Waandishi wa Habari Kukamatwa na Polisi ni Uonevu!. Serikali Yatakiwa Kutenda Haki Kwa Kuheshimu Uhuru wa Habari, na Haki za Binadamu-Jicho Letu.

Wanabodi

Matukio ya Waandishi wa Habari Kukamatwa na Polisi katika utekelezaji wa majukumu yao, yameelezwa baadhi ni uonevu tuu wa vyombo vya dola, hivyo umetolewa mwito kwa Serikali na mamlaka zake, kuacha uonevu kuwaonea waandishi wa habari, hivyo serikali imetakiwa kutenda haki kwa kuzingatia uhuru wa habari, na kuheshimu haki za binadamu.

Wito huo umetolewa kwenye mjadala wa kipindi cha "Jicho Letu Ndani ya Habari" kinachotangazwa mubashara na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi.

Kwa wenye nafasi, angalia Star TV, wengine andamana nami

P.
Vipi umeacha kuripoti mambo yanayo andikwa kwenye THE ECONOMIST maana yanamchafua msukuma mwenzio..kama ulivyoripoti ya Kabendera!
 
Kweli wametoleana uvivu!

Hii ya RC wa DSM enzi za uvamizi wa clouds lilimuumbua yule mtangazaji!

Na pale ndo waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari mlipoonyesha kutokuwa pamoja na kutanguliza maslahi binafsi mbele
Wanatanguliza tumbo badala ya utu!
 
Vipi umeacha kuripoti mambo yanayo andikwa kwenye THE ECONOMIST maana yanamchafua msukuma mwenzio..kama ulivyoripoti ya Kabendera!
Hakuna uthibitisho kuwa ndiye ripota wa The Economist, mimi naendelea kuripoti kila kinachoripotiwa na the Economists kuhusu Tanzania, regardless ripota ni nani, I just present facts of what it is reported and not about the reporter.
P
 
Mkuu P, upo sawa tatizo kwa haya ya karibuni huenda alietamka 'kamata huyo' yupo juu sana Mawinguni.
 
Wanabodi

Matukio ya Waandishi wa Habari Kukamatwa na Polisi katika utekelezaji wa majukumu yao, yameelezwa baadhi ni uonevu tuu wa vyombo vya dola, hivyo umetolewa mwito kwa Serikali na mamlaka zake, kuacha uonevu kuwaonea waandishi wa habari, hivyo serikali imetakiwa kutenda haki kwa kuzingatia uhuru wa habari, na kuheshimu haki za binadamu.

Wito huo umetolewa kwenye mjadala wa kipindi cha "Jicho Letu Ndani ya Habari" kinachotangazwa mubashara na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi.

Kwa wenye nafasi, angalia Star TV, wengine andamana nami

P.
Worse comment
 
Hilo linaongelewa na kujadiliwa sana... hadi kukemewa kwa nguvu zote...

Ila unafahmu kinachowapata wanaojitahidi kutafuta uhuru...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom