Waandishi jaribuni kuwa sahihi.

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,674
1,685
Hivi karibuni wabunge wa bunge la jamhuri katika kikao chao waliwaomba mawaziri wanne pia waziri mkuu wajipime kwa manufaa ya umma hao ni waziri wa mifugo, waziri wa ulinzi, waziri wa mambo ya ndani na waziri wa mali asili na utalii. Wengi tulimsika mheshimiwa Kagasheki akitangaza bungeni kuachia wadhifa huo na mheshimiwa Mathayo akijiuma uma kuchukua hatua ya kujiuzuru (hakutaka) lakini waziri mkuu baadae akatueleza kuwa mheshimiwa Rais katengua nyadhifa zao wote wanne. Tunakumbuka si mheshimiwa Nchimbi wala mheshimiwa Nahodha waliotoa kauli ama ya kujiuzuru au ya kupinga kuwajibika. Sasa jana wakati nasikiliza taarifa ya habari ya ZBC walitueleza mheshimiwa Nahodha kajiuzuru ambapo sio sahihi, hata mheshimiwa Lowasa nae hakustaafu bali alijiuzuru wadhifa wa waziri mkuu hivo kumuita mstaafu sio sahihi. Sasa hii nimeikuta kwenye facebook:-
"BAADA YA KUFUKUZWA KAZI KWA UZEMBE RAIA MWENZETU WA KAWAIDA SHAMSI VUAI NAHODA AANZA POROJA NDANI YA UWANJA WA ALABAMA ZANZIBAR"

 
Kuna mambo mengi sana ktk uandishi wengine wanaandika ili gazeti lipate wateja,wengine hawajui matumizi ya maneno ya kiswahili,kustaafu,kustaafishwa, kujihudhuru na kutenguliwa kwa kitu au mtu ni maneno yenye maana tofauti kabisa,wawe wanasoma kamusi ya kiswahili kwanza kabla ya kuandika mada
 
Kuna mambo mengi sana ktk uandishi wengine wanaandika ili gazeti lipate wateja,wengine hawajui matumizi ya maneno ya kiswahili,kustaafu,kustaafishwa, kujihudhuru na kutenguliwa kwa kitu au mtu ni maneno yenye maana tofauti kabisa,wawe wanasoma kamusi ya kiswahili kwanza kabla ya kuandika mada
Kweli mkuu, cha kustaajabisha ni kuwa hawa wahariri kazi yao ni nini haswa, ikiwa pana mwandishi kakosea maana inatakiwa mhariri arekebishe kabla ya kuchapishwa gazetini au kutangazwa radioni na kwenye television. Au huwa pana maelekezo ya wanasiasa kwa hawa jamaa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom