Waandishi 40 kati ya waandishi 50 waliouawa mwaka huu, wamekufa kwa kulengwa kwa makusudi na watu wenye silaha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Waandishi wa habari wapatao 50 wamepoteza maisha wakiwa kwenye kazi zao ndani ya kipindi cha mwaka 2020 kwa mujibu wa shirika la kutetea waandishi na vyombo vya habari duniani, Reporters Without Borders.

Kwenye mazungumzo mafupi kwa njia ya video na DW, mkuu wa Kamati ya Usalama wa Waandishi wa Habari ya Afghanistan, Najib Sharifi, amesema kwamba nchi hiyo haijawahi kuwa ya kuogofya kama ilivyo sasa, kwani kwa sasa kila mwandishi wa habari yuko hatarini.

Ndani ya kipindi cha wiki sita, Afghanistan imeshapoteza waandishi wanne wa habari, na wote ama waliuawa kwa risasi au kwa mabomu yaliyotegeshwa kwenye gari zao.

Hali ni hivyo hivyo kwenye maeneo mengine ya ulimwengu, kwa mujibu wa Shirika la Waandishi wa Habari Wasiokuwa na Mipaka, RSF, katika ripoti yake hiyo ya pili kutolewa.

Ingawa idadi ya waandishi wanaouawa wakiwa wanaripoti matukio ya mapigano imepunguwa, wale wanaouawa kwa kudhamiriwa imeongezeka maradufu.

Arubaini kati ya waandishi 50 waliouawa mwaka huu, wamekufa kwa kulengwa kwa makusudi na watu wenye silaha.

Mtangazaji wa kituo cha televisheni nchini Afghanistan, Malala Maiwand, aliuawa mapema mwezi huu wa Disemba, katika mashambulizi ambayo kundi lijiitalo "Dola la Kiislamu" lilidai kuhusika.

Lakini Sharifi anasema kwamba si rahisi kuwatambuwa wahusika na malengo yao. Zamani Taliban na kundi hilo la "Dola la Kiislamu" walikuwa wakibebeshwa tuhuma za mauaji kama hayo, lakini sasa tangu Taliban na serikali ya Afghanistan kuanza mazungumzo ya amani ni vigumu kumtambuwa muhusika.

Waandishi wa habari wanakabiliwa na vitisho na mashambulizi kutoka makundi ya wahalifu
 
Vipi waandishi wa Tanzania Kuna aliyeuawa 2020? Naona umeleta takwimu za Afghanistan tuu.
 
Back
Top Bottom