Waandishi wa Habari mna matatizo gani? Mahojiano ya Salama na Kikwete yamenihuzunisha sana!

Sema sometimes ukiwa unafanya mazungumzo na mtu unayemheshimu kupindukia, au role model au unampenda mnoo unapatwa kama na wenge.

Hili nililiona siku ya kwanza Trevor Noah anafanya mahojiano na Obama. Yaani alikuwa anaishia kuchekacheka tu na kutabasamu muda wote, ikabidi Obama awe anaongea tu kama anahutubia.
too much confidence and mwisho wa siku unaharibu kabisa
 
Watu tusilaumu bure kuhoji watu wakubwa kunahitaji watu wenye elimu kubwa na ufahamu mkubwa labda niulize jina la Salama ni la kiislamu au kikristo? Tuanzie hapo kwanza
achana na udini point ni hapo kuwa swala la elimu au mtazamo pana unahtajika sana..nadhani bado kama taifa hatujapata mtu kama huyo kiukweli
 
Sawa lakini bado kulikuwa na mambo mengine ya muhimu ya kuzungumza kuliko kumuuliza Rais maswala ya kupika.
na dhani kiukweli hata ile interview aitoe tu ameharibu sana ..mtu unauliza evi unajua kupika sasa mkuu kama yule hata akijua kupika ana wafanyakazi wangapi na watu wa kumsaidia wangapi..nadhani pressure ilikuwa kubwa sana pia
 
Mimi naamini hata bila kuiongelea SIASA yaani ile safari ya maisha yake tu binafsi hadi kufikia urais na maisha ya baada ya Urais ingekuwa njema sanaa

Naelewa salama alichotaka ni kukaa katika ile safe side na kumuuliza the other side ya life yake ambayo wengi hatuijui lakini mwisho wa siku hata alivyoongelea havikuwa vya kushtua kiasi. Kiufupi ni matarajio ya watu yalikuwa makubwa sana kuliko kipindi kilivyokuwq
lakini pia vipindi hivi vya interview wengi wao wanaofanya sikuhizi wamekosa content nzuri..kila mtu anahoji tu ili mradi basi na hakuna lingine
 
sasa tusaidiane kuwatoa upumbavu wao..kiukweli ni nafasi hadimu sana mtu kama JK kukaa nae kiti kimoja alafu maswali unayouliza mmhhh kiukweli salama atuombe radhi kabisa
Umeeleweka ndugu yangu ila jitahidi kwenye a usiweke ha no adimu sio hadimu, Asante
 
Kwa hyo ulitaka amuulize kuhusu watu wasiojulikana?.
ANGEJIBU?
au ulitaka amuulize kuhusu Bei ya cement?
muwe mnaangalia na AWAMU.
haya yote chanzo Ni magufuli na ccm yake mjitafakari.
 
Usiwalaumu hao watu.
Nani mwenye uwezo wa kujadili ishu nzito nzito za nchi hii? Hadharani?
Gazeti la majira lipo wapi?
Sio TCRA ni Wizara ya Habari! Redia nyingi sana zitakosa watu! Mfano Clouds, E fm na Wasafi! Kwa mfano pale EFM eti Kingwendu,Steve Nyerere, Musa Kipanya,Swebe, Sina Mario's na wengine wengi hawana elimu ya uandishi ni janja janja tu,Rudi Wasafi FM nako yale yale,Hadi kina Baba Levo eti na wao watangazaji,ndiyo maana hua wanaongea hovyo hovyo tu Radioni
 
Nafikiri aina ya kipindi pia inachangua , salama ametumia ubunifu wake kuunda brand yake ya channel yake , hata hao unaowaona wakihojiwa wanaenda pale wakijua it's about life experience as a person, nothing less or more ,

Ukifatilizia vizuri utakuja kujua Kuna phase ya kuwaomba interviews , wengine hawatokei kabisa hapo , na uwezekano ni kuwa wanaotokea huwenda wanaotokea kwa nakubaliano ya hawataki maswali flani na flan..
 
Mkuu Salama Na siyo kama Hard Talk.

Angalia na maudhui ya kipindi yenyewe.

Nadhani kile ni kipindi cha mambo soft soft sana ndio maana JK alikuwa anaulizwa mpaka mambo ya wake zake na mengine ya kupika.

Binafsi nilikereka Kwasababu JK ana lundo la mambo ya kuzungumza na ni mzungumzaji mzuri kwasasa lakini hakupata nafasi hiyo.

Na Kwa siasa zetu zilivyo akianza kuonekana sana kwenye TV akizungumzia mambo mazito ataonekana siyo mzalendo, anawashwawashwa, anakwamisha kazi au anaingilia utawala uliopo.
JK anatoa kitabu kasema mwaka huu kabla ya June, na hawezi kuongea yote hata kuna swali alijibu kuwa mengine yatakuwa kwenye kitabu sasa hawezi kuongea yote pale wakati kitabu kinakaribia kuisha. Mimi nasubiri sana hicho kitabu najuwa nitapa mengi kama cha Mkapa nimetoka kukimaliza kusoma kuna mambo mengi ya kujifunza una enjoy kusoma kwa kweli. Katika mahojiano kasema wazi kitabu kitakuwa na mambo yote.
 
Sio kitu rahisi brother ila angeandaa maswali at least ya kufanya kipindi kiwe memorable yaani mtu akitazama atoke na interest ya kurudia kukitazama au mafunzo flani muhimu. ila sikuona hayo mkuu ndio maana watu wakawa dissapointed
JK anaandika kitabu na kasema pale subirini kitabu kila kitu ataweka sasa aje ayaongelee yote pale. Tuje kununua kitabu ndio kumbukumbu bora kabisa utasoma wewe na wengine watakuja kusoma ina faida kubwa kuliko mahojiano ya dakika 45. Kitabu ndio kila kila nakasema kabla ya june kitatoka kwa lugha mbili.
 
Interview ilikua chini ya viwango mno,

Kiufupi kampotezea muda Rais wetu.

Angetafuta watu wanaojua mapishi kuliko kumuita Rais Mstaafu na kumuuliza mambo ya mapishi.

Ila naweza kuwa nakukomaza kwa mambo magumu magumu kwakua umezoea kukaa jikoni na umbea wa Instagram kwahiyo ilikua sawa kabisa kwako.
Dogo usifikiri kumuhoji rais ni Kama kumuhoji ebitoke....lazima kuna mipaka iwepo ili kutokuharibu hali ya hewa
 
Kabla ya kuwa mwanasheria, nilisoma kozi ya uandishi wa habari na utangazaji wa radio na Tv, nimefanya kwenye Radio ndani na nje ya nchi.

So nafahamu basics za uandishi wa habari. Nikaachana nako kwa maana sikuona kama kuna future huko.

So ukiniambia nianzishe kipindi unanirudisha nyuma more than 20 years ago. Na sita rudi huko.

Ninapokosoa nakosoa kama mtaalam naelewa ninachokiandika hapa.
Mtaalamu wa kuwinda ndege
 
kwanza salama hana adabu, anamkaliaje mzee wetu mapaja nje vile!! anataka kumtia majaribuni au?
 
Kila kipindi kina walengwa wake kile cha salama ni kipindi cha burudani tu na umbea umbea siyo cha mambo serious hata akileta watu serious anawauliza maswali ya kawaida. Siyo kama kipindi cha Generali Ulimwengu, yani ni jambo la kushangaza ukiwa unategemea Salama aulize maswali yaiyojikita kisiasa zaidi.
Ila why hakumuuliza Fatma kuwa una mume, au watoto 🤣🤣🤣
Audience tungependa kujua hilo.
 
Ila why hakumuuliza Fatma kuwa una mume, au watoto 🤣🤣🤣
Audience tungependa kujua hilo.
Alimuuliza mkuu, na akasema mume wake ni daktari mkubwa na walikutana akiwa na miaka sijui 12 wakawa marafiki hadi wakaja kuoana na wana watoto wawili.
 
Wajumbe tulikaa na tukampangia maswali ya kuuliza maana waandishi wa habari wa Sasa hivi kuchafua hali ya hewa hawajambo.
 
Sijui kidhungu,lakini hiki hapana! You have freedom of Speech, but I can not guarantee freedom after your speech!
Kwa kitaalamu watu wa aina yako tunawaita walking dictionary ,mnakalili mnakua mmfungwamo kwenye mlichokalili
 
Waandishi wa habari wa Tanzania hawana weledi kabisa kabisa.

Nimeangalia mahojiano ya Rais Mstaafu na Salama Jabir kwakweli inasikitisha mno. It is a Golden opportunity wasted.

Mtu unapata nafasi ya kuzungumza na Rais badala ya kuuliza maswali yenye tija na kutufanya watazamaji tujifunze mambo ya msingi ya kitaifa wakati kuna mambo kadhaa ya kupata opinion yake, unaishia kumuuliza Rais eti tofauti ya kuwa babu na baba ni ipi? Au unazungumziaje kifo cha Kobe Bryant. Jamani?

Next time ukiwa na mgeni kama huyu toa taarifa mapema. Ambia watazamaji watume maswali yachuje baki nayo yale muhimu tu, then uliza kama unakosa cha kuuliza.

Mnatukosea Sana waandishi wa habari kutuletea mambo rahisi rahisi tu kujaza ubongo wetu.
Wewe ndo una tatizo... umeshindwa kung'amua
Context TV station yenyewe unaiona, its not about hard news ni kama infotainment na vipindi vyake vingi vipo hvy na audience yake ndo ipo hvyo.
Si kila kitu kwa kila mtu!!
 
Back
Top Bottom