Waandishi wa hababari wamekuwa wabaguzi kuripoti habari za uvunjifu wa haki za binadamu. Ila wao yakiwakuta ndio midomo juu

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kuna habari inatembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwandishi wa gazeti la mwananchi huko Zanzibar amepigwa na kudhalilishwa na wana usalama huko Zanzibar. Inadaiwa maafande wa KMKM walimvamia na kumpa kichapo kisha kumtesa na kumlazimisha avunje simu yake aliyotumia kuwapiga picha wakati wakifurusha wamachinga maeneo ya Darajani Zanzibar.

Lakini hawa watu wanatabia mbaya sana kama ni raia wa kawaida amepatwa na madhara kama haya hawawezi kuripoti kama wakiripoti ni kwa shingo upande sana.

Hii tabia ya kujipendelea nyie tu huwa ni uzembe usiofaa kabisa. Na kinyume na maadili ya kazi yenu
 
Lakini angalao Waandishi wa Zanzibar walikuwa wanajitutumua kuliko hawa wa Tanganyika waliokuwa wameufyata Mkia
 
Back
Top Bottom