Waandishi makanjanja na hatma ya Tanzania

Huyu mwandishi inaelekea hata hamjui Robert Maxwell. Kuanguka kwa huyu fisadi wala haikuwa kwasababu ya kuchanganya biashara na siasa.

Ina fact kwa UK ni kawaida kwa wafanyabiashara wanaohusika na vyombo vya habari kuchanganya siasa na biashara.

Ukiangalia UK na USA, Rupert Murdoch na vyombo vyake (SKY NEWS, FOX NEWS, SUN etc) wanafikia hata kuamua nani awe rais au PM. Hivyo hivyo Italy kwa Berlusconi na vyombo vyake anaendelea na biashara pamoja na siasa.

Kuanguka kwa Maxwell ilikuwa sio kwasababu ya kujihusisha na siasa, ilikuwa kwasababu ya ufisadi. Muda wote alikuwa anatumia njia za mkato kujitajirisha kwa cost ya wafanyakazi wake na wanyonge wengine.

Mwandishi hajafanya homework ya kutosha labda kwasababu yuko biased na lengo lake lilikuwa kumshambulia mengi. Ukiandika makala ukiwa na chuki na mtu sio rahisi kuja na arguments ambazo ni balanced.

Nakuunga mguu kwa asilimia 700. Naamini mwandishi ana chuki fulani dhidi ya Mengi. Penye ukweli daima uongo hujitenga. Na gazeti hilo ni moja ya magazeti ambayo yalianzishwa yakiwa na ajenda rasmi nazo ni kupinga ukweli, kusafisha mafisadi kwa kutumia kalamu za waandishi na migongo ya wananchi.
Lakini nawapa pole maana WATANZANIA wameelimika na busara zaidi kutambua pumba na mchele.
 
...mwandishi anajifanya anamtakia mema Mengi kwa kumpa ushauri kumbe majungu tuu na kuanguka kwa Mengi ndio wanachotaka,hizi media propaganda zipo tangu adam kwa hiyo sioni cha ajabu hapa,i respect mengi kwa anayoyafanya katika society kwa kuajiri watu wengi na kulipa kodi...kuna uzalendo zaidi ya huo?

Mkuu
Ni maoono yangu tu.
Nafikiri hata huko BUZWAG walioajiliwa wengi ni watanzania na bado nafikiri huko kunamishahara minono kuliko ya kwa mengi.

Nahata huko kwa akina Yona na Mkapa sijui songas au wepi bado nafikiri nako kuna mishahara na wengi waajiliwa ni watanzania je?hicho ni kipimo cha uzalendo? ama ni biashara ndiyo inawalazimu kuajili watu na mengi akiwemo lasivyo wasingeajili?
 
Nakupata Mkuu wangu.
Ndio maana nikasema unapoliangalia jambo usijikite zaidi kwa kuangalia huko nyuma Mengi alifanya nini ama Manji alifanya nini ama MkamaP alisema nini ktk hoja ile kwa hivyo ktk hoja hii nimeshaelewa anataka kusema nini hivyo sihitaji kusoma maandishi yake tena.

Ndiyo invisible nikamukumbusha ya kwamba kwa mtu aliyekuwa amekwishamsikiliza SAULI hakuwa na haja tena baade kumsikiliza PAULO maana alikuwa ameshamwelewa yule madili yake ni kuuwa tu.
Ndivyo tulivyo wanadamu unaweza anza vizuri ukamaliza vibaya ama kuanza vibaya ukamaliza vizuri.

MkamaP, unataka kutuaminisha kuwa Shubash Patel na Manji kwa sasa wameongoka na kubadilika kutoka u-SAULI hadi kuwa kama PAULO? kama ni hao kweli ndio wamiliki wa hicho kigazeti, hakuna haja ya ku umauma maneno, Hoja nzima ni upuuzi mtupu.
 
MkamaP, unataka kutuaminisha kuwa Shubash Patel na Manji kwa sasa wameongoka na kubadilika kutoka u-SAULI hadi kuwa kama PAULO? kama ni hao kweli ndio wamiliki wa hicho kigazeti, hakuna haja ya ku umauma maneno, Hoja nzima ni upuuzi mtupu.

hapana sitaki kukuaminisha nachotaka kusema hapa nikuwa usijaji mtu kwa matendo yake ya zamani ama kupuuzia maneno yake ya sasa kwa kutumia maneno ya zamani.

Ndio nikauliza je? ktk ule mchakato wa uchaguzi wa 2005 Mengi aliuunga mkono lile kundi la mtandao hadi kupelekea kundi hilo kukamata hatamu? Na je kama ndiyo alifanya hivyo tuyapuuzie mambo yake ya sasa yakupingana na mtandao maana wakati ule aliuunga mkono mtandao?
Nafikiri tunaenda pamoja.
 
Inasemekana magazeti hayo ni ya Karamagi.Hakika mafisadi wamejipanga.Wana JF inabidi tuchukue hatua za makusudi kuwadhibiti watu hawa.Kwenye uongo,ukweli usimama.Mzee Mengi anaamua kuisaidia jamii,mhandishi anadai kuwa mafisadi wamekwisha-hajasikia habari ya NDC?
 
Inasemekana magazeti hayo ni ya Karamagi.Hakika mafisadi wamejipanga.Wana JF inabidi tuchukue hatua za makusudi kuwadhibiti watu hawa.Kwenye uongo,ukweli usimama.Mzee Mengi anaamua kuisaidia jamii,mhandishi anadai kuwa mafisadi wamekwisha-hajasikia habari ya NDC?

Ndiyo mkubwa UFISADI lazima umalizwe kwa hali na mali.Sasa Ukiisha changamoto kwako ni nini tufanye basi ili tuondokane na huu umasikini wetu?
 
Mkuu
Ni maoono yangu tu.
Nafikiri hata huko BUZWAG walioajiliwa wengi ni watanzania na bado nafikiri huko kunamishahara minono kuliko ya kwa mengi.

Nahata huko kwa akina Yona na Mkapa sijui songas au wepi bado nafikiri nako kuna mishahara na wengi waajiliwa ni watanzania je?hicho ni kipimo cha uzalendo? ama ni biashara ndiyo inawalazimu kuajili watu na mengi akiwemo lasivyo wasingeajili?

Wewe Mkama "Pumba" sijui unakichwa gani cha ovyo namna hiyo! Sisi tunazungumzia ufisadi uliofanyika kuwapa bure wageni maliasili zetu wewe unazungumzia vijimishara walipwao walalahoi wanaofanya mikazi ya kufa mtu huko Buzwagi na kwingineko! Natamani ningekluwa na uwezo ningekufuta urai wa tz. Ulaaniwe kwa kuunga mkono ufisadi.
 
Mwandishi Wetu ( Gazeti la Sauti Huru) Disemba 30,2008

Mr Mwandishin wetu!

The total context of your presentation shows very clear where you are coming from and of course where you are heading.

Let me tell you all this..!

You are deadly wrong on the methodology and the pathway.

You will never ever get to where you are heading.

Mkuu hutafikia ...Goal!

If they pay you ...be honesty... rudisha !!!

You should be able to read the moment in which you r operating...!

Mkuu do you think it will work?
 
Azimio fikiria jinsi habari hiyo mtu akiichukuwa akaiweka katika mailing list yake akaisambaza itafikia wangapi huko maofisini na kama unavyojua huko maofisini watu hawana muda wa kuchambua mambo wengi wanapokea kile ambacho wametumiwa kwenye email zao kwahiyo mwandishi anakuwa amepiga bao tena kubwa sana nina uhakika hilo gazeti halina tovuti kwahiyo hiyo habari imepatikanaje humu ? Ina maanisha kwamba kuna kitu kinaendelea sasa sasa vina imehamia upande huu
 
Hiki ni kigazeti gani tena? Msaada tu ili tusijeshindwa kukitendea haki.

Naona kama vile unakisagia "kigazeti" hicho; kwa nini usilize kuwa ni "Gazeti gani" badala ya "kigazeti gani"
 
Wewe Mkama "Pumba" sijui unakichwa gani cha ovyo namna hiyo! Sisi tunazungumzia ufisadi uliofanyika kuwapa bure wageni maliasili zetu wewe unazungumzia vijimishara walipwao walalahoi wanaofanya mikazi ya kufa mtu huko Buzwagi na kwingineko! Natamani ningekluwa na uwezo ningekufuta urai wa tz. Ulaaniwe kwa kuunga mkono ufisadi.


teh teh teh teh teh.

ndiyo maana nyani anakwambia ndivyo tulivyo teh teh teh,yani hutaki kuielewa hoja yangu kwa kuwa.........,Mkubwa hapo hoja yangu ilikuwa mtu kuwapa kazi watanzania na kulipa kodi huo sio uzalendo ni utaratibu tu kama taratibu zingine zilizopo hapa duniani .

Rafiki yangu mimi sitetei mafisadi ila naponda mafisadi wote na haswa wale nyoka wanaojuwa kuwa manipulate hisia za watanzania.

Nimekuulizeni swali Je Mengi ktk uchaguzi 2005 aliuunga mkono mtandao ama aliupinga?
Na je nini alifanya baada ya kugunduwa ITV wamefoji sahihi ya Mtikila?

Mkuu ukiamua kutafuta haki ya kweli itafute kwelikweli osihofu kuhoji kitu chochote unachokiamini ndivyo sivyo.
 
Mwanakijiji heshima mbele, nadhani kumfananisha Robert Maxwell na Reginald Mengi kunaweza kuwa sio sahihi kwani ingawa kweli Mengi ni newspaper magnate kama alivyokuwa Maxwell lakini Maxwell hakuwa anatetea wanyonge na kupiga vita ufisadi kama anavyofanya Mengi. Mpaka sasa Mengi hajaonesha kuwa anataka kuingia kwenye active politics isipokuwa hao mafisadi anaowaumbua ndio wanawatumia vikaragosi wao kuspin hata kumfananisha na marehemu Maxwell. Mbona hamuandiki kumfananisha na successful newspaper magnates kama Rupert Maddox au hata belucsson wa Italia? Haya yote ni majungu na spin za mafisadi na Mungu yupo wote mtaangamia!!

Mkuu Bulesi nakubaliana na hoja hii.Mengi vijiweni anajulikana kama mzee wa misifa.Hiyo ndiyo weakness yake.
Hata hivyo on the positive side Mzeee Mengi vilevile ni mtetezi wa wanyaonge wasio na sauti.Hebu fikiria ni viongozi wangapi consistently na kila mwaka wana kula na viwete,maalbino na wasio jiweza?Pamoja na kuwa na mamlaka na uwezo?
Jiweke wewe katika position ya kula mlo na Bush au JK, uatajiskiaje kama ni maskini na Tanzania.
Tukipata ingalau jibu dogo hapo tutaweza kuona self drive aliyonayo Mengi.
Hata hivyo kosa kubwa la Mengi ni kuwaandama mafisadi kwa vyombo vyake vya habari.
Wananchi tunafaidika na hilo ingawaje nafikiri hii ni kujitolea tu kwa Mengi na vyombo vyake.Sipati jibu nikijiuliza je habari za ufisadi hazifiki kwenye vyombo vingine vya habari kama TVT,Daily News, Uhuru?Mbona havina investigative news za kuumbua ufisadi?
 
Kimtazamo wangu nafikiri wote ni mafisadi, tukihoji alivyoanzisha IPP huwezi amini ni ufisadi tu. Hivi uliza wafanyakazi wanaonfanya IPP wanalalama kuhusu Mengi anatoa mshahara ya kumfanya mtu utetee ufisadi maana huna jinsi, watanzania tunapenda kazi za kuajiriwa na si kujiajiri.

Anaonekana kutoa misaada mingi sana kwa vilema kitu ambacho ni kizuri sana, lakini basi uwe na huruma kwa wale wanaokufanya wewe uonekane ukizingatia kampuni mpaka ikamilie lazima iwe na watu. Hata hiyo inayosemekana ni kupigania haki kwa Mengi ni ufisadi tuna sifa kwa wingi. MENGI ANAPENDA ATUKUZWE KITU AMBACHO NAFIKIRI HATUKO TAYARI. AKAE NA UTAJIRI WAKE SIYO KUTUMIA VIVURI VYAKE ETI ANATETEA MASLAHI KUMBE NI BINAFSI.
 
Kimtazamo wangu nafikiri wote ni mafisadi, tukihoji alivyoanzisha IPP huwezi amini ni ufisadi tu. Hivi uliza wafanyakazi wanaonfanya IPP wanalalama kuhusu Mengi anatoa mshahara ya kumfanya mtu utetee ufisadi maana huna jinsi, watanzania tunapenda kazi za kuajiriwa na si kujiajiri.

Anaonekana kutoa misaada mingi sana kwa vilema kitu ambacho ni kizuri sana, lakini basi uwe na huruma kwa wale wanaokufanya wewe uonekane ukizingatia kampuni mpaka ikamilie lazima iwe na watu. Hata hiyo inayosemekana ni kupigania haki kwa Mengi ni ufisadi tuna sifa kwa wingi. MENGI ANAPENDA ATUKUZWE KITU AMBACHO NAFIKIRI HATUKO TAYARI. AKAE NA UTAJIRI WAKE SIYO KUTUMIA VIVURI VYAKE ETI ANATETEA MASLAHI KUMBE NI BINAFSI.

Ni kweli Caroline lakini kumbuka Mengi ni bepari ,hilo tusisahau.Bepari kimsingi hutumikisha wengine kwa faida yake.
Mfanyakazi ana uhuru wa kupetition au kuacha kazi , hizo ndio njia alizo nazo.
Weakness kubwa ya Mengi ni kupenda sifa ndio maana vijiweni anaitwe mzee wa misifa.Hakuna taarifa ya habari ambayo haina habari zake.Ndio maana mtoa hoja kamfananisha na Robert Maxwell katika siku zake.
Kupenda sifa nako lakini kuna gharama zake .
Sifa na siasa zinaenda pamoja, katika sehemu ambazo Mengi amewagusa wanasiasa wamejaribu kumweka katika nafasi yake.
Hata hivyo mchango wake katika vita ya ufisadi bado iko palepale, ni ule msuli wake wa pesa na vyombo vya habari umemfikisha hapo alipo.
 
Mwandishi Wetu ( Gazeti la Sauti Huru) Disemba 30,2008

YUKO wapi bilionea Robert Maxwell? Nani anasikia tena tambo, nyodo na majigambo yake? Amefutika. Amebaki historia.

Maxwell alikuwa ni bilionea mwenye kumiliki magazeti makubwa kama Daily Mirror na Daily News na pia alikuwa mchapishaji wa vitabu. Alivuma mno kwenye miaka ya themanini kutokana na utajiri wake.

Kamwe hakuna aliyefikiria kama itafika siku Maxwell atafilisika na kuwa kapuku hadi kushindwa kumudu kulipa madeni yaliyomkabili.

Hii ni hulka ya watu wengi wakiwemo matajiri na hata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu. Wanapofika kwenye mafanikio, wanajisahau na hawafikirii kama kuna kuanguka. Wanadhani wataendelea kula raha milele.

Kiichomponza Maxwell ni uamuzi wake wa kuchanganya biashara na siasa na haswa siasa za malumbano. Alitumia vyombo vyake vya habari kuhubiri kile alichotaka na kufanya alichojisikia.

Alifanya hivi kwa kuwa hakukuwa na wa kumzuia, alimshambulia kila aliyemtaka huku akijiweka kwenye tabaka la juu zaidi na kujiona kama ni mungu mtu hadi kufikia hatua ya kulazimisha kila asemalo liwe.

Maxwell akageuka mwiba. Malumbano yakapamba moto akayaingiza magazeti yake kwenye mapambano – yakandika kile chenye maslahi kwake na kusahau matatizo ya wananchi.

Hapo wasomaji wakaanza kugawanyika kutokana na mabadiliko ya mfumo wa magazeti yake. Yalijaa habari za majisifu yake na mapambano, wakaamua kuacha kuyanunua.

Kuanzia hapo akaanza kuyumba kibiashara, mauzo yakashuka, madeni yakamzonga na mwishowe alifilisika.

Maxwell akakosa pa kushika, hakupata tiba ya matatizo yake akawa ni kama mtu aliyechanganyikiwa na hatimaye 5, Novemba, mwaka 1991 akakutwa amefariki ndani ya boti ya kifahari iliyoegeshwa kwenye ukanda wa Tenerife , kisiwa cha Canary nchini Hispania na alizikwa kwenye mlima Olives, Jerusalem .

Kila mmoja alizungumza lake juu ya kifo chake, wengine walisema ameuawa na wapo walioamini amejiua kutokana na msongo wa mawazo yaliyosababishwa na kuanguka kibiashara.

Badaa ya kifo chake, mabenki yakaanza kuuza mali alizokuwa anamiliki yakiwemo makampuni ili kufidia madeni, mwanae hakuwa na la ziada naye alilazimika kuuza hisa zake na mali kuwa mikononi mwa watu wengine.

Huo ndio ukawa mwisho wa zama za bilionea Robert Maxwell aliyeishia kupata ubunge badaa ya purukushani zake za kisiasa na kutumia fedha nyingi kudhamini Chama cha siasa.

Hakika huu ni mfano tosha unaofaa kumpa somo Reginald Mengi, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP. Kwani naye anaonekana kushindwa kujigawa na kubaki mguu mmoja kwenye siasa mwingime kwenye biashara.

Mengi amejitosa kwenye siasa za malumbano. Kama ambazo alianza nazo Maxwell, hajui ashike wapi, bado anatamani kuendelea na biashara na huku wakati huohuo anatamani na amegeuka mshika mbili.

Ukimsikiliza kwa makini kauli zake utagundua anaweweseka na kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe. Ni dhahiri anahitaji msaada. Si msaada wa kifedha bali ni wa maombi na ushauri.

Wanatakiwa watu wenye busara wamuweke chini na kumshauri kuacha moja na kuendelea kuweka nguvu kwenye jambo moja vinginevyo atakosa moja ama yote.

Kwanini tusianza kuhisi kwamba hata yowe analopiga hivisasa la kuhujumiwa ndio ishara ya kuporomoka kwake?

Kwamba mambo yameanza kumuendea kombo na sasa anaamua kusaka mchawi. Anatafuta wa kumshushia lawama pale atakapoishia ukingoni na kubaki kwenye ukapuku.

Hakuna haja tena ya kurudia orodha ya malumbano aliyowahi kuingia na watu wa kada mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na viongozi wa serikali huku kila kukicha akilia kuonewa ila anaonekana kutamani kuwa mwanasiasa.

Kama ilivyokuwa kwa Maxwell, Mengi naye anatumia kwa kasi vyombo vyake kuhubiri kile anachotaka kiwe. Akitumia kigezo cha kupambana na ufisadi kupenyeza hoja zake anazozitaka kwa lengo la kuwashambulia anaowalenga.

Mengi leo amegeuka mwanasiasa na si mfanyabiashara tena kama tulivyomzoea kwa miaka mingi. Anarukia kila hoja ambazo nyingine hazimuhusu.

Pia anatumia vibaya kofia ya kuongoza vyombo vya habari kama mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari mchini (MOAT) kuamua anachotaka.

Mamlaka hiyo anaitumia kuviongoza na kuvipeleka anapopataka vyombo vya habari hata ambavyo havimiliki na kuvitumia kama kipaza sauti cha kusema lolote analojisikia.

Hii ni hatari kwa usalama wa nchi. Mtu mmoja akiachwa awe na nguvu kiasi hiki na hata kuwa na ujasiri wa hali ya juu wa kuwashambulia viongozi wa juu serikalini.

Tujenge mashaka sasa, Mengi anafanya harakati hizi kwa maslahi ya nani? Je, ni kweli ana uzalendo kiasi hiki ama ana lake jambo ?

Kama ni kweli angekuwa mzalendo na muungwana kama anavyotaka aonekane, angetumia njia stahili, kufikisha kile anachotaka kuliko kutumia njia hii ya mapambano na malumbano alizozoea kutumia.

Kwanini tusiamini kile kinachozungumzwa kwamba anataka kuwania Urais? Ingawa miezi kadhaa iliyopita, alishuka waraka mrefu na kutumia fedha nyingi kulipia kurasa za magazeti kukanusha habari hizi.

Bado hajatushawishi tuamini kwamba hana mpango na ikulu au kama si yeye basi amemua kuweka nguvu kusaidia mtu au kundi fulani liweze kuingia ikulu.

Kama anaitamani ikulu basi atumie utaratibu unaoeleweka kuliko kuingia na mtindo huu wa kuchafua na kulumbana na watu, labda atuambie kama bado anafanya mazoezi kwanza.

Na kama anajiamini ajitose tuone umwamba wake, alumbane na wanasiasa wa kweli tuone kama anaweza kuweka hoja nzito na si kulalamika kila kukicha.

Mengi awe huru na si kuendeleza siasa za kujificha na kupiga kelele mitaani – siasa za porini huku akishusha malalamiko yasiyokwisha miaka nenda rudi.

Watu wamechoka malalamiko na tuhuma zisizoeleweka, wanataka kusikia mambo ya msingi yatakayowasaidia wengi zaidi kuliko kile kinachomuhusu mtu binafsi anayetaka ufalme huku akipigia debe maslahi yake.

Mengi anapaswa kuchagua moja, biashara ama siasa ingawa inabidi akichagua siasa afikirie mara mbili; siasa haziwezi kwa kuwa ana jazba.

Akumbuke kwamba ili abaki na nafasi yake aliyonayo asijihusishe na masuala ya siasa kwani mwisho wake ni mbaya na duniani kote hakuna mchanganyiko huu ambao labda sasa tumuite ni ‘mfanyabiasiasa.’

Salute Mwanakijiji kwa kuthubutu kusema kile ambacho wengi wamejiumauma kusema au walisema wakapingwa lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, Mzee Mengi lipo hata dogo analoweza fanyia kazi kutoka katika andiko lako hili hata kama afanani sana na Maxwell lakini yako wanayofanana na kama asipochukua hatua ya kubadilika watafanana kabisa na Maxwell.
 
Back
Top Bottom