Waandishi wa habari kwanini hamkulisema hili!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari kwanini hamkulisema hili!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Sep 13, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Wakuu ndani ya jukwaa letu la siasa nami niungane na wenzangu wote waliotangulia kulaani vikali ukatili uliofanywa na kufanyiwa tasnia hii ya habari,kwa mwana habari wetu toka kanda ya nyanda za juu kusini,kudhalilishwa na hatimaye kudhulumiwa nafasi yake ya kuishi duniani.

  Imekuwa ni mila na desturi zetu binadamu kumtupia lawama Mungu kwa kisingizio cha kusema kazi ya Mungu haina makosa,lakini kwa hili la Mwangosi serikali haikwepi lawama,ina stahili kuwajibika kwa kuelea mambo haya kiasi cha kufikia hatua hii ya kudhulumu haki ya msingi ya mwanadamu ya kuishi.

  Matukio mengi yanayo fanywa na chombo hiki cha dola tumekuwa tukilalamika mara kwa mara,lakini serikali hii imekuwa ikiyafumbia macho na kusababisha hali tete ndani ya nchi inayo jinasibu kuwa kisiwa cha amani.Mzaha mzaha siku zote huzaa usaha ,leo yametimia mwandishi ameuwa,haki yake imedhulumiwa mbaya zaidi POLICE FORCE UNIT imepora laptop na kamera ambazo zilitumika kama vitendea kazi vya marehemu.

  Kinacho sikitisha kwa sana ni utiifu wa jeshi hili ambalo siku zote limekuwa likitoa kiapo cha mtiifu kwa rais na nchi yetu,lakini kinyume cha kiapo hicho jeshi limejaa majambazi,vibaka,matapeli na wachonga ngenga.

  Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mh Leonard Derefa aliwahi kusema jeshi hili livunjwe na tuunde jeshi linalo endana na hali ya wakati uliopo, lakini alibezwa na wenzake kwa kuwa tu walijua nia zao ovu zilizoko nyuma ya pazia.

  Sasa nijikite kwenye nia hasa ya mada yangu ya leo,waandishi walio andamana sauti zao za uchungu zilipasua anga la nchi hii lakini haikutosha kuwakemea polisi pekee yake na kuiacha serikali inayo kitumia chombo hiki cha usalama wa raia na mali zake kutenda kinyume na matakwa ya jeshi hilo.

  Bila mashinikizo ya kisiasa ambayo yalitumika kuvuruga mkutano wa ndani wa CDM hali hii isingetokea,serikali iliyoko madarakani inaona chama chake ndicho pekee kina haki ya kufanya shughuli za kisiasa,hali hii ndio iliyosababisha matukio haya ya dhuluma dhidi ya haki.

  Mabaya zaidi,walishindwa hata kukemea vyombo vyetu vya habari ambavyo vimejikita kiitikadi zaidi kwa kuwa na maslahi fulani bila kujali tasnia hii ya habari ndiyo mhimili pekee wananchi wanao utegemea kuelimisha umma na kuwafumbua macho kujua haki zao za msingi.Nilitegemea kauli kali toka kwenye vinywa vyao kulaani ukiritimba na upotoshaji wa habari unao fanywa na baadhi ya vyombo vya habari kwa nia ya kuibeba serikali na watu fulani ndani ya jamii kwa maslahi ya uchumia tumbo.

  Serikali haikwepi lawama na ndo maana hata tume yake inaonekana magumashi,lakini cha ajabu waandishi wa habari hili hawakuliona.Polisi wetu ni sawa na mbwa,mbwa anapotumwa na bwana wake anachojua ni kutimiza wajibu hata kama anayekwenda kumng'atwa hana hatia,ndo maana nachelea kusema serikali inatakiwa ilaaniwe kwa matendo yake ya kulitumia jeshi hili vibaya ili kulinda uozo uliopo.

  Kilichojiri pale Jangwani ilionekana kama ni kelele ambazo hazimzuii mwenye nyumba kukosa usingizi,tulitegemea kusikia hotuba nzito ikitolewa kwa mpangilio mzuri ikiwa ni pamoja na kutumia damu ya Mwangosi iliyomwagika kuanika uovu wote unaofanywa na serikali kwa kupitia jeshi hili,hapo maandamano yenu yangekuwa na tija.

  Hatujui nini kauli mbiu ya maandamano yenu kwa kuwa hamkuweka mambo yenu kimpangilio.Mwisho,nasema silaha za moto na mabomu ya machozi idadi yake ni ndogo kuliko idadi ya wapigania haki wa kweli dhidi ya dhuluma wanayo fanyiwa wananchi.

  RIP Daud Mwangozi.
   
 2. real thinker

  real thinker Senior Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kaka pole coz umeongea kwa uchungu ila ucjal soo wababe wa hii nchi watajuta coz their days to be on power are numbered. Mwangosi natumain mungu atakuwa nawe uko uliko, amen!
   
 3. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  asante kaka ila pole pekee haitapooza mioyo ya wanyonge mpaka pale Watanzania watakapo ijua haki yao na kuamua kuisaka.Haiwezekani kila mtawala ana fanya majaribio kwa wapiga kura wake lengo lake hasa nini kama si kutafuta re action
   
 4. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata mimi napata mashaka makubwa juu ya nia thabiti ya wanahabari kushughulikia kadhia hii. Nimewasikia viongozi wao wakitamba eti watawafundisha watanzania namna sahihi ya kushughulikia matatizo kama hayo katika nchi hii kwa kuwa wao ni weledi na wenye busara. Cha kushangaza mpaka sasa wanachuma majani eti wauue mti badala ya kukata mizizi!
   
 5. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Umaskini,uoga kutokuwa na uhakika wa maisha umepelkea Watanzania kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao bila kujali uzawa na uzalendo wao.Vitsho dhihaka,kejelinakila aina ya ubaya itapelekea nchi kuto kukalika kutokana na matabaka ya wenye nacho ambao wameishikilia serikalina wanyonge ambao hawajkui kesho yao itakuwaje.
   
 6. G.T.L

  G.T.L JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Tuko nyuma ya mawazo yako MKUU.Asante Saana.
   
Loading...