Waandishi na wabunge mnamuogopa Rashid Othman? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi na wabunge mnamuogopa Rashid Othman?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 9, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Pamoja na madudu yote yanayotokea na kuhatarisha usalama sijaona hata gazeti au chombo chochote cha habari kinacholeta majibu ya RO kuelezea uzembe na matukio haya mbalimbali. Haiwezekani matukio yote yaliyotokea kuanzia kashfa za ufisadi na sasa masuala ya usalama ambayo yanatishia hata usalama wa Rais hajawahi kukaa chini na kuzungumza na waandishi kutuelezea inakuwaje?

  Kinachoudhi hakuna hata wabunge wenye ujasiri wa kutaka maelezo juu ya masuala haya ya usalama hadi jambo fulani baya litokee ndio wawe wa kwanza kusema ni mapenzi ya Mungu na kuwa "tusitafute mchawi"

  kweli?
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Rashid Othman ni nani kwani?
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Haaaahaaaa! Kuna mtu ananiambia mzigo mzito mtwike mnyamwezi....watu wa pwani sisi hayo makazi mazito mazito hatuyawezi!Lol
   
 4. stanluva

  stanluva Senior Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jaribu kufikiria mara 3 ulishawahi kusikia jina hili au? Simple way nenda kwenye web page ya google! Kisha chapa Rashid Othman utapata majibu!
   
 5. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkurugenzi wa UWT
   
 6. B

  Bull JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MK, Unabifu na Rashidi Othmani?

  Saidi Mwema, mkuu wa Rushwa alishaongea kuhusiana na kila tatizo linahusika na usalam, hapa kuna Structure za usalama wa nchi ambazo kila kiongozi anae husiana na usalam anasehemu zake anazo ziangalia, Mfano Jeshi pia linaangalia usalama wa Nchi, ulishawai mkuu wa majeshi kaongea lolte kuhusiana na matatizo ya usalama hapa TZ?

  RO yeye ni mkuu wa upelelezi, kama cheo chake kinavyojieleza, sio katika kila suala la usalama yeye awe mzungumzaji, mambo yeke ni ya chini kwa chini

  Nchi nyingi duniani kulinda usalama wa taifa, viongozi wa upelelezi hawabwatukibwatuki kwenye vyombo vya habari na wala sio vizuri kwa usalama wa nchi waandishi habari hasa wa TZ ambao wanaandika un-investigated reports kuanza kukurupuka na kulete hoja za kubuni
   
 7. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwani ni nini ambacho wamekataa kuandika ama kusema bungeni ambacho amefanya Othman?
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nafikiri Mzee Mwanakijiji anajaribu kuhoji kwamba RO anafanya nini kama mambo ya kiusalama yanazidi kwenda kombo na yeye yupo tena kimya. Sikubaliani na wewe Bull eti RO ni mkuu wa upelelezi, yeye ni mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa, so hii ni zaidi ya upelelezi.

  Kila mara tumemsikia panetta (director wa CIA) akitoa ufafanuzi wa mambo mengi tu juu ya security ya USA, je RO anadeal na issues nzito kuliko Panetta? Tuwe wakweli tu kwamba TISS imedorora tangu mkapa amuue Gen. Imrani Kombe ambaye alikuwa angalau anajua kazi yake.

  Watu wanaiba pesa BOT, TISS hawajui au wanajua lakini wanakaa kimya kwa sababu nao wanapewa mgao. Mfano issue ya mauaji ya albino hatukuhitaji kupiga kura za siri, idara ya usalama wa taifa ilitakiwa iwe inajua issue hizi kabla hata hazija ibuka. Mauaji ya albino yameanzia kongo DRC na soko kubwa la viungo vyao lipo huko lakini RO na timu yake wamekuja zinduka tayari mauaji yameanza na kuyakomesha inachukua muda.

  Sawa, wamejitahidi kupeleleza lakini lazima walaumiwe kwanini wanasubiri mpaka jambo litokee? Angalia yule mtoto aliyerusha chupa za mafuta ya taa ili alipue gari za ubalozi wa marekani majuzi. Inasemekana kuna shehe alitoa mahubiri ya kuhamasisha waislamu kuishambulia marekani, je RO na timu yake hawapo misikitini? au wanasubiri yale ya 1998 ndo wagutuke?

  Nasikitika kusema kipindi cha RO na timu yake ya TISS kutajirika ndo kimefika. Mwaka 2000 kwenye uchaguzi mkuu watu wa idara ya usalama walifikia hata kusema UDSM pale eti wanafunzi wa Engineering walipogoma eti wana mabomu ya petroli basi ilikuwa taabu kweli, magari ya FFU 6 yalipiga kambi pale kwa wiki nzima. kumbe ilikuwa ni njia yao ya kujipatia allowance na mambo mengine.
   
 9. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,525
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mimi mgeni jamani ndo nimeshuka kwenye basi sasa hivi!!!!!
   
 10. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #10
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja ya Mzee Mwanakijiji inachanganya mambo mengi lakini inaonekana wazi kwamba haifahamu TISS na majukumu yake chini ya uongozi wa RASHID OTHMAN kama Mkurugenzi Mkuu. Sina uhakika kama Mzee Mwanakijiji ana maana gani anapomfananisha RASHID OTHMAN na mpelelezi ambaye ameshindwa kuwakamata wezi wa BOT, wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi – albino, kumkamata mtoto aliyerusha chupa ya mafuta ya taa ili kulipua magari kwenye Ubalozi wa Marekani na kuwazuia wanafunzi wa Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wasifanye maandamano mwaka 2000.

  Mzee Mwanakijiji anasema RASHID OTHMAN na vijana wake wa TISS wanaacha kutimiza majukumu yao kwa sababu wanapata mgao unaotokana na uhalifu. Nafikiri Mzee Mwanakijiji anatafuta habari kwa njia za uchokozi na hajafanya utafiti wa kile anachotaka kukisema. Ana bahati mbaya sana kwa sababu hajakadiria uharibifu anaofanya kwa kuelezea TISS na Mkurugenzi wake Mkuu kwamba imedorora.

  Pamoja na kwamba Mzee Mwanakijiji hajataja tukio lolote ovu ambalo linahatarisha Usalama wa Taifa ni vizuri afahamu kwamba Idara ya Usalama inayoongozwa na RASHID OTHMAN, kwa sisi tunaoishi mitaani, TISS kama ‘Central Intelligence Agency’ ya Marekani inayoongozwa na LEONS’ PANNETA zina kazi ya kutoa ushauri juu ya makadirio ya hali ya kiusalama na sio kutoa sera, kufanya kazi za kipolisi au Jeshi la Wananchi. Sisi tulio mitaani tunakuwa na wasi wasi kama kweli Mzee Mwanakijiji anafahamu majukumu ya kazi za vyombo vya Usalama akianzia na TISS na hutumia mtandao huu kutoa somo kwa wananchi. Inabidi afanye utafiti wa kutosha na hata awaulize Wabunge kama wanaionaje TISS chini ya RASHID OTHMAN.

  Mzee Mwanakijiji anatakiwa afahamu kwamba TISS, kama ina upungufu, upungufu huo unaweza kuonekana pia kwenye vyombo vingine vya Kimataifa vinavyofanana nacho kama CIA ya Marekani, KGB ya Shirikisho la Urusi au hata MOSSAD ya Israel. CIA ni chombo kikubwa cha Marekani kinachofanya kazi kama TISS, lakini chombo hicho kina mafanikio na mapungufu yake. Chombo hicho kikubwa kimekuwa na kile kinachoitwa ‘Intelligence Failure’ kuanzia vita vya Korea, miaka ya 50, Vietnam miaka ya 70, Iraq miaka ya 90 hadi sasa, na Cuba – Bay of Pigs na Afghanistan. Mzee Mwanakijiji anaombwa asome juu ya hilo kabla ya kuishambulia TISS ambayo sisi tulio mitaani tunasikia ikisifiwa kwa weledi, ujasiri na umakini wa watendaji wake chini ya RASHID OTHMAN.
   
 11. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  RO hana tatizo kwa sababu amefanya kazi kwenye idara hiyo kwa miaka nenda rudi na yeye na walio wakomavu kama yeye kwenye idara hiyo wanao uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi. Matatizo mengi yanayojitokeza mara nyingi hayahusiani na utendaji kazi wa idara kama hiyo, bali yanahusiana na viongozi hususan kiongozi mkuu wa nchi. Kama kiongozi wa nchi anataka wakati wote vyombo hivi viipake nchi rangi ya hudhurungi nchi ionekane inapendeza, hawawezi kufanya vinginevyo inabidi watii amri ya aliyewateua.
   
 12. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Fikra Mbadala, naomba usikurupuke na kuandika MM mwanakijiji haijua vyema hiyo TISS.
  Nikipiga hesabu ya tka ulipojisajiri hadi leo napata wasiwasi wa ukomavu wako katika JF na uelewa wako. sawa waweza ukwa na uelewa mzuri tu, lakini naweza fkiri kuwa wewe huwa unaingi katika forum zile ambazo huitaji kuumiza kichwa katika kufikiri au unasoma threads za namna hiyo. Kama hilo si sahihi basi UNALAKO JAMBO (rudia na kurududia mifano uliyoitoa na halafu ukweli katika uhalisia wa TISS)
  2 years in JF 11 posts, umedumaa? Mvivu wa kusoma? unatumiwa? ..... nakupa kazi kasome post za Mwanakijiji. halafu siku nyingine Usikurupuke hivyo, eeenh!
  Kama umetumwa waambie "Baba hataki".. hawatakutuma tena enhee!
   
 13. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Licha ya maelezo yako marefu, hujafafanua huo weledi kiasi cha kusifiwa umeisaidia vipi nchi! Tunachoweza kuona ni kuwa TISS imekuwa kama kigenge cha kulinda uhalifu, na wenye nguvu ndio wanaitumia kutekeleza watakayo kwa kutumia hicho kitengo chenu mliopo mitaani kama unavyojiita. Mnafanya mambo gani ya siri, na siri hiyo ni kwa ajili ya nani, na kwa faida ya nani? Ninadhani inafika wakati idara hiyo iangalie basis za kuundwa kwake, kama ilikuwa ni kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya wezi wakiwa madarakani au kuiepusha nchi na mabalaa kama yaliyotukumba.

  Usianze kutetea failures kwa kufananisha na failures za CIA, walau CIA inaweza kutokea hadharani na kusema wamefanya kadha wa kadha, sijui kama kuna lolote linaweza kuelezwa na ninyi mliopo mitaani. Watanzania tumeingiwa na roho ya ubinafsi, kutojali utu wa wengine na haki ya wengine, na mwisho kila mmoja anaona bora ashirikiane hata na shetani ili mradi ajilimbikizie mali. Ninyi mliopo mitaani itabidi mjichunguze upya, na mjaribu kuona kama kweli mnastahili kuendelea kuwekwa mtaani. I am totally pissed off by this thing called TISS, kazi kukaa kuwachunguza wenye mapenzi mema na nchi hii kwa maslahi ya wezi. Mko wapi wakati nchi hii ikiuzwa na watu kufanya wanavyotaka? nyie endeleeni kukaa huko mitaani na kusifiana kwa kuwakomoa wanahalisi wa Tanzania, ipo siku tutaitetea nchi yetu na kuitoa kwenye udhalimu huu. Mungu ibariki Tanzania
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  hivi umesoma nilichoandika hapo juu au unafikiria nimeandika usichosoma?
   
 15. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tatizo la watanzania wanapenda kujilinganisha na vitu vidogo vidogo ambavyo havina tija na wanasahau kujilinganisha na mafanikio ya nchi nyingine. In a million year ujinga unaotokea bongo au kubaliki ktk nchi yeyote hapa duniani zaidi ya south afrika ambapo wamechagua rais mbakaji
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapa panahitaji maelezo zaidi mkuu wangu!
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  gari la Rais na pancha
  Magari ya msafara wa Rais na mafuta yaliyochanganywa
  Ndege ya Rais kugongwa na gari
   
 18. Devils Advocate

  Devils Advocate Member

  #18
  Jun 18, 2010
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mmh mkuu sijui wewe uko katika dunia ipi!! Lakini sina ujanja labda nikupe mifano michache.

  Please visit: https://www.cia.gov/news-information/press-releases-statements/index.html

  Uone wenzetu walivyo open na mambo wanayoongelea.
   
 19. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Mzee Mwanakijiji tutasema mengi sana, kwa nini huyu kafanya hivi ama hafanyi hivi, lakini ukweli wa wazi ni kuwa system yote ya uongozi wa nchi hii imeoza. Hakuna mwenye moral authority ya kumchukulia mwenzake hatua. Raisi hawezi kumwajibisha yeyote kwani wote wanajua udhaifu wake na alipofanya ufisadi. Usitegemee hata siku moja JK kumchukulia hatua RO wakati anajua kuwa RO anajua ufedhuli wake, hali kadhalika RO hawezi kumwajibisha mdogo wake yeyote haijalishi amefanya kosa gani. Hii ndiyo Tanzania yetu.

  Sasa Tanzania imeiva kwa mapinduzi, mimi nasema wakati wa maneno umepita na sanduku la kura kwa mwendo huu kamwe haliwezi kuleta mageuzi tunayoyalilia, mimi siwezi kupoteza muda wangu kwenda kusiamama foleni ya kupiga kura wakati najua matokeo ni wasanii kurudi tena madarakani. Mapinduzi kama yaliyofanyika Niger ndiyo ukombozi wa Tanzania, vinginevyo wananchi sasa waingie mitaani kutaka CCM itokomee. Tusidanganyane hakuna njia nyingine, tunahitaji organization ya kuwahamasisha wananchi tuchukue jukumu la kufanya mapinduzi ya kuung'oa utawala huu wa ccm. IMETOSHA.
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  Hata msafara wa Rais kurushiwa mawe Mbeya.
   
Loading...