Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Umati wa watu umejitokeza leo nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar es Salaam ukishinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania iliyoshikiliwa nhini Afrika kusini kufuatia kesi ya fidia inayomhusu Bwana Hermanus Steyn wa nchio hiyo na Serikali ya Tanzania.
******
Kundi la Watanzania limejitokeza leo nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo jijini Dar likishinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania inayoshikiliwa Afrika Kusini
Ndege hiyo inashikiliwa kwa siku tano zilizopita kutokana na kesi ya kudai fidia inayomhusu Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini dhidi ya Serikali ya Tanzania
Watu hao waliokusanyika nje ya Ubalozi huo wameonekana wamebeba mabango mbalimbali huku wakiimba “Tunataka ndege yetu”
UPDATES
Watu watatu wanaodaiwa kuwa viongozi wa maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania yaliyofanyika nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini wanashikiliwa na Polisi
Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa amesema wao kama Jeshi la Polisi hawaruhusu maandamano wala mtu kufanya anavyofikiria yeye
Amesema “Baada ya kupata taarifa niliamuru Kikosi cha kutuliza ghasi (Field Force Unit - FFU) na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala kwa ajili ya kuchukua hatua, kwanza kuzuia maandamano na kuwakamata walioratibu maandamano
Aidha, ameongeza kuwa chochote watu hao wanachotaka kupeleka kwa umma wanaweza wakaandika au wanaweza wakatuma wawakilishi