Waandishi wa Habari kugoma kuandika habari za Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa Habari kugoma kuandika habari za Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by makoye2009, Sep 13, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Ndugu wanahabari popote mlipo,

  Napenda kuwapa ushauri ambao mnatakiwa kuufanyia kazi. Baada ya mshikamano wenu wa maandamano kupinga mauaji ya mwandishi mwenzenu marehemu Daudi Mwangosi sasa mnatakiwa muende hatua nyingine mbele. Hatua hii bila shaka itawasaidia nyie wenyewe na umma wa Watanzania kuwakomboa kutokana na hili zimwi au jinamizi la utawala wa CCM.

  Mnachotakiwa kufanya sasa ni kususia au kugoma kuandika habari zozote zinazohusiana na Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi ambalo liko chini ya Wizara hiyo. Hii itasaidia kwa Serikali kuchukua hatua zinazostahili kuhusiana na mauaji ya Daudi Mwangosi. Mpaka sasa inavoonekana serikali inajaribu kucheza na akili za Watanzania kwamba kuna kitu kinafanyiwa kazi kuhusu mauaji hayo ya Nyololo-Iringa. Lakini ukweli wenyewe kwa kila dalili inavyoonyesha ni kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi hawana nia ya dhati ya kulishughulikia swala hili kwa umakini!

  Inasikitisha kama siyo kuchekesha kuona kwamba ni askari mmoja tu ndiye anadaiwa kukamatwa na kuhusishwa na mauaji ya Mwangosi ilhali walioshiriki kwenye mauaji hayo ni zaidi ya askari 10 kama picha zinavyoonyesha! Tunataka asjkari wote waliohusika na mauaji hayo wakamatwe. Baada ya hapo tunataka RPC mkoa wa Iringa Bwana Michael Kamuhanda akamatwe mara moja kwani yeye ndiye mtuhumiwa nambari 1 na ndiye aliyetoa amri ya kupigwa na kushambuliwa kwa Mwangosi akiwa eneo la tukio kule Nyololo. Laiti huyu RPC asingefika Nyololo na kuamrisha hao maafande wake leo hii tusingelikuwa tunazungumzia habari ya mauaji ya Daudi Mwangosi!

  Pia tunataka Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Nchimbi ajiuzulu mara moja akifuatiwa na Kamanda wake Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Mwema. Tunataka pia Vifaa vya kazi vya marehemu Mwangosi vikiwemo Kamera ya Video na Laptop yake virudishwe mara moja vikiwa intact(bila kuchakachuliwa ya yale yaliyorekodiwa siku hiyo).

  Mwisho kabisa tunataka Rais Kiwete aunde Tume Huru jharaka iwezekenavyo ili kushughulikia mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi wa Iringa na yule muuza Magazeti wa Morogoro-Somebody Ally. Waandishi wa Habari jueni kuwa kama mtakomaa tu na kesi ya Mwangosi na mkaacha matukio ya nyuma kama hili la Morogoro mtaonekana kuwa mko-biased(upendeleo)!Tayari watu wanalalamika chichini huku mtaani kwamba kwanini Waandishi wa habari wamelishupalia sana hili la Mwangosi?Mbona Morogoro hatukusikia kelele na maandamano ya waandishi kama sasa?Au kwa vile ni mwenzao? Hii picha kwa jamii siyo nzuri.

  waandishi jueni kuwa nyie ni jeshi lenye nguvu kubwa.Kila Mtanzania na Serikali wanajua kuwa Media ni Mhimili wa 4 baada ya Serikali,Bunge na Mahakama. Mnaweza kuzungumza,kushawishi na kuleta Mabadiliko katika Taifa hili ambalo kwa chini ya Uongozi wa CCM taifa letu limeanza kupoteza haki zake za msingi. Tumieni kalamu zenu kwa weledi na umakini mkubwa kwani umma wa Watanzania uko nyuma yenu.Huu ndiyo ushauri wangu kwa leo.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. D

  Dik JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Point noted kamanda
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja mkuu
   
Loading...