Waandishi bora 25 wa Tanzania ni hawa wafuatao...

Jun 8, 2011
52
19
Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............
1.Jenerali Ulimwengu( gazeti la Rai zamani na kwa sasa Raia Mwema pia ni mchangiaji kwenye The East African la kenya)
2.Mwanakijiji(Mwanahalisi, Tanzania Daima na mitandaoni)
3.Lula Wa Ndali Mwana Nzela(Raia Mwema)
4.Saed Kubenea(Mwanahalisi)
5.Ansbert Ngurumo(Tanzania Daima)
6.Evarist Chahali(Raia Mwema na www.chahali.com)
7.Ojuku Abraham(Dira kwa sasa)
8.Msomaji Raia(Raia Mwema)
9.Johnson Mbwambo(Raia Mwema)
10.Kondo Tutindaga(Mwanahalisi na Kwanza jamii)
11,Fr Privatus Karugendo(Raia Mwema)
12.Nova Kambota(zamani Dira kwasasa mtandaoni www.novakambota.com)
13.Dismass Lyassa(Mwananchi na mkurugenzi Global Source Watch GSW ubungo)
14.Kinabo(Tanzania Daima)
15.Samson Mwigamba(Tanzania Daima)
16.Fredrick Katulanda(Mwananchi)
17.William Shao(Majira na mwandishi wa "Miaka 2000 ya ukristo historia iliyopotoshwa)
18.Godfrey Dilunga(Raia Mwema)
19.Maggid Mjengwa(Raia Mwema na mtandaoni MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo)
20.Ndimara Tegambwage(Mwanahalisi na mtandaoni uhuru hauna kikomo )
21.Nkwazi Nkwabi(Dira na mtandaoni )
22.Marehemu Adam Lusekelo(Daily News with the light touch na mtandaoni)
23.Freddy Macha(Mwananchi, The Citizen na mtandaoni Freddy Macha)
24.Issa Michuzi(mtandaoni www.issamichuzi.blogspot.com)
25.Bubelwa Bandio(mtangazaji voice of America na mtandaoni "The Way You See The Problem Is The Problem")

HAWA NDIYO WAANDISHI 25 WA KITANZANIA WENYE USHAWISHI MKUBWA SANA KWA WANANCHI NA MWISHO WA UTAFITI WETU TULISHAURI TAASISI MBALIMBALI ZIWATUMIE WATU HAWA KWENYE KUHIMIZA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO MFANO KILIMO KWANZA, ELIMU NA KATIBA MPYA......NI HAYO TU WADAU , IWAPO UNA MAONI USISITE KUNIANDIKIA KWENDA kiwalanikwagude@rocketmaail.com
 
Mkuu sidhani michuzi kama ni muandishi wa habari .. yaani wa kumuweka katika hilo kundi .." michuzi haandiki chochote" mimi nitamuweka katika kundi la wapiga picha BORA ..
 
Kwa michuzi HAPANA,ni bora hata Absalom Kibanda,Mhariri(Tanzania Daima)
 
Michuzi rafiki hapo nakupa big no!!!!!ni wa mrengo mmoja.
Thread ni nzuri Ila mwandishi katibua kitu kimoja kwa kumuingiza Michuzi. Huyu Issa Michuzi si mwandishi Wa habari kwani hajasoma taaluma bali ni kanjanja aliyeibuka miaka ya 80's kwa kupiga picha na kuzipeleka Daily News. Ndipo kwenye miaka ya 90's akapewa kazi kiushikaji. Naunga mkono kuingiza jina la Josta Mwangulumbi wa MwanaHalisi na Paskally Mayega Wa Tanzania Daima
 
Jee ni waandishi wa Kiswahili tu? Kuna wale wa Kiingereza ambao nao wamekuwa waandishi wazuri tukwa muda mrefu. Hawa ni Karl Lyimo, Azaveli Lwaitama, Fiki Krashani, Wilson Kaigarula, Hilal Sued, Anthony Ngaiza, Ayub Ryoba na marehemu Stanley Kamana.
 
Huu ni uchaguzi wa wadau mbali mbali na si wa mleta mada.

Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............
 
Mimi nanunua raia mwema kwa ajili ya johnson mbwambo
he is no 1 to me

halafu huyo msomaji raia mwema hana jina?sio jenerali???????????
 
Nimekuwa nafanya uchunguzi kwa mwaka wa 5 sasa juu ya waandishi wa kitanzania wenye ushawishi kwa wananchi, uchunguzi nimeufanya kwenye vyuo vikuu, mikoani, mijini, kwenye nyumba za ibada, vyama vya siasa na vijijini nikishirikiana na team ya watafiti wa maswala ya kisiasa wa chama cha Republican cha Marekani na wafuatao ni waandishi wanaokubalika sana miongoni mwa watanzania tena habari zao zinapendwa sana............

Upload ripoti kamili tuone vigezo gani umetumia, siyo kuchanganya tu mambo. Humo kuna wapiga picha, kuna waandika makala tu ambao kazi yao siyo waandishi (columnists), na je, hilo ni kundi gani la waandishi? siasa? uchumi? Utamaduni? mazingira? hebu fafanua, na kumbuka baadhi ya vyombo ulivyotaja ha amiaka mitano havina...hujawa makini.
 
Hawa waandishi bora ni WaTANZANIA Au WaTANGANYIKA. Nijuavyo mimi Tanzania haiwezi kuwepo bila ZANZIBAR. Naona mleta hoja kachemsha. Mbona ZANZIBAR kuna waandishi wazuri tu. Mfano Ali Saleh au Ali Bato na wengine wengi. Lakini list yote ni Tanganyika land. Heading ibadilishwe, iandikwe : WAANDISHI BORA 25 WA TANZANIA BARA.
 
Back
Top Bottom