Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,578
Wanabodi,

Kuna hoja nyingi huwa zinaibuliwa humu JF kuhusiana na sisi waandishi wa habari, kwa vile na mimi ni mwandishi, naomba nichangie kwa lengo la kuhabarisha na kuelimisha na sio kujitetea!

Intro ya Pasco au Paskali.
Mimi ni Mtanzania, nimezaliwa jiji Dar es Salaam, nimesoma primary Dar es Salaam na sekondari Dar na Arusha, nikaenda JKT na kutua Chuo cha Uandishi wa Habari TSJ, Chuo Kikuu cha DSM, na kuhudhuria mafunzo mbalimbali ndani na nje a nchi.

Sehemu kwanza kufanyia kazi ni gazeti la Daily News, enzi zile tuna magazeti matatu tu, Daily News, Uhuru na Mfanyakazi. Kisha nikaenda RTD, wakati ule Tanzania tuna redio moja tuu, na a pili ilikuwa ni Sauti ya Injili kule Moshi. Mwaka 1994, Tanzania ndio ikaruhusu TV, hivyo nikajiunga na DTV, ambako ndiko niliendesha kile kipindi cha Kiti Moto. Mwaka 2000 nikajiunga na TBC ambapo mwaka 2002 nilifukuzwa kazi kwa kosa la insubordination.

Toka mwaka 2002 hadi leo 2012, nimekuwa ni mwandishi wa kujitegemea.
Sasa hivi habari zangu nazisambaza kwenye magazeti 10. vituo vitano vya TV, vituo vitano vya Redio, na several online forums. Nimespecialize kwenye Radio and TV Production, hivyo kazi a kuandika, naandika kwa kujitolea, just for the love of it, na silipwi na media yoyote kuwaandikia, nawapa habari bure, kama ambavo ninavyoandika bure humu JF.

Hapa nilipofikia, siwezi tena kuajiriwa na yeyote, wala siwezi kutumwa na yoyote, ofisi yangu iko eneo la mjini kati, pango tuu la ofisi, ni zaidi ya mshahara wa DC!, hivyo naombeni sana nisisikie ule upuuzi kuwa Pasco anaandika kwa kutaka chochote!. Naandika just for the love of it, to inform and I get nothing!.

Hoja za Rushwa na Bahasha za Waandishi.
Kuna hoja ya waandishi wa habari kupokea bahasha ambayo inatafsiriwa vibaya kama rushwa/hongo/chochote/mlungula etc. Mchokoza mada ni Mkuu Lunyungu kama alivyoichokoza hivi
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako. Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi.

Mimi issue ya akina Pasco imenishangaza sana baada ya rafiki yangu kuambiwa anatakiwa kuandaa bahasha ya khaki ili habari zake zitoke popote.Huyu jamaa analeta suluhisho katika majanga ya moto kwenye hii .Yaani pale maelezo anatakiwa kulipa 60,000 tshs kwa saa moja na ana ambiwa kwa uwazi aandae bahasha kulingana na uzito wa mtu ili habari zile ziandikwe .Hii imenishangaza mno .Hivi hawa waandishi si wako kwa kuandika habari? Au wewe Pasco na wenzako mko kupata bahasha ndipo muandike na nasikia kama huwezi kumpoza editor unaweza pigwa chini pamoja na bahasha yako kwa mandishi .Pasco msaada wako tafadhali.
Mkuu Lunyungu kwanza pole kwa hii, yote usemayo ni kweli mimi kama mwanahabari, nimeisha vipokea sana hivyo vibahasha na mpaka hapa nilipofika sasa, hivyo vibahasha vya waandishi, mimi ndio msambaza!.
Ila naomba kufuatia msiba mkubwa JF tulionao kwa sasa, Msiba wa Regia Mtema, please lets keep off this topic mpaka baada ya msiba nitakueleza kila kitu na ni kwa nini nasupport hivyo vibahasha, nimevihalalisha na nina vigawa with clear conscious!
Mkuu Pasco , sasa msiba umepita na Mh.Regia apumzike kwa amani .Naona sasa ni wakati muafaka unipe jibu juu ya wewe na wenzako kupenda bahasha za khaki ili muweze kuandika habari kwa watanzania kujua nini kinaendelea .Karibu tuanzie hapa kwanza maana kwangu nimeshangaa kwamba unahongwa ili uandike habari hata zile ambazo ni za manufaa kwa jamii lakini lazima bahasha ya khaki .
Angalizo, kabla sijaanza kujibu hoja, samahani sana Mkuu Lunyungu kwa kutoijibu thread yako kufuatia thread ile kumchafua member fulani wa jJF, naowaombeni wachangiaji wa uzi huu, tujikite kwenye issue na sio kwenye watu, pia nakumbushia sheria za JF, mtu kama amejitambulisha yeye ni fulani, naombeni tuheshimu utambulisho huo, hata kama unadhani unamjua huyo fulani ndio fulani kiukweli huruhusiwi kumtaja, hiyo ni name calling. Naombeni reference zote kwenye mada hii zitamhusu Pasco wa JF na sio vinginevyo!

Mkuu Lunyungu, ni kweli waandishi wa habari hupokea bahasha, na mimi kama mwandishi, nimeishazipokea sana, mpaka sasa mimi ndio nazigawa, ila ukweli halisi wa mambo, sio kweli kila bahasha mwandishi anayopokea ni rushwa! Ziko bahasha waandishi wanapokea sio rushwa na zipo bahasha kweli ni rushwa. Sasa tuanzie hapa, na mimi nitaendesha hilo somo kidogo kidogo kwa kutoa dozi ndogo ndogo mpaka hatimaye mwisho wa siku tutaelewana na mtatuelewa sisi ndugu zenu waandishi.

Mada itakuwa kwenye vipengele kadhaa!

1. Bahasha za Waandishi ni nini?
2. Je, kuna bahasha aina ngapi?
3. Je, kuna uhalali wa Waandishi kupokea bahasha hizo?
4. Je, ni bahasha zipi sio rushwa?
5. Je, ni bahasha zipi ni rushwa?
6. Je, Bahasha za "asante"-Takrima nayo ni rushwa?
7. Je, ni kweli kwa waandishi kupokea bahasha ni kuendekeza njaa?
8. Kuibuka kwa kada ya Makanjanja kufukuzia Bahasha?
9. Je, ni waandishi ndio waoomba hizo bahasha au sources ndio huzitoa wenyewe?
10. Pasco wa JF na msimamo wa kutetea bahasha!

Kwa hayo na mengine mengi yatakayojitokeza, fuatana nami katika mada hii ya Waandishi wa Habari na Bahasha!

Pasco wa JF,

Karibuni sana!

1. Je, Bahasha za Waandishi ni nini?
Bahasha za waandishi wa habari, ni fedha zilizowekwa kwenye bahasha ambazo waandishi wa habari hupewa, ama ili wahudhurie mahali, waandike habari, wazuie habari fulani isitoke, waandike habari mbaya kuhusu jambo fulani, au waandike habari za kufagilia au hata uzushi. Kwa kifupi bahasha ni fedha waandishi wanazopewa na bahasha nyingine ni za asante tuu ama takrima. Mara nyingi bahasha hizi zimetafsiriwa kama zote ni rushwa, ila ukweli wa mambo, sio kweli bahasha zote ni rushwa, japo nyingine kweli ni rushwa ila sio bahasha zote ni rushwa!.

2. Je, kuna bahasha aina ngapi?

Bahasha ziko za aina nyingi, lakini aina kubwa ambayo ndio most popular ni bahasha ya pesa, "those little brown envelopes'. Lakini bahasha ziko za aina nyingi kama vile rushwa zilivyo za aina nyingi na pia zinatumia majina tofauti. Bahasha sio lazima iwe pesa?. Ziko bahasha za favours fulani ambapo mwandishi anapewa favours ili afanye positive coverage, facility visit- ni mwandishi anapewa trip fulani hadi nje ya nchi ili kufanya favourable coverage, free bees, kama chakula, vinywaji hutolewa kwa waandishi kama chai, vitafunwa, chakula na vinywaji ili waandishi wakuandike vizuri. Materias kama vizawadi fulani kuanzia vitendea kazi, mavazi, laptops, na wenye bahati zao hupewa zawadi mpaka za magari au kupewa/kujengewa nyumba. Mpaka sasa tunavyozungumzia bahasha hizi, bado tunazungumzia bahasha kama bahasha na hakuna uthibitisho kuwa bahasha hizi ni rushwa!.


3. Je, kuna uhalali wa waandishi kupokea bahasha hizo au kuzidai?
Jibu ni ndio, kwa zile bahasha ambazo ni halali. Naomba nitaileta justification baada ya kusema bahasha zipi ni halali na bahasha zipi si halali, yaa ni rushwa!. Sasa zile bahasha za halali, kuzipokea ni halali, na tena usipopewa, una haki ya kuzidai!. Na kwa zile bahasha ambazo ni favour, takrima, bakhshish na asante hizi haziombwi wala hazidaiwi, huletwa tuu na wahusika na kugaiwa, ila pia naunga mkono bahasha hizi zipokelewe!.
Bahasha mbaya ni zile za rushwa na hizi ndio hata mimi nazipinga!.

4. Je, ni bahasha zipi sio rushwa?
Nilianza uandishi zamani enzi za redio ni moja tuu, RTD na magazeti mawili tuu ya Daily News na Uhuru. Wakati huo mimi nilikuwa RTD. Ofisi ilikuwa na magari hivyo tunapelekwa kusubiriwa na kurudishwa. Ukiwa na tukio lako, unaleta gari yako ina pick waandishi na kuwarudisha. Enzi hizo hakuna bahasha!. Ukiwa na safari nje ya mkoa unaleta barua kuwa utangarimia waandishi, hivyo unawalipia usafiri chakula na malazi na kuwarudisha bila bila!.

Vyombo vya habari vilipofumka na kuwa vingi, sasa ikawa sii rahisi kuwapelekea usafiri vyombo vyote na pia matukio ya habari ni mengi, si rahisi kila chombo kupeleka waandishi wake kila mahali, hapa sasa ndio zikaanza bahasha za mwanzo za halali.

Hivyo ukiwa na habari yako ili waandishi waweze kufika, lazima uwapatie usafiri na kwa vile vyombo viko vingi huo usafiri kupita kote utapoteza muda mrefu, then wewe mwenye tukio lako unawapa go ahead waandishi kujitegemea kwa usafiri na wewe utawarudishia naili yao na kuwaongezea nauli ya kurudia na huu ndio mwanzo wa bahasha ambazo ni genuine.

Hivyo bahasha ya usafiri hii ndio bahasha ya kwanza genuine na halali ambayo mwandishi anapewa. Kwa vile vyombo vyenye usafiri wake sio lazima kupewa bahasha za naili. TBC ni miongoni mwa media zenye usafiri wake na mara kibao waandishi wa TBC na baadhi ya media wakimaliza kazi hutimka bila kusubiri bahasha.

Kwa kuanzia wanabodi, naomba tukubaliane kuwa bahasha za usafiri ni genuine kama zinatolewa kwa malengo ya kuwawezesha waa ndishi wafike mahali pa tukio na kurudi. Media zetu ni masikini za kutupwa!, Pamoja na kuwa na vituo vya TV lukuki na vingine viko kwa zaidi ya miaka 10, vituo vyote hivi viko hoi bin taaban kiuchumi na kuna vingine vina survive kwa kudra ya mwenyeenzi Mungu!. Ukiondoa TBC ambayo ni spoon fed, vituo vingine vyote vinavyo survive God knows!. Umasikini wa vituo hivi utaujua kwa kuangalia amount of local programing na quality of creativity na quality of production ni very poor!. Hatuna local series hata moja! Series zote 100% kwenye TV zetu zote, ni foreign! Hakuna media yoyote nchini yenye budget ya invetigative stories, Jerry Mura alipoondoka ITV, Usiku wa Habari ukajifia natural death! Ukiondoa talk show ya Kiti Moto enzi zile, bado sijaona talk show ambayo inaniwahisha nyumbani never to miss it, Dakika 45 ya ITV sasa ni angalau angalau. Jeneral on Monday alitaka kujitahidi lakini wapi!. Talk show zote za studio ni cheap stuff ambazo ndizo only we can afford, redio na magazeti ndio msiseme kabisa!.

Kufuatia umasikini huo, whoever mwenye news yake ambayo iko mbali, lazima awafacilitate waandishi wafike, the easiest facilitation ni kupitia bahasha. Media zote dunia nzima ili ziweze kutimiza wajibu wake ni lazima ziwezeshwe ili ziwawezeshe waandishi wake watimize wajibu wao! Uwezeshaji wowote wa media, hizi ndizo bahasha zenyewe!. Rais wetu afanyapo ziara za mikoani na hata nje ya nchi, husafiri na pool of journalits ambao lazima wewezeshwe kwa bahasha!. Mkisikia ripota wa ITV, TBC, Chanel Ten au Star TV anaripoti ziara ya rais akiwa nje ya nchi, ukae ukijua chombo chake pekee hakija jeuri ya kumpeleka kuripoti Marekani bila kuwa facilitated na Ikulu!. Kwa maana hiyo mpaka Ikulu inakata panga!

Mtu asikutanganye eti CNN na vyombo vya habari vya Marekani wanaosafiri kwenye Airforce One na rais Obama, wanasafiri bure!. Wanakatiwa bahasha za nguvu kutoka vyombo vyao na labda hivyo vyombo vyao vinachangia gharama, lakini hizo fedha za vyombo vyao ni mibahasha minene toka ma multanational na matlilateral companies/organizations, lakini the bottom line ni bahasha!.

Kuna watu wanaweza kuleta hoja kuhusu BBC ambacho ndicho chombo pekee cha habari ambacho hakipokea matangazo, hivyo hakipokei bahasha ya mtu!. Kwa wasio jua watafikiri BBC ndio chombo malaika hakipokei bahasha!, No!. BBC wanapokea bahasha kupitia kodi ambayo inakatwa kwa kila mtu aliyeko Uingereza, haijalishi unaisikia au husikilizi redio yake au huangalii tivi yake, unailipia utake usitake!. Hizi ndizo bahasha ambazo BBC inakiburi cha kuwakatia waandishi wake watimize wajibu wao!.

Bahasha za Posho za Vikao nazo Rushwa?

Tunaendelea na bahasha safi. Hapa Tanzania huwa tunayo vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano, vyote hivyo hutengewa posho iitwayo sitting allowances, yaani posho za vikao. Hizi ni pesa halali ambazo zinalipwa kwa kila aliyealikwa. Waandishi wakialikwa kama wajumbe wa vikao hivyo, na wakahudhuria kama wajumbe wengine, mwisho wa siku hulipwa kama wengine na bahasha hizi pia ni halali na nazitetea kwa nguvu zangu zote!.

Kwa msio elewa, wakati wa kikao cha bunge, mtashuhudia vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano mengi yakifanyikia Dodoma siku za Jumamosi na Jumapili na Spika huwatangazia wabunge na kusisitiza "utaratibu " utafuatwa, anamaanisha kila atakayehudhuria, atalipwa ile sitting allowance ya bunge ambnayo ilikuwa 80,000 sasa ni 200,000!. Kwenye vikao, mikutano, semina, warsha na makongamano haya, waandishi hualikwa lakini wao kwa vile sio wajumbe, huripoti tuu opening na kutoka nje, hapa sasa ndipo vile vibahasha vya ama transport ama lunch hutolewa na waandishi huishia zao. Posho hizi hazina uhusiano na kuimfluence reporting bali kuwawezesha waandishi watimize wajibu wao!. Hizi pia ni posho halali hivyo bahasha halali ambazo sio rushwa!. Mkiamua kuziita nazo ni rushwa, sawa, ila waanze kwanza hao wabunge watangulie gerezani nasi wanahabari tutawafuatia!.

Bahasha za Grants/Fellowships/Scholarships na Sponsorships za Awards mbalimbali kwa Waandishi, nazo Rushwa?

Kuna mashirika na taasisi mbalimbali zinatoa fungu fulani kwa waandishi kuandika kuhusu jambo fulani, usually indepth, mfano Tanzania Media Fund, inatoa funding kwa journalist kuandika stories toka vijijini, au investigative stories. Hizi ni bahasha nene zenye kucover usafiri, chakula, malazi, kwa field trip hata za mwezi mzima, nyingine ni attachment mahali kwa muda hadi miezi 6, hizi nazo ni bahasha, jee nazo ni rushwa?. No hizi ni bahasha safi!.

Mashirika/ makampuni au taasisi huweza kugharimia kukundi cha habari kuandika about specific news, hii inaitwa sponsorship mfano TAMWA ON FGM, TGNP dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia, JET thidi ya uharibifu wa mazingira etc. Bahasha nene hotolewa ili waandishi waandike kusu specific topic, hizi nazo rushwa?. Mifano iko mingi, mia kidogo ambapo bahasha hutolewa kwa waandishi genuinely na sio rushwa!. Wale mnaolazimisha kila bahasha kwa mwandishi ni rushwa, nawaombbeni sana mthink twice, tubishane kwa hoja na sio kulazimisha hoja!

6. Je, Bahasha za "asante"-Takrima nayo ni rushwa?

Nimeruka number 5 ili kumalizia kundi la mwisho la bahasha safi, hizi zinaitwa bahasha za asante, bahasha hizi waandishi hulipwa kupewa asante kwa kazi nzuri walizofanya, hizi ni kama tip au keep change, hazina uhusiano wowote na kuimfluence bali hizi ni appreciation.

Kulitokea news ya mteja mmoja muhimu alikuwa ana news yake siku ya Alhamisi mchana, akataka magazeti 6 ya Kiingereza, Daily News, Guardian, Citizen, This Day, The Express, na The African. Nikamtajia the Bussiness Times, akasema yeye ofisi yake hawalinunui na wanaliona kama lipolipo tuu.

Siku ilipofika nikawapitia hao waandishi waliochaguliwa nikawapeleka, miongoni mwao kukawepo mwandishi wa Bussiness Times nikamwambia gazeti lako halitakiwi, akaniomba sana aje, nikamkatalia taharibu bajeti, akaomba kuja hata bure bila bahasha!, nikamkubalia!.

Kufika pale waandishi wakajitambulisha, ilipofika zama ya jamaa wa Bussiness Times, yule bosi akamzodoa wewe nani kakuita hapa?, kabla hajajibu, nikaingilia kati kuwa nimemleta mimi, bosi akatoa amri aondoke kwa vile hatamlipa, mimi nikamwambia bosi, nitamlipa mimi!. Hoyu bosi akasema kuna vijigazeti vingine viko viko tuu, vinachapishwa na kuishia kufungia samaki na maadazi!. Hata mimi nilijisikia vibaya!.

Akamuita mzungu wake akazungumza saa nzima!, kuja kumaliza jamaa wa Bussiness Times akaniaga, fasta, nikamlinda, akaondoka zake! Wale wengine wakasubiria bahasha nene, by the time zimetoka ni saa 10 jioni!. Tukaondoka zetu.

Kesho yake asubuhi, boss kanipigia simu kuniambia asante sana, amesikia news yake imetoka lead story front page na picha kubwa full color ila hajui gazeti gani!. Akiwa njiani kuelekea kazini akanunua Daily News, Guardian, Citizen, This Day, The Express na The African. Kutafuta story hakuona kitu!. Akanipigia tena kuniuliza iko gazeti gani?. Nikamwambia bado sijaliona ila nitakwenda ofisi kwake saa 4.

Nikapitia ubao wa Magazeti ndipo nikaona big headline kwenye Bussiness Times!, of all the papers!. Nikalinunua kwenda nalo huku njia nikawapigia wale wengine wote licha ya bahasha nene, there is nothing!, wote wakasema shauri ya kusubiria bahasha, walichelewa deadline, hivyo wataitoa kesho yake!. Kufika ofisi nikaripoti kwa boss sababu ya kuchelewa na kumkabith the BT, alifurahi na kushukuru sana, ila hakukumbuka ndio yule jamaa aliyemzodoa!

Kesho yake Jumamosi kucheki magazeti yote hamna kitu!. Nikapiga tena simu na kuuliza kulikoni, ndipo wakanijibu story imekaa kibiashara zaidi, hivyo imewekwa bussiness news, Jumamosi na Jumapili hakuna bussiness news!, hivyo nisubirie mpaka Jumatatu, huku mzungu anaondoka Jumapili anataka kuondoka na news clips zake!. Nilalaumiwa nimemlet down!. Ikabidi Mzungu aondoke na clip moja tuu ya BT!

Jumatatu kweli magazeti mengine wakatoa, sio front page na sio headline!. Wakati wa postmortem na boss akaishukuru sana BT, akanituma nimtafuteb yule mwandishi amuombe msamaha in person na kuamua kumlipa 5 times more as appreciation! Hii ni bahasha ya shukrani, it has nothing to to na rushwa!. Zile tuzo mbalimbali wanazopata waandishi zikiandamana na bahasha nene, ni shukrani na sio rushwa!. Waandishi wengine hupewa trips za abroad kama asante kwa kazi nzuri. Bahasha hizi za asante ndio kundi la nmwisho la bahasha safi.

Baada ya kuzitaja bahasha ni bahasha genuine, sasa nitaziorodhesha bahasha ambazo ni rushwa.

Bahasha ya Kushinikiza Positive Covarage

Hii ndio bahasha ya kwanza ya rushwa, hutolewa na source ili kuwa entice waandishi wawafanyie favourable covarage. Kwa kawaida bahasha hii inakuwa nene fulani, bahasha hii huandamana na obligation kuwa lazima story itoke. Bahasha hizi za shinikizo la story kutoka hazitolewi kwa waandishi wote, bali to only few selected, na kwa vile bahasha hizi ni rushwa, hutolewa kwa kificho!. Zile bahasha za halali kama za usafiri husainiwa wazi wazi na hukawiwa kila mtu akiona kwa sababu there is nothing to hide, lakini hizi hutolewa kwa kificho, no one will know nani amepokea bahasha na nani hajapokea kutokana mazingira ya usiri. Watoaji wa bahasha hizi wanajua ni rushwa na wapokeaji wanajua ni rushwa! (to avoid conflict of interest, nawaombeni msiniulize zaidi kuhusu hizi!).

Bahasha za Kuzuia Habari Kutoka-Hii ni Rushwa!

Kuna bahasha za kuzuia story fulani isitoke!, hizi ni bahasha zinazotembezwa kwa waandishi ili kuzuia story fulani isitoke ili kulinda maslahi fulani au jina la mtu fulani lisichafuke!. Hii inahusisha kuitwa kwenye tukia na kutake a good care ya waandishi ili wasiripoti kabisa kuhusu tukio fulani! Hii mara nyingi huusisha ama scandals au black mail. Mfano kigogo mmoja mheshimiwa sana, ameshitakiwa kwa kosa la kufumwa akifanya mapenzi na Changudoa ufukweni. Story hiyo ikitoka itamvunjia heshima sana mzee, hivyo anakata fungu fulani la kutakata la kuwatake care waandishi wote wanaoripoti toka mahakamani ili kesi ya kigogo ikitajwa waipotezee. Au Wafanyakazi wa kiwanda fulani wamegoma, wewe ni mwandishi unakwenda kucoiver story, unaanza na mgomo, ili kubance story, lazima uwatafute na management, ile kufika management, unakuwa well taken care off, uamuzi ni wako, ulinde heshima ya taaluma yako na ulale njaa, ama uuze utu wako jioni ukakae viti virefu, uamuzi huwa ni individual!


Blackmail na Framing ni rushwa mbaya kabisa!

Hii inahusisha waandishi kupata habari mbaya kuhusu vigogo fulani, mwandishi ku solicit money ili kuzuia kumlipua muhusika huyo!. Au umezinyaka picha za utupu za kigogo fulani unamuonyesha na kudai kiasi cha fedha ili uzizichapishe!. Kesi ya rafiki yangu Jerry Muro ili fall kwenye kundi hili!

Sambamba na blackmail, kama polisi wanaweza kukuisingizia kesi ndivyo waandishi wa habari wanavyeweza kuku frame na kukuandikia habari mbaya za kutunga, mfano wa alichofanyiwa Dr. Salim Ahmedv Salim na gazeti la Mtanzania ili kumbeba JK awe mgombea!,

Saa hizi usiku umekuwa mkubwa sana, kesho nitaendelea na hizi bahasha chafu ambazo ndizo rushwa na ni za kuogopwa kama ukoma!

Bahasha za Usafiri, Lunch na free bies nazo ni rushwa, je wakati gani ni Rushwa?

Kwa mliofuatilia pale mwanzo nilisema, bahasha ya usafiri ikitolewa kwa lengo la kuwawezesha waandishi kufika eneo la tukio bila kuingilia wataripoti nini, hiyo sio rushwa, ila bahasha hiyo hiyo inapotolewa kwa kuitwa hivyo hivyo usafiri kwa lengo la positive covarage, then bahasha hiyo ni rushwa!. Baada ya taarifa uchavuzi wa mazingira ya mto Tigiti, Barrick waliandaa ripoti yao positive na kuwagharimia waandishi na walioandika Barick ilichotaka!. Hiyo provision ya usafiri kwa waandishi uliofanywa na Barric kweli ni ku facilitate ili kupata positive coverage, hivyo unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa na rushwa, na unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa sio rushwa!. The deviding line is very thin ndio maana sishangazwi na wale wanaoona kila bahasha ni rushwa!.

Vivyohivyo offer za lunch, dinner na vijizawadi zawadi, kuna wakati ni rushwa na kuna wakati sio rushwa!. Ukienda semina warsha au kikao, wajumbe wote wakapowa sitting allowances zao, wote mkala lunch, au zile event, waalikwa wote wanapewa vijizawadi na waandishi wakiwemo, then sio rushwa, lakini waandishi mkiitwa mahali, hakuna event yoyote, mkapigwa lunch ya nguvu na baada ya hapo mkapewa bahasha ya transport haka kama hujapewa news yoyote, hiyo ni rushwa!

Bahasha za Matangazo ya Biashara Kugeuzwa Habari nayo ni rushwa Mbaya inayoua Taaluma ya Habari!

Wanabodi,

Kwa vile hapa nchini hatuna sheria ya kugharimia vyombo vya habari vya umma, hii inamaana vyombo vyote vya habari Tanzania, vinalazimika kutegemea matangazo ili visurvive! Serikali ndiye mtangazaji mkubwa kuliko mtangazaji mwingine yoyote wa matangazo. Vyombo vya habari vya serikali, gazeti la Daily News na TBC, vyenyewe vina advantage ya ziada over and above vyombo vingine vyote, kwa sababu, japo sina ushahidi wa uthibitisho, but trend inaonyesha kuna "waraka wa siri", unaoelekeza matangazo yote ya serikali, lazima kwanza yaende vyombo vya habari umma na ya ziada ndio ndio yaende vyombo binafsi!, hii ni kinyume cha ushindani huru wa kibiashara!. Advantage ya pili ya vyombo hivi, licha ya kupata preference ya matangazo ya serikali, pia mishahara yao inatoka hazina!, hivyo tunaviendesha vyombo hivi kwa kodi zetu!

Kufuatia hali hii, vyombo vingine vyote vya habari ambavyo navyo ni utitiri, vinasurvive kwa matangazo hayo hayo, hali inayopelekea kusurvive kwa kugawana umasikini wetu as a result, media zote, zina survive katika lindi la umasikini!. Umasikini huu ndio unaopelekea media zenyewe kushindwa kuwagharimia waandishi wake katika kila assignment na ku compromise ama kukubali kukosa baadhi ya habari, ama kukubali kusaidiwa "bahasha" ili waweze kupata kila habari!

Media zote haziwezi kulipa mishahara inayotosheleza angalau kujikimu kwa zile basic needs, let alone saving! Kama mishahara ya serikali ndio hiyo mnayoisikia na wafanyakazi wa serikali wana survive, mishahara ya kwenye media zetu binafsi ni half ya ile ya serikali, ukiondoa IPP Media na Mwananchi!, nayo pia haitoshelezi, hivyo wana habari naweza kusema wote, wanaishi kwenye njaa kali!.

Baadhi ya wanahabari haswa wale ma senior editors wa magazeti wanamiliki vyuo vya uandishi wa habari, wale wapiga picha wanamili vyuo vya picha au photo studios na wale wa Redio na TV wanamiliki production houses na ma senior journalists kibao ama wana survive kwa membership kwenye press clubs, majukwaa ya wahariri, au underground advertising companies na PR companies ili to make both ends meet! Shughuli zote hizo za pembeni wahariri/ waandishi na watangazaji wanazozifanya sio rushwa ila ni kinyume cha maadili kwa sababu zina cut accross the line of conflict of interest! At this jancture, naomba nikiri wazi, bado wako waandishi wachache makini ambao wamesimama imara katika maadili, na hawa utawajua ile siku wanapoondoka duniani, wanakuwa wamekuja with nothing, wanaondoka with nothing na wanaacha nothing!

Kufuatia survival ya media ni matangazo, na kusema ukweli matangazo ni ghali, tangazo la 60 sec prime ya ITV ni 800,000 na TBC ni 600,000 wakati full page ya Daily News/Guardian na Citizen ni 4,000,000 plus!. Baadhi wa maofisa masoko wa makampuni mbalimbali, ambao wameishajua njaa ya vyombo vyetu vya na hivyo ku devise mbinu ya kugeuza matangazo ni habari. Kama una tangazo lako unataka litoke inside news ya ITV utalipia 800,000 lakini badala ya tangazo ukiwaita waandishi pale moven pick na kuwapiga lunch ya nguvu kwa kisingizio chochote, mwisho wa siku uawapatia kale ka bahasha ka "usafiri" ndani umewakea 100,000 then tangazo lako lita sail inside news for less na with more time! Ndio maana mnaona kila siku ni habari za makampuni ya simu, makampuni ya bia, na biashara mbali mbali na vihabari vyao na picha magazeti, mara wamezindua hiki na hiki, mara washindi wa bahatinasibu hizi na zile mara wanatoa donation hii na ile etc, hayo yote ni matangazo kuyageuza habari, hii ni rushwa mbaya!


Paskali
 
Kwanini Rais Mstaafu Mkapa alikuwa hawakubali nyie waandishi wa Habari wa Tanzania,
Utusaidie na hilo Pasco
 
1. Je, Bahasha za Waandishi ni nini?
Bahasha za waandishi wa habari, ni fedha zilizowekwa kwenye bahasha ambazo waandishi wa habari hupewa, ama ili wahudhurie mahali, waandike habari, wazue habari fulani isitoke, waandike habari mbaya kuhusu jambo fulani, au waandike habari za kufagilia au hata uzushi. Kwa kifupi bahasha ni fedha waandishi wanazopewa na bahasha nyingine ni za asante tuu ama takrima. Mara nyingi bahasha hizi zimetafsiriwa kama zote ni rushwa, ila ikweli wa mambo, sio kweli bahasha zote ni rushwa, japo nyingine kweli ni rushwa ila sio bahasha zote ni rushwa!.
 
Kwanini Rais Mstaafu Mkapa alikuwa hawakubali nyie waandishi wa Habari wa Tanzania,
Utusaidie na hilo Pasco


Hakuna kitu kibaya na kitekelezi kwa reputation ya Kiongozi wa state kama "The forth estate" hasa katika haya mataifa machanga ambayo hata kiongozi ajitahidi namna gani ni kazi saana kutatua matatizo yote. Kheri sasa kama wangekua wana weka effort kubwa katika hilo; (as much as Tanzania sidhani kama we qualify katika hio). Mkapa is one confident dude... A reasonable confident Leader he was. In other words ni kwamba as much as he was confident alikua anajua wazi kabisa kua Vyombo vya habari ni vya kuvi potezea mbali if he was to work vile atakovo "a salient absolute leadership" - a kind of Leadership ambayo kiongozi wenu awapelekesha but mwaona it is right he is doing so na mwaridhia kwa lolote. The Irony ni kwamba ni mwandishi mwenyewe. What makes it worse ni wanahabari wetu wa Tanzania ambao wengi ni wana habari njaa (mtanisamehe wahusika ila ndio ukweli in most cases).

Nilisikitika saana kwamba for the very first time Mkapa aliamua kufunguka kwa media was to comment on "why alikua hajaipatia Michezo uzito wakati wa Uongozi wake".... Jamani, wewe mwandishi wa habari unapata nafasi ya Kuongea na kiongozi mkubwa kama yeye ambae hafungukagi hata siku moja; then unakubali kuhojiana nae kuhusu habari za Mchezo hali kuna maswali lukuki ambayo Watanzania tunataka kujua.... Siamini kwamba yule mwanahabari alikua hajui hilo... that is the sad part of it.... Inakua kama Mwandishi wa habari hana akili na Mtanzania ataesoma hio habari nae mjinga pia.....
 
2. Je, kuna bahasha aina ngapi?

Bahasha ziko za aina nyingi, lakini aina kubwa ambayo ndio most popular ni bahasha ya pesa, "those little brown envelopes'. Lakini bahasha ziko za aiona nyingi kama vile rushwa zilivyo za aina nyingi na pia zinatumia majina tofauti. Bahasha sio lazima iwe pesa?. Ziko bahasha za favours fulani ambapo mwandishi anapewa favours ili afanye positive covarage, facility visit- ni mwandishi anapewa trip fulani hadi nje ya nchi ili kufanya favourable coverage, free bees, kama chakula, vinywaji hutolewa kwa waandishi kama chai, vitafunwa, chakula na vinywaji ili waandishi wakuandike vizuri. Materias kama vizawadi fulani kuanzia vitendea kazi, mavazi, laptops, na wenye bahati zao hupewa zawadi mpaka za magari au kupewa/kujengewa nyumba. Mpaka sasa tunavyozungumzia bahasha hizi, bado tunazungumzia bahasha kama bahasha na hakuna uthibitisho kuwa bahasha hizi ni rushwa!.
 
pasco wa JF!
je huoni bahasha km imetolewa kwa lengo la takrima huweza kum'badilisha muandishi aliyepokea bahasha hiyo na kwenda kuandika habari ya kurudisha shukrani ya takrima hiyo? (km hujanielewa ntafafanua zaidi)
 
2. Jee kuna bahasha aina ngapi?

Bahasha ziko za aina nyingi, lakini aina kubwa ambayo ndio most popular ni bahasha ya pesa, "those little brown envelopes'. Lakini bahasha ziko za aiona nyingi kama vile rushwa zilivyo za aina nyingi na pia zinatumia majina tofauti. Bahasha sio lazima iwe pesa?. Ziko bahasha za favours fulani ambapo mwandishi anapewa favours ili afanye positive covarage, facility visit- ni mwandishi anapewa trip fulani hadi nje ya nchi ili kufanya favourable coverage, free bees, kama chakula, vinywaji hutolewa kwa waandishi kama chai, vitafunwa, chakula na vinywaji ili waandishi wakuandike vizuri. Materias kama vizawadi fulani kuanzia vitendea kazi, mavazi, laptops, na wenye bahati zao hupewa zawadi mpaka za magari au kupewa/kujengewa nyumba. Mpaka sasa tunavyozungumzia bahasha hizi, bado tunazungumzia bahasha kama bahasha na hakuna uthibitisho kuwa bahasha hizi ni rushwa!.

Kwa maneno machache tu naomba niseme kwamba in most cases bahasha hizo ni rushwa!!!!! Miaka miwili iliyopita, nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari juu ya jambo fulani. Pale maelezo nilifanya booking ya ukumbi na kulipia (nakumbuka hata receipt sikupata kwani nilipigwa mkwara kwamba kwa tarehe ile na siku za karibu na hiyo tarehe ukumbi ulikuwa tayari uko booked). Receipt alikuwa suala kubwa kwangu kwa wakati ule, nilitaka nipate nafasi ya kukutana na waandishi wa habari.

Tangazo liliwekwa na waandishi wa habari walikuja kwa wingi, walikuwa kama 50 au 60 kutoka vyombo mbali mbali. Niliwaambia nilichotaka Watanzania wakijue na mwisho nilitoa nafasi ya maswali. Baada ya hapo nikatangaza kwamba mkutano umekwisha. Wengine waliondoka mara moja lakini wengine waligoma kuondoka na kuendelea kuniuliza maswali ingawaje mkutano tayari ulikuwa umefungwa. Zilipigwa picha nyingi tu. Kesho yake, kwa mshangao ni gazeti moja tu la Majira lilitoa ile habari. Magazeti mengine yote hakuna lililoandika. Nilipomuuliza jamaa yangu, akaniuliza kama nilitoa bahasha, nikasema la, akaniambia bila bahasha habari haziwezi kupewa nafasi kwenye magazeti. Kwa kifupi bila kutoa rushwa, habari zako haziwezi kuandikwa!!! Pasco hata ukijitetea vipi mnapokea rushwa ndio muandike habari.

Tiba
 
1. Jee, Bahasha za Waandishi ni nini?
Bahasha za waandishi wa habari, ni fedha zilizowekwa kwenye bahasha ambazo waandishi wa habari hupewa, ama ili wahudhurie mahali, waandike habari, wazue habari fulani isitoke, waandike habari mbaya kuhusu jambo fulani, au waandike habari za kufagilia au hata uzushi. Kwa kifupi bahasha ni fedha waandishi wanazopewa na bahasha nyingine ni za asante tuu ama takrima. Mara nyingi bahasha hizi zimetafsiriwa kama zote ni rushwa, ila ikweli wa mambo, sio kweli bahasha zote ni rushwa, japo nyingine kweli ni rushwa ila sio bahasha zote ni rushwa!.

Mkuu Pasco hizi bahasha zote hua zina malengo yanayo fanana no matter yametolewa wakati gani. At least ndio ninavo amini. Vigezo ambavo hupelekea mtoaji atoe bahasha hio yategemea vigezo vya muhimu.


MTOA BAHASHA



  1. Ni kiongozi mkubwa na mara nyingi ana controversial views za wadau/wanaharakati hasa in the world of media iwe in Politics/business.
  2. Ni mfanya biashara mkubwa ama mmilliki wa rasilimali ambazo ni gumzo la media iwe katika natural/non-natural resources; Mfano labda tueseme Barrik.
  3. Ni Company kubwa hapa nchini na kukuza brand na jina la Kampuni is of utmost importance hasa ukizingatia kua Competition ipo stiff.
  4. Ni mwananchi wa kawaida tu....

The above ndio hu determine the nature of the envelope apewayo mwandishi. Hao the above woote ni kama vile tuseme ni a corparate world (or closely related); Kasoro hio # 4. Hawa watu katika huo ulimwengu hawafanyi mambo kwa kubahatisha wala kubabaisha. Na hao hao watoa bahasha once you are out of the media business you are out of there payroll. They give you something hata kama hujawafanyia kitu bado tayari ni a salient agreement kua tupo pamoja kwa lolote lile. Hivo basi kama tayari ushapewa bahasha mara ya kwanza, ya pili, ya tatu. Ina maana mshajenga mahusiano ya karibu na Trust pia. An agreement kwamba "next time umesikia news about me" just print for I know you Know what I want/don't want there. Hivo hapo hio bahasha itakuja mwisho but at the end of the day ni kua imelenga kwa kazi ulofanya. At least huo ndio uelewa wangu.
 
Kwanini Rais Mstaafu Mkapa alikuwa hawakubali nyie waandishi wa Habari wa Tanzania,
Utusaidie na hilo Pasco
Kivumah, ni kweli Mkapa alikuwa anawadharau waandishi wa Tanzania, kwanza Mkapa mwenyenyewe ni mwandishi, kitendo cha kuwadharau waandishi wa habari, ni kitendo cha kusikitisha!. By nature Mkapa ni hot tempared person, ni mtu makini lakini kuhamaki kwa urahisi, hivyo aliwadharau waandishi wa habari wa Tanzania kwa hisia kuwa watamuuliza maswali ya kumuembarass, kuliko kuwa embarased, aliamua kuwapotezea.

Ukiona kiongozi yoyote ana shy away from the media, au ana shun away, ujue huyo ni kiongozi ambaye hajiamini!. Kuwaogopa waandishi wa habari ni lack of confidence. Japo wengi mlimuona Mkapa kama kiongozi shupavu na jasiri, mbele ya waandishi wa habari, alikuwa muoga kama kunguru ndio maana kuna wakati anaongea kama anagombana!.

Binafsi enzi za Mkapa, nimeshawahi ku force baadhi ya mahojiano naye. Most of the times, wanaozui mahojiano na viongozi wetu ni wale ma press secretaries wao. Enzi za Mkapa ndizo enzi zangu nikiwa mwandishi, niliwahi kuomba mahojiano naye, nikakataliwa. Kuna wakati nikiwa New York kuripoti UN GA, Mkapa alikuja na miongoni mwa ratiba zake akapangiwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Hawa viongozi wetu hujisikia fahari sana kuhojiwa na waandishi wa nje na kila wakifanya safari za nje ya nje, access ya waandishi ni free, lakini wakirudi home, ni makauzibe kwa kwenda mbele!. Basi Mkapa akiwa hapo UN akaandaliwa press conference na mimi kama mwandishi nikahudhuria. Kwenye press conference ile mimi nilijinyamazia kimya kabisa, sikuuliza swali lolote!. Press Sec wake akaniuliza, vipi wewe, mbona huulizi swali?, au lugha haipandi? Nikamjibu kama wana nia ya dhadi tumuuilize rais wetu maswali, wamuandalie press conference kama hizo kwa waandishi wetu wanyumbani, its awkward rais wangu mimi ndio nimuulizie maswali ughaibuni!. Press conference kama hiyo haikuwahi kutokea mpaka amestaafu!

Kwa wenye kumbukumbu ya mahojiano ya mkapa na Tim Sebastian kwenye Hard Talk wananielewa kuhusu Mkapa na media. Tena nahisi ndie yeye aliye ban kile kipindi cha "Kiti Moto!".
 
Mkuu Pasco!

Kwani waandishi huwa hawana mshahara/ posho kutoka kwenye chombo cha habari anacho kifanyia kazi?
Hivi mantiki nzima ya ‘bahasha kwa waandishi' huwa ni nini haswa? Sasa bahasha huwa ni zanini?
Je usawa wa ku riport habari utakuwepo kati aliyetoa / asiyetoa bahasha kwa mwaandishi?

Mkuu Pasco, aksante sana kutuamsha tuliokuwa tumelala binafsi nilikuwa silijui ki hivyo hilo tatizo la bahasha, nilidhani waandishi wachache tuu ( makanjanja) ndio wapokea bahasha kumbe hata waandishi wapiganaji na wao ni 'bahasha takers' ......tumekwisha!!
 
pasco wa JF!
je huoni bahasha km imetolewa kwa lengo la takrima huweza kum'badilisha muandishi aliyepokea bahasha hiyo na kwenda kuandika habari ya kurudisha shukrani ya takrima hiyo? (km hujanielewa ntafafanua zaidi)
Mkuu Zumbemkuu, nitafika huko kwenye bahasha za takrima na bahasha za asante kama appreciation na sio rushwa. Vumilia kidogo nitafika huko!?
 
Mkuu Pasco!

Kwani waandishi huwa hawana mshahara/ posho kutoka kwenye chombo cha habari anacho kifanyia kazi?
Hivi mantiki nzima ya ‘bahasha kwa waandishi’ huwa ni nini haswa? Sasa bahasha huwa ni zanini?
Je usawa wa ku riport habari utakuwepo kati aliyetoa / asiyetoa bahasha kwa mwaandishi?

Mkuu Pasco, aksante sana kutuamsha tuliokuwa tumelala binafsi nilikuwa silijui ki hivyo hilo tatizo la bahasha, nilidhani waandishi wachache tuu ( makanjanja) ndio wapokea bahasha kumbe hata waandishi wapiganaji na wao ni 'bahasha takers' ......tumekwisha!!
Papason kama umenisoma mwanzo, sio kila bahasha ni rushwa, nyingine ni genuinely lunch, transport au sitting allowance kihalali kabisa!? Nitafika huko kwenye uhalali wa baadhi ya bahasha.
 
Mkuu Pasco, labda kwa nyie wenye taaluma/uzoefu katika tasnia hii ya habari, vipi mambo haya ya bahasha yapo pia katika "nchi za wenzetu" au hata majirani zetu hapa - ke, ug, rw? Najua sio lazima tuige kila kitu lakini nataka kujua ,mifano ya "best practices" tu!

Nimeona umezungumzia kuhusu IDs - Pasco/Pascal Mayalla. Inawezekana ni kwa bahati mbaya tu au pengine kwa makusudi, lakini mara kadhaa "Pasco" umekuwa ukitoa maelezo ambayo kwa mtu mfuatiliaji wa habari katika media mbalimbali inakuwa vigumu kukufautisha na "Pascal Mayalla". Kwa mfano Pasco anarefer kipindi cha tv ambapo mtu fulani alikuwa anahojiwa/ulizwa maswali halafu "Pasco" anasema aliuliza swali fulani....wakati kwa member wa JF aliyetizama kipindi hicho anajua aliyeuliza swali hilo ni "Pascal Mayalla". Huu ni mfano tu wa jinsi wewe mwenyewe unavyochukua au kujifunua kwa id ya Pascal Mayalla. Anyway sina nia ya kuendeleza mjadala huu (kwani ni nje ya mada yako) lakini niliona ni vema wewe mwenyewe ukachuka responsibility ya kiwango cha anonymity unachokitaka.
 
Kwa maneno machache tu naomba niseme kwamba in most cases bahasha hizo ni rushwa!!!!! Miaka miwili iliyopita, nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari juu ya jambo fulani. Pale maelezo nilifanya booking ya ukumbi na kulipia (nakumbuka hata receipt sikupata kwani nilipigwa mkwara kwamba kwa tarehe ile na siku za karibu na hiyo tarehe ukumbi ulikuwa tayari uko booked). Receipt alikuwa suala kubwa kwangu kwa wakati ule, nilitaka nipate nafasi ya kukutana na waandishi wa habari.

Tangazo liliwekwa na waandishi wa habari walikuja kwa wingi, walikuwa kama 50 au 60 kutoka vyombo mbali mbali. Niliwaambia nilichotaka Watanzania wakijue na mwisho nilitoa nafasi ya maswali. Baada ya hapo nikatangaza kwamba mkutano umekwisha. Wengine waliondoka mara moja lakini wengine waligoma kuondoka na kuendelea kuniuliza maswali ingawaje mkutano tayari ulikuwa umefungwa. Zilipigwa picha nyingi tu. Kesho yake, kwa mshangao ni gazeti moja tu la Majira lilitoa ile habari. Magazeti mengine yote hakuna lililoandika. Nilipomuuliza jamaa yangu, akaniuliza kama nilitoa bahasha, nikasema la, akaniambia bila bahasha habari haziwezi kupewa nafasi kwenye magazeti. Kwa kifupi bila kutoa rushwa, habari zako haziwezi kuandikwa!!! Pasco hata ukijitetea vipi mnapokea rushwa ndio muandike habari.

Tiba
Mkuu Tiba, pole kwa yaliyokukuta hapo Maelezo. Kwanza naomba kukiri kuwa sometimes kuna habari huwa haziripotiwi kwa sababu mtoa habari hajatoa chochote, lakini pia, sio kweli kuwa ili habari yako itoke, ni lazima utoe chochote. Kuna habari kibao zinaripotiwa bila kutoa chochote na kuna wakati unatoa chochote na habari bado haitoki!. Determinant ya habari kutoka au kutotoka sio bahasha!.
 
Papason kama umenisoma mwanzo, sio kila bahasha ni rushwa, nyingine ni genuinely lunch, transport au sitting allowance kihalali kabisa!? Nitafika huko kwenye uhalali wa baadhi ya bahasha.

Mkuu Pasco!

Hivi ethics and compliances za uandishi wa habari zinaruhusu ‘bahasha / bakshishi’ ziwe alternative kwa lunch, transport, sitting allowances kwa mwandishi wa habari ?
 
I wish Doctors were given BAHASHAS. Bahasha yeyote is asking for a favour but mostly asking for haki yako. Ni unyama ulioje siku hizi kwenye ofisi za serkali ambazo unakwenda kutafuta haki yako lakini unajikuta hiyo haki inabidi kuinunuwa kwa bahasha tena nene.
 
Mkuu Pasco, labda kwa nyie wenye taaluma/uzoefu katika tasnia hii ya habari, vipi mambo haya ya bahasha yapo pia katika "nchi za wenzetu" au hata majirani zetu hapa - ke, ug, rw? Najua sio lazima tuige kila kitu lakini nataka kujua ,mifano ya "best practices" tu!

Nimeona umezungumzia kuhusu IDs - Pasco/Pascal Mayalla. Inawezekana ni kwa bahati mbaya tu au pengine kwa makusudi, lakini mara kadhaa "Pasco" umekuwa ukitoa maelezo ambayo kwa mtu mfuatiliaji wa habari katika media mbalimbali inakuwa vigumu kukufautisha na "Pascal Mayalla". Kwa mfano Pasco anarefer kipindi cha tv ambapo mtu fulani alikuwa anahojiwa/ulizwa maswali halafu "Pasco" anasema aliuliza swali fulani....wakati kwa member wa JF aliyetizama kipindi hicho anajua aliyeuliza swali hilo ni "Pascal Mayalla". Huu ni mfano tu wa jinsi wewe mwenyewe unavyochukua au kujifunua kwa id ya Pascal Mayalla. Anyway sina nia ya kuendeleza mjadala huu (kwani ni nje ya mada yako) lakini niliona ni vema wewe mwenyewe ukachuka responsibility ya kiwango cha anonymity unachokitaka.
mkuu ni the same person, ila pasco wa JF anataka sheria za JF zifuatwe, hapa kuna pasco wa JF, nje ya hapo ni Pascal Mayalla,
ina maana kwenye mijadala ya hapa JF mchukulie km Pasco wa JF.
 
Back
Top Bottom