Waandishi bora 25 wa Tanzania ni hawa wafuatao...

Nilitegemea kuyaona majina ya Nizar Visram na Joseph Mihangwa hapo.......Anyways,ni mtazamo wa mtoa mada huo
 
Kwa kiasi kidogo nakubaliana na utafiti wako. Ingawa sijali sana ulitumia njia gani, ningependa kujua kama waandishi hao walivyopangwa kwa namba kunamaanisha ubora wao. Yaani namaanisha kama yule wa namba moja amemshinda wa namba 25 kwa ubora. Na pia ningependa kujua kama uliowataja ni waandishi wa magazeti ya Kiswahili tu au ni pamoja na ya Kiingereza. Na pia nilitaka kujua kama umejumlisha waandishi wote wakiwemo wale wa vitabu. Ninavyojua waandishi wa habari ambao wameandika vitabu (majina yakiwa katika mabano) ni pamoja na Jenerali Ulimwengu (Rai ya Jenerali), Wilson Kaigarula (Mini Devils), William Shao (Miaka 2000 ya Ukristo: Historia Iliyopotoshwa), Ndimara Tegambagwe (Uhuru wa Habari Kitanzini na vitabu vingine kadhaa), Attilio Tagalile (Endless Toil) na wengine kadhaa. Uandishi wa watu hawa unanivutia sana. Kwa mfano niliposoma kitabu cha Shao kinachoitwa Miaka 2000 niliona mengi ambayo sikuwa nimeyafikiria awali, na uandishi wa Mini Devils ndio ulionifurahisha zaidi kuliko hadithi yenyewe. Kama mnafanya utafiti mwingine, mtenganishe pia na waandishi wa vitabu na aina ya vitabu wanavyoandika.
 
mh, mi nadhani mleta mada ana lengo lake kuna watu alitaka kuwafananisha na magwiji wa waandishi tunaowajua, jambo ambalo ni kuwadhalilisha! hakuna chochote hapa ni kutupotezea muda tu, labda ingekuwa na maana kama mtoa mada angekuwa mkweli kwamba hayo ni maoni/mtazamo wake, nisingemlaumu kwani uelewa wake kuhusu taaluma ya uandishi wa habari unaweza kuwa unaishia hapo... nijuavyo mimi kuna miongoni mwa hao, hata katika waandishi 100 tanzania hawamo, kama unabisha waulize media council/misa/au taasisi yoyote ya taaluma ya uandishi wa habari
 
Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............
1.Jenerali Ulimwengu( gazeti la Rai zamani na kwa sasa Raia Mwema pia ni mchangiaji kwenye The East African la kenya)
2.Mwanakijiji(Mwanahalisi, Tanzania Daima na mitandaoni)
3.Lula Wa Ndali Mwana Nzela(Raia Mwema)
4.Saed Kubenea(Mwanahalisi)
5.Ansbert Ngurumo(Tanzania Daima)
6.Evarist Chahali(Raia Mwema na www.chahali.com)
7.Ojuku Abraham(Dira kwa sasa)
8.Msomaji Raia(Raia Mwema)
9.Johnson Mbwambo(Raia Mwema)
10.Kondo Tutindaga(Mwanahalisi na Kwanza jamii)
11,Fr Privatus Karugendo(Raia Mwema)
12.Nova Kambota(zamani Dira kwasasa mtandaoni www.novakambota.com)
13.Dismass Lyassa(Mwananchi na mkurugenzi Global Source Watch GSW ubungo)
14.Kinabo(Tanzania Daima)
15.Samson Mwigamba(Tanzania Daima)
16.Fredrick Katulanda(Mwananchi)
17.William Shao(Majira na mwandishi wa "Miaka 2000 ya ukristo historia iliyopotoshwa)
18.Godfrey Dilunga(Raia Mwema)
19.Maggid Mjengwa(Raia Mwema na mtandaoni MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo)
20.Ndimara Tegambwage(Mwanahalisi na mtandaoni uhuru hauna kikomo )
21.Nkwazi Nkwabi(Dira na mtandaoni )
22.Marehemu Adam Lusekelo(Daily News with the light touch na mtandaoni)
23.Freddy Macha(Mwananchi, The Citizen na mtandaoni Freddy Macha)
24.Issa Michuzi(mtandaoni www.issamichuzi.blogspot.com)
25.Bubelwa Bandio(mtangazaji voice of America na mtandaoni "The Way You See The Problem Is The Problem")

HAWA NDIYO WAANDISHI 25 WA KITANZANIA WENYE USHAWISHI MKUBWA SANA KWA WANANCHI NA MWISHO WA UTAFITI WETU TULISHAURI TAASISI MBALIMBALI ZIWATUMIE WATU HAWA KWENYE KUHIMIZA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO MFANO KILIMO KWANZA, ELIMU NA KATIBA MPYA......NI HAYO TU WADAU , IWAPO UNA MAONI USISITE KUNIANDIKIA KWENDA kiwalanikwagude@rocketmaail.com

No research No right to write...Hukijui ulichoandika...Kama ni kwa mtazamo na upenzi wako binafsi sina shaka na hilo
 
Hao wote ni waandishi wanao ongelea masuala ya siasa. Si wa tanzania wote wanaopendelea siasa. Vipi kuhusu waandishi wa tasnia nyingine kama uchumi,sayansi,sanaa,michezo na burudani? Nako kuna waandishi mahiri. Review taarifa yako.
 
Naomba kufahamu iwapo kuna research yoyote imewahi kufanywa kutambua waandishi wakali hapa bongo? kina nani hao? wapi wapi? na ni wangapi? kwa maana pale kijiweni kwangu kila siku hii ndiyo topic

NAWASILISHA WADAU!
 
Nimemsoma William Shao katika kitabu chake kingine kinachoitwa HADAA: UNAFIKI MAREKANI NA UGAIDI DUNIANI. Kwa kweli kimeusuuza moyo wangu. Nilikuwa naami kabisa kuwa Osama ndiye aliyeipiga Marekani tarehe 11 septemba 2001. Lakini baada ya kusoma kitabu hicho nimeondokana na imani hiyo moja kwa moja. Kwa kweli naweza kukiri kuwa ni mwandishi mahiri. Sasa naona kwanini mwanajamii mmoja alisema Shao ni miongoni mwa waandishi 25 bora wa Tanzania.
 
Mnamsahau Hilal Sued mwandishi mahiri wa makala za kiingereza tangu enzi za family Mirror?
 
Hiyo ni mitizamo yao. kwangu ni tofauti kabisa.

This is poor type of research. Kwanza haina jina, author hasemi ilikuwa na lengo gani, ilifanyika kwa muda gani na wala hakuna methodology iliyotumika. Hizi ni hisia tu za mtu binafsi.
 
Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............
1.Jenerali Ulimwengu( gazeti la Rai zamani na kwa sasa Raia Mwema pia ni mchangiaji kwenye The East African la kenya)
2.Mwanakijiji(-----------, Tanzania Daima na mitandaoni)
3.Lula Wa Ndali Mwana Nzela(Raia Mwema)
4.Saed Kubenea(-----------)
5.Ansbert Ngurumo(Tanzania Daima)
6.Evarist Chahali(Raia Mwema na www.chahali.com)
7.Ojuku Abraham(Dira kwa sasa)
8.Msomaji Raia(Raia Mwema)
9.Johnson Mbwambo(Raia Mwema)
10.Kondo Tutindaga(----------- na Kwanza jamii)
11,Fr Privatus Karugendo(Raia Mwema)
12.Nova Kambota(zamani Dira kwasasa mtandaoni www.novakambota.com)
13.Dismass Lyassa(Mwananchi na mkurugenzi Global Source Watch GSW ubungo)
14.Kinabo(Tanzania Daima)
15.Samson Mwigamba(Tanzania Daima)
16.Fredrick Katulanda(Mwananchi)
17.William Shao(Majira na mwandishi wa "Miaka 2000 ya ukristo historia iliyopotoshwa)
18.Godfrey Dilunga(Raia Mwema)
19.Maggid Mjengwa(Raia Mwema na mtandaoni MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo)
20.Ndimara Tegambwage(----------- na mtandaoni uhuru hauna kikomo )
21.Nkwazi Nkwabi(Dira na mtandaoni )
22.Marehemu Adam Lusekelo(Daily News with the light touch na mtandaoni)
23.Freddy Macha(Mwananchi, The Citizen na mtandaoni Freddy Macha)
24.Issa Michuzi(mtandaoni www.issamichuzi.blogspot.com)
25.Bubelwa Bandio(mtangazaji voice of America na mtandaoni "The Way You See The Problem Is The Problem")

HAWA NDIYO WAANDISHI 25 WA KITANZANIA WENYE USHAWISHI MKUBWA SANA KWA WANANCHI NA MWISHO WA UTAFITI WETU TULISHAURI TAASISI MBALIMBALI ZIWATUMIE WATU HAWA KWENYE KUHIMIZA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO MFANO KILIMO KWANZA, ELIMU NA KATIBA MPYA......NI HAYO TU WADAU , IWAPO UNA MAONI USISITE KUNIANDIKIA KWENDA kiwalanikwagude@rocketmaail.com

Michuzi tupa kule weka Nizar Visram
 
Nyaronyo Kicheere, Eric Kabendera, Stan Katabaaro, Naijuka Kasihwaki, Zephania Ubwani, Sukhdev Chhatbar, to mention but a few. "Msomaji Raia" ni Kiongozi mmoja wa Kiroho ambaye uchambuzi wake uliwafikia wakulu wakamuonya "asichanganye" dini na siasa !! Ameacha
 
Muhidin Issa Michuzi kwa uchunguzi wangu wa kina amesoma TSJ 2004-2006 na alikuwa mwanafunzi bora wa somo la photojournalism awamu hiyo na mwanafunzi bora wa pili kiujumla katika darasa hilo aliloongoza Amabilis Batamula ambaye sasa ni Mhariri wa Majarida ya FEMINA. Issa Michuzi - Wikipedia, the free encyclopedia

No research no right to speak:msela:
 
Back
Top Bottom