dos santos
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 256
- 128
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari leo asubuhi kupitia kituo cha TBC,kuhusiana na mkutano wa waandishi wa habari na viongozi wa BAKWATA huko Igunga. Nilichoshuhudia ni sintofahamu baina ya waandishi wa habari na viongozi hao wa BAKWATA.Mvutano ulikuwa ni juu ya vazi la Hijabu.
Mshangao nilioupata ni pale baadhi ya waandishi walipokuwa wanang'ang'ania maelezo yao ndo sahihi kuliko yaliokuwa yanayotolewa na viongozi hao.Kiasi kwamba kukatokea malumbano baina yao kila upande ukishutumu mwingine anatumika kisiasa. Mshangao zaidi ni Mwandishi kabla hajaenda kuripoti hiyo habari ameshaonesha hisia na dhana ya kutoamini anachotakiwa kuripoti kwa wananchi,na badala yake anaanzisha mabishano. Wasiwasi je mwandishi huyu ataripoti alichonukuu au hisia na dhana zitajaa katika kuripoti habari hiyo?
Ukweli ni kuwa (hawapendi kuusikia) waandishi wengi wamekuwa wakitumika kisiasa,na wengine wakiripoti kishabiki katika habari mbalimbali.Jinsi walivyokuwa wakiuliza maswali kwa viongozi hao, kulikuwa na utashi zaidi wa kisiasa kuliko taaluma ya uandishi wa habari. Kama kuhoji ndo muongozo wa taaluma yao,angalia ripoti za tukio la Babu wa Loliondo.
Je waandishi walihoji kwa kina usahihi wa maelezo yaliyokuwa yanatolewa kuhusiana na dawa hiyo? Au wao ndo walikuwa ni vinara wa kuhamasisha wananchi kwamba dawa hiyo inaponya hata kabla ya ripoti za kitaalamu kutolewa. Waliongozwa zaidi na ushabiki kuliko usahihi wa jambo lenyewe. Hatimaye muda umetoa majibu sahihi,dawa hiyo inaponya au la.Bila shaka jibu unalo.
Tuwanasihi waandishi wasiripoti kishabiki au kutumiwa kisiasa ni hatari kwa jamii yetu.Na waandishi nao wakubali kukosolewa na pia wakubali walipokosea, kwani hakuna kundi linalojiona lipo sahihi zaidi, na lisilokosoleka kama wao. Wao si Malaika ni binaadamu wa kawaida wana udhaifu kama wengine. Kumbuka mwandishi ana haki ya kuwa shabiki wa chama chochote cha siasa ila anapokuwa katika taaluma yake anabanwa kuripoti kwa utashi wake.
Tuwapongeze kwa kazi nzuri wanayoifanya na tuwakosoe pale wanapokwenda kombo.Kwa kushirikiana tutafika