Kumezuka tabia ya waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro kujihusisha na utapeli kwa kuchukua fedha za watu (wadau) wakidai ni gharama za kutuma habari lakini kinachotokea ni wizi mtupu.
Juzi mama mmoja wa Uru Mjini wilaya ya Moshi Vijijini ametoa Tsh. laki 4 kwa waandishi wa habari wanne ili waripoti tukio la mtoto wake mwenye Utindio wa ubongo kubakwa na kupewa ujauzito, mpaka sasa waandhi hao watatu wa TV na mmoja wa gazeti wameshindwa kutoa habari yake.
Huu ni utapeli wa aina yake, ni jukumu la viongozi wa Press Club kilimanjaro kuchukua hatua dhidi ya waandishi hawa ambao ni wanachama wenu na hata kama si wanachama wenu wanachafua tasnia ya habari.
Ni hayo tu kwa leo, wasiporudisha tunawaanika chap ili vyombo vya vichukue hatua, ushahidi upo na mhanga yupo.

- Tunachokijua
- Baada ya kutokea kwa dokezo hili JamiiForums imefuatilia tukio hili Kwa kupiga simu kwa wahusika ili kubaini ukweli wake.
Kwanza, Waandishi wa habari, Mama wa mtoto na mtoto wamekiri kutokea tukio la kubakwa kwa mtoto aliyekuwa anasoma ambaye kapata ujauzito. Inaelezwa taarifa hizo hazijatolewa kwenye vyombo vya habari hadi sasa kwasababu anayetakiwa alizungumzie na kuweka mizania wa hiyo taarifa ni RPC wa Kilimanjaro ambaye bado anasubiriwa RPC lizungumzie kwa sababu kesi ipo bado polisi na Waandishi wanatakiwa "wabance Story".
Jamiiforums imemhoji mama wa mtoto huyo (Jina tumelihifadhi) ili kujua kama alitoa kiasi cha laki nne ili Waandishi waripoti tukio la kubakwa kwa mwanaye amekana na kusema hana uwezo wa kutoa hiyo fedha sababu anafanya biashara ndogo ndogo. Mama huyo anaeleza kuwa yeye ni mfanyabiashara ya matunda na kipato chake ni kidogo sana hawezi kumudu kulipia laki nne kama taarifa zinavyoeleza.
Naye, mtoto wa Kiume wa Mama huyu ambaye ni kaka wa huyo anayeelezwa kubakwa amekanusha suala la mama yake kutoa laki nne kwa Waandishi wa habari. Huyu Kaka wa Mtoto aliyebakwa ndiye alitoa taarifa kwa wanahabari ili wafuatilie kesi ya kubakwa kwa mdogo wake sababu haipelekwi Mahakamani.
Aidha, Kiongozi wa Club ya waaandishi wa habari wa mkoa huo amekana na kusikitishwa na habari zinazodai kuwa waandishi hao wa Mkoa huo wamelipwa pesa ili watoe hizo habari kitu ambacho si kweli.