MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Haiwezekani mwenzenu anapotea tu hivi hivi huku ninyi mko kimya kila mmoja na hamsini zake, mnaitia aibu sana tasnia ya habari nchini. Sina imani kabisa kama hata 80% ya wanahabari wetu wanazijua haki zao. Yaani mmeishia kupiga kelele zisizokua na impact yeyote kila mmoja anaogopa wasiojulikana.Kwakweli inashangaza sana.
Ndugu Azori Gwanda mwandishi wa mwananchi amepotea lakini jitahada za waandishi wa habari wenyewe kuhakikisha kua mwenzao anapatikana si za kuridhisha hata kidogo. Mazingira aliyopotea Azori hayana tofauti na alivyopotea msanii Roma Katoliki, lakini kwakua wasanii waliamua kuungana kwa umoja wao na kuamua nini wafanye, hatimaye walifanikiwa kumpata mwenzao. Lakini waandishi wetu wa habari kila mtu na hamsini zake.
Unajua hata magaidi wanapoteka mtu hua kuna kitu wanahitaji kutoka kwa maadui zao ili wamwachie mateka huru, ikiwa kuna chanzo cha kuanza kutafuta ni maringira gani alipotelea mtu ni lazima ukweli utafahamika kua yuko wapi, na ikishajulika yuko wapi basi kuna haja ya kuwauliza au kuwalikia waliomshikilia wamwachie hata kama ni kwa makubaliano flani flani. Lakini waandishi wa habari bongo kila mmojana na ugali wake bhaasi.
Yawezekana kabisa kuna mgawanyiko mkubwa sana baina ya wabahari wetu, ndio unaowafanya washindwe kuungana na kujuya yu-wapi mwenzao. TEF,MCT na vyombo vingine vinavyowakilishia taaluma hii ni vimebaki kama majina tuu, viongozi wake kila mmoja na maslahi yake.
Nimeamini kabisa lile suala la kutaka kila mwandishi walao awe na shahada ya kwanza ya chuo kikuu ni sawa na ni zuri pengine watu watajielewa.
CC
Paskali Mayala
Mwanahabari huru