Waandishi kujitosa kwenye siasa - ujanja au ujinga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi kujitosa kwenye siasa - ujanja au ujinga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kiwalanikwagude, Jul 3, 2011.

 1. k

  kiwalanikwagude Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natupa memory zangu nyuma i think ni 2008 kuna mwandishi mmoja anakwenda kwa jina la Rosemary Mwakitangwe aliwahi kuandika makala kwenye the number one newspaper in Tanzania almaarufu kama Raia Mwema akihoji mantiki ya wanahabari kujitosa kwenye siasa.

  Sasa hapa jamvini kuna waandishi wengi Mwanakijiji na wenzake naomba mtweleze hivi baadhi yenu kama Nkamia mnapojitosa kwenye siasa mna maana gani? mnaenda kuharakisha ukombozi au kujiongezea kipato?

  Sasa wote mkikimbilia huko nani atawesemea wanyonge? kwa maana mimi naamini vyombo vya habari ni mhimili wa kwanza wa jamii yoyote tofauti na upuuzi wa baadhi ya wanasiasa kuwa ni mhimili wa nne!

  NAOMBA JIBU WANA JF
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi Mwanakijiji ni mbunge? au Diwani? just asking!
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  watu wako busy na Dk Slaa ...subiria kesho utajibiwa!!
   
 4. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  mbona umewaona waandishi peke yao wakati bungeni kuna walimu,madaktari,wanaimba hip hop,taarabu,wahandisi,wachumi nk.
  siasa ni kwa kila mtu mkuu na si kwamba ukiwa mwandishi inakuondolea sifa.
  tafakari.
   
 5. Researcher

  Researcher Senior Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii si kwa wanahabari peke yao, dhana nzima ya uongozi imepotea kabisa katika nchi yetu.

  Nionavyo mimi: Kundi fulani la wanajamii linapendezwa na uzalendo, utashi, haiba na uwezo wa ndugu X katika kusimamia maslahi yao kisha wanamshawishi, kumpendekeza na hatimaye kumchagua kuwa mwakilishi wao.

  Au basi walau: Ndugu Y anakerwa matatizo katika jamii inayomzunguka, anakuwa na upeo kisha wito wa kujitoa katika kuyatatua kisha anaomba ridhaa na ushirikiano wa wanajamii yake wamwezeshe kusimama mstari wa mbele katika utatuzi.

  Lakini walio wengi: Ndugu Z anagundua kwamba ili afikie malengo yake inabidi apate wadhifa fulani. Kisha anaanza harakati zake ikiwa ni pamoja na kushawishi, kuahidi, kujiweka karibu na kundi fulani na hata kuwekeza mali kwa dhamira ya kuupata huo wadhifa.

  Epuka sana akina Z.
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni bora Waandishi kuliko Wafanyabiashara
   
Loading...