissa, mimi ni Pasco wa jf, nakuomba usifananishe!, Pasco wa jf akarudin TBC kufanya nini?!. Nana pekee ya kuisaidia TBC ni kwa sisi humu jf tuiandike sana TBC mpaka wakuu wasikie waibadilishe!.

Kuhusu bahasha, nimesema ziko bahasha safi ambazo sio rushwa na ziko bahasha chafu ambazo ni rushwa!. Mpaka kati ya bahasha safi na chafu ni malengo ya hizo bahasha, zikitolewa kwa malengo mabaya, ni rushwa, zikitolewa kwa malengo mazuri ni bahasha safi!.
 
leo mmemshika pabaya kijana wa lowassa mweee!basi dada faiza inatosha jamani,mkubwa hakombi mboga,msameeni tu.
 
Back
Top Bottom