OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,180
- 103,672
Wakati Simba wanaelekea katika kufanya mabadiliko ya uwendeshaji wa klabu hio kulitokea Makundi matatu
1 Waandishi wa Habari za Michezo
2 Watangazaji wa Habari za Michezo
3 Wachambuzi wa Habari za Michezo
Makundi haya kwa Umoja wao yote yaliungana kuiponda klabu ya Simba na hasa muwekezaji Mo Dewji
Wengine walifika mbali zaidi kwa kuonyesha kuwa hili jambo la uwekezaji halifai na halina faida yoyote ile na kuionyesha jamii kuwa Mo Dewji ni kama vile ni mnyonyaji na anataka kuimiliki Klabu ya Simba pasi na hio klabu kupata faida yoyote ile
-Maulid Kitenge* aliamua kuongoza japo la wanahabari wake kumpa muda mrefu Mzee Kilomoni ili tu ionekane kuwa Simba imeporwa na Mzee kilomoni anachokisimamia yupo sahihi. Ilifikia wakati kipindi chake cha michezo mada ni Simba na FCC tu yaani yeye alijipambanua ni mfuasi wa wapinga mabadiliko ya Simba.
Ni kweli, ukweli huchelewa sana kueleweka leo Yanga wemefuata yaleyale waliyokuwa wakiyapinga hao Waandishi, watangazaji na wachambuzi wa habari za michezo.
Na hao hao wote bila ya chembe ya aibu wameisifia sana Yanga kama vile hili jambo ni jipya hapa Tanzania. Ukweli mpira wa Tanzania unahitaji uvumilivu kama walionao Viongozi Wanachama, Mashabiki na Wachezaji wa Simba licha ya juhudi kubwa ya kuliinua na kulipigania soka letu kimataifa bado Simba inapigwa vita sana na baadhi ya watu hasa Waandishi na Wachambuzi wa habari za michezo
Licha ya vitimbi vyote hivi tunawaambia bado mtaiga kila zuri au kila lililofanywa na Simba katika kuelekea mafanikio yenu kubwa acheni roho mbaya michezo si UADUI Michezo ni FURAHA na kizuri kiigwe na kibaya kiachwe.