Waandishi Arusha wagomea mkutano, kudai uhuru wa mwandishi wa ITV

UKAWA hii ishu mnataka kuidandia mchukuliepo ujiko. ha ha haaa.! UKAWA buanaa, roho mbaya zenu zitawaua. mtashangaa ishu itaisha na ITV wataendelea kuripoti habari za arumeru na huyo mkuu wa wilaya kama kawaida.

UKAWA tumieni nguvu nyingi kujipanga namna gani mtaingia madarakani, haya mengine mnapoteza muda tu bure.

hii ni ishu ya mwandishi wa ITV na mkuu wa wilaya, UKAWA fanyeni yenu. khaaa.! kila kitu mwadandia tuu utadhani hamna cha kufanya.
Hatimae amepatikana aliyemzidi MOTOCHINI kwa kuwa The Most Bogus person in the Forum. Hongera! What a Bogus comment?
 
Shida kunawanaotumiwa
Kwani waandishi wa UHURU media nao wamegoma?vipi wa Clouds? Jambo leo je? Hivi clouds wana mwandishi au ripota kutokea arusha? Maana kila wakitangaza habari za arusha huwa ni negatively!! Hasa habari za siasa,afadhali na uhuru Fm kuliko clouds!
 
WAANDISHI wa habari Mkoa wa Arusha leo wamegoma kuripoti ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kukamatwa kwa mwandishi wa kituo cha televisheni cha ITV, Halfan Lihundi.


Lihundi ambaye huripoti ITV kutokea Arusha, alikamatwa jana na polisi kupitia amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, kwa kile kilichoitwa kosa lakuandika habari za uchochezi.

Awali, kabla ya hatua hiyo ya waandishi kugoma walimwomba Waziri Lukuvi kuingilia kati suala hilo la kushikiliwa mwandishi huyo kwa kuwa habari anazotuhumiwa kuandika zinatokana na migogoro ya ardhi. Hata hivyo, Lukuvi aliwaeleza kuwa hawezi kuingilia suala hilo kwa kuwa liko nje ya mamlaka yake.

Kutokana na kauli hiyo, waandishi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Claud Gwandu, waliweka msimamo wa kususuia ziara ya Waziri Lukuvi.

"Mnapohitaji waandishi habari mnatuita lakini waandishi wa habari wanapokuwa na matatizo hamtaki kuwasikiliza na kuingilia kati kutatua matatizo hayo," 'alisema Gwandu.

Baada ya msimamo huo wa waandishi hao kupitia kwa mwenyekiti wao, Waziri Lukuvi aliondoka na msafara wake kuelekea Arumeru akiongozana na waandishi wa Shirikika la Habari la Utangazaji la Tanzania (TBC).
 
Safi sana huu uwe ni mwanzo tu wa kupambana dhidi ya manyanyaso mbali mbali dhidi ya wanahabari.
 
Hapana, ila watazamaji na. Wasikilizaji wa TBC walishatangaza mgomo usio na kikomo muda mrefu tu! Hivyo hata wakitangaza watakuwa wanajitangazia wenyewe na kusikiliza/kujitazama wenyewe!!
ookey...muwe mnawasiliana na kushauriana kabla ya kupost uzushi
 
Back
Top Bottom