Kumezuka malumbano makali miongoni mwa wanahabari wa mkoa wa Mbeya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroard Slaa kufuatia waandishi wa habari wa magazeti ya NIPASHE na TANZANIA DAIMA kudaiwa kuweka kibindoni mshiko wa Sh.300,000 uliotolewa na viongozi wa chama hicho ili wagawane wanahabari wote walioshiriki ziara hiyo. Taarifa kutoka katika ziara hiyo zinadai kuwa Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Angelica ndiye aliyekabidhiwa Sh.300,000 akiwa na Mwandishi wa Nipashe Emmanuel Lengwa ili wakawagawie wenzao. Hata hivyo katika hali ya kushangazai waandishi hao wawili wakaamua kugawana wenyewe mshiko huo kitendo ambacho kimeudhi waandishi wengine.