Waandishi wa Habari Iringa wamemgomea nani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa Habari Iringa wamemgomea nani??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by moshingi, Mar 15, 2012.

 1. m

  moshingi JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF,
  mtakumbuka hivi karibuni waandishi wa habari wa Iringa walijitokeza humu wakidai kuwa watagoma
  kuandika habari za serikali mkoani humo kwa vile walinyimwa posho kwenye ziara ya makamu wa rais
  na kwamba walilazimika kulala kwenye gari...lakini haikutosha walifanya maandamano ambayo watu wengi humu waliyashangaa kwani ni jambo lililo wazi marupurupu ya safari za kikazi mtumishi hulipwa na mwajiri wake vinginevyo
  wangesema kuwa serikali ya mkoa ni mwajiri wao....Baada ya hapo tumeshudia matukio mengi makubwa yanatokea
  huko Iringa hayaripotiwi kwa uma, mfano majuzi tu chuo kikuu cha Mkwawa kiliungua moto habari hiyo haikupata nafasi...
  Kisha limetokea tukio baya la Ujambazi Mhadhiri wa Tumaini University - Iringa raia wa Marekani Dr. Monica alivamiwa nyumbani kwake Gangilonga na kujeruhiwa vibaya kwa sasa amepelekwa Nairobi kwa ndege ya AMREF kutibiwa...habari hii pia haijaripotiwa...sasa kama waandishi hao wamegoma tujiulize wamemgomea nani?? Karibuni tulijadili hili...
   
 2. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe wadhani wanamgomea nani? Labda hawajagoma bali wanaona matukio yote yaliyotokea hayana uzito wa kutokea katika vyombo vyao vya habari ama wameyatuma lakini wahariri wao hawajayapatia uzito wa kutokea kama habari katika vyombo husika.
   
Loading...