Waandishi 23 walikumbwa na mikasa mbalimbali wakitimiza majukumu yao kwa mwaka 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Jumla ya waandishi wa habari 23 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wamekumbwa na mikasa wakati wakitimiza majukumu yao katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba 2021, mwaka huu.

Ofisa programu wa Baraza la Habari Nchini (MCT) Paul Malimbo ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 2, 2021 kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga.

Malimbo alikuwa akisoma tamko la baraza hilo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kukomesha ukatili dhidi ya wanahabari

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu inaangazia jukumu la msingi la vyombo vya uendeshaji mashtaka katika kuchunguza matukio na kufungua mashtaka sio tu yanayohusu mauaji ya wanahabari, bali pia yanayohusu vitisho kwa waandishi.

Amesema kwa mujibu wa kanzi data (database) ya baraza hilo waandishi hao walikumbwa na mikasa mbalimbali ikiwemo kunyimwa taarifa, kutishiwa, kukamatwa bila hatia, kuondolewa kwa nguvu katika eneo la tukio wanalo ripoti, na kuharibiwa vifaa vya kazi.

“Matukio ya waandishi kupigwa, kunyang’anywa vifaa vyao vya kazi, kunyimwa taarifa, kukamatwa, kutishwa na kufungiwa kwa vyombo vyao yamepungua ukilinganisha na miaka miwili iliyopita,”amesema.
 
Back
Top Bottom