Waandishi wa Habari mna matatizo gani? Mahojiano ya Salama na Kikwete yamenihuzunisha sana!

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,308
2,000
Waandishi wa habari wa Tanzania hawana weledi kabisa kabisa.

Nimeangalia mahojiano ya Rais Mstaafu na Salama Jabir kwakweli inasikitisha mno. It is a Golden opportunity wasted.

Mtu unapata nafasi ya kuzungumza na Rais badala ya kuuliza maswali yenye tija na kutufanya watazamaji tujifunze mambo ya msingi ya kitaifa wakati kuna mambo kadhaa ya kupata opinion yake, unaishia kumuuliza Rais eti tofauti ya kuwa babu na baba ni ipi? Au unazungumziaje kifo cha Kobe Bryant. Jamani?

Next time ukiwa na mgeni kama huyu toa taarifa mapema. Ambia watazamaji watume maswali yachuje baki nayo yale muhimu tu, then uliza kama unakosa cha kuuliza.

Mnatukosea Sana waandishi wa habari kutuletea mambo rahisi rahisi tu kujaza ubongo wetu.
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,846
2,000
Niliona hayo mahojiano kwenye whatsapp status ya ndugu yangu, kipande cha kwanza nasikia anamwabia hivi unajua kama tunakupenda, baada ya hapo hata sikuangalia huo uharo tena.

Tunampemda yeye na nani, nani kamtuma akamwambie tunampenda Kikwete?

Ndio maana tcra inataka waandishi wawe angalau wameenda shule, hawa wa Tanzania wengi ni makanjanja, zero brain, wanafanya hadhi ya waandishi wa habari Tanzania inashuka kila siku.

Hovyo sana.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,480
2,000
Waandishi wa habari wa Tanzania hawana weledi kabisa kabisa....
Mkuu Salama Na siyo kama Hard Talk.

Angalia na maudhui ya kipindi yenyewe.

Nadhani kile ni kipindi cha mambo soft soft sana ndio maana JK alikuwa anaulizwa mpaka mambo ya wake zake na mengine ya kupika.

Binafsi nilikereka Kwasababu JK ana lundo la mambo ya kuzungumza na ni mzungumzaji mzuri kwasasa lakini hakupata nafasi hiyo.

Na Kwa siasa zetu zilivyo akianza kuonekana sana kwenye TV akizungumzia mambo mazito ataonekana siyo mzalendo, anawashwawashwa, anakwamisha kazi au anaingilia utawala uliopo.
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,308
2,000
Niliona hayo mahojiano kwenye wahstapp status ya ndugu yangu, kipande cha kwanza nasikia anamwmabia hivi unajua kama tunakupenda, baada ya hapo hata sikuangalie huo uharo tena...
Kamkosea Sana Rais wetu mstaafu,

I wish mtu mwingine amtafute yule mzee wetu amfanyie interview ya maana.

You can imagine unapata audience na Rais unapoteza kizembe vile.
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,124
2,000
Hata mimi nilikuwa nategemea itakuwa "the best" maana katika watu aliowaalika nadhani Kikwete angekuwa na vitu vingi sana vya kuzungumzia hata kama ukiitoa siasa kama alivyofanya Salama.

Mwisho wa siku interview ilikuwa ya kawaida sana, siwezi hata kui_rate vizuri ukilinganisha na baadhi ya zilizopita
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,480
2,000
JK anafahamu Sana historia ya nchi hii, kumuuliza maswali na kupika ni kumkosea heshima,
...
Kumbuka Drama alizotengeneza baada ya kusema yeye na Mkapa walipanga kipato cha kati kiwe 3,000.

Angalia pia alipokuwa anazungumzia Nyerere kuhusu mambo ya Kujimwambafai. Akaishia kufokewa na kina Ally Hapi !!!
Mkuu utawala huu unaishi kwa hofu kuu na kujishukushuku muda wote.

Unaweza kuongea kitu kingine, wao wakawa na tafsiri tofauti na kuanza kukushambulia.
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,124
2,000
Mkuu Salama Na siyo kama Hard Talk.

Angalia na maudhui ya kipindi yenyewe...
Mimi naamini hata bila kuiongelea SIASA yaani ile safari ya maisha yake tu binafsi hadi kufikia urais na maisha ya baada ya Urais ingekuwa njema sanaa

Naelewa salama alichotaka ni kukaa katika ile safe side na kumuuliza the other side ya life yake ambayo wengi hatuijui lakini mwisho wa siku hata alivyoongelea havikuwa vya kushtua kiasi. Kiufupi ni matarajio ya watu yalikuwa makubwa sana kuliko kipindi kilivyokuwq
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,124
2,000
Nadhani maudhui hayakuwa ya hardtalk
Exactly lakini haimaanishi kusiwe na serious issues kiasi, kuna watu kama Idris au Taji Lihundi aliwahoji kuhusu life lao na bado kuna vitu vingi sana unajifunza kwenye safari ya maisha yao.

Kwa kikwete ilikuwa tofauti na labda kwa sababu alisema mambo mengi atayaongelea kwenye kitabu chake, ila bado naona ile interview Salama alifanya under peformance
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,480
2,000
Exactly lakini haimaanishi kusiwe na serious issues kiasi, kuna watu kama Idris au Taji lihundi aliwahoji kuhusu life lao na bado kuna vitu vingi sana unajifunza kwenye safari ya maisha yao. Kwa kikwete ilikuwa tofauti na labda kwa sababu alisema mambo mengi atayaongelea kwenye kitabu chake, ila bado naona ile interview Salama alifanya under peformance
Sema sometimes ukiwa unafanya mazungumzo na mtu unayemheshimu kupindukia, au role model au unampenda mnoo unapatwa kama na wenge.

Hili nililiona siku ya kwanza Trevor Noah anafanya mahojiano na Obama. Yaani alikuwa anaishia kuchekacheka tu na kutabasamu muda wote, ikabidi Obama awe anaongea tu kama anahutubia.
 

S T O I C

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,371
2,000
Hata mimi nilikuwa nategemea itakuwa "the best" maana katika watu aliowaalika nadhani Kikwete angekuwa na vitu vingi sana vya kuzungumzia hata kama ukiitoa siasa kama alivyofanya Salama.
Mwisho wa siku interview ilikuwa ya kawaida sana, siwezi hata kui_rate vizuri ukilinganisha na baadhi ya zilizopita
Mkuu umenena angalau angetupa historia ya hili taifa...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom