Waandamanaji huko Hongkong waanza kuiomba USA na Trump kuwasaidia

China ina mfumo mbaya sana wa siasa!

Mfumo wa chama kimoja cha CCP!

Wananchi wote wanakandamizwa na hakuna demokrasia!

Members wote wa CCP ndio wenye madaraka wananchi 1.2Bil wanafuata hao CCP

Rushwa ni kubwa,wanaoruhusiwa kula rushwa ni CCP pekee!

Haki za binadamu hakuna!

Mfumo ya mahakama ni wa hovyo kabisa,mahakama hazitoi haki kwa wote kwa usawa!

Censorship kubwa kwenye mitandao nk!

CCP ndio inasimamia propaganda na vyombo vyote vya habari China!

Their narrative is correct,others hazitakiwi!

Halafu Jiwe na CCM wanasema tu-copy huo upumbavu!

Majinga kabisa haya maCCM!
 
POINTS
Fitina za mmarekani hizo kuiangusha uchina. Hapa China anahitaji kutumia nguvu ya ziada akilemaa hongkong inaondoka.amuulize Putin mbinu alizotumia kuichukua Crimea
Anachotaka Amerka Ni Kuigawa Uchina Tu Ili Hata Iwe Wepesi Kuitawala Kwamaana Yawepesi wa China Kushindana Na US

Well Jamaa Wanatakiwa Watumie Nguvu Zaidi Ya Zile Za Crimea Asee Bila Hvyo itawakost den
 
Fitina za mmarekani hizo kuiangusha uchina. Hapa China anahitaji kutumia nguvu ya ziada akilemaa hongkong inaondoka.amuulize Putin mbinu alizotumia kuichukua Crimea
Mkuu Kwaio unaamini Waandamanaji wa Hongkong wamehongwa na USA under CIA?
 
kinachofanyika Hong kong tukizembea kitakuja tu kutokea na Tanzania.. ipo siku watu watalipwa hela waingie road waandamane kupigania haki za mashoga.
Screenshot hii comment utakuja kukumbuka.
 
Kihistoria HK ni sehemu ya China.

Opium war ndiyo iliyosababisha Mchina kupokonywa maeneo yake ikiwemo HK na Waingereza. Chanzo cha hii vita ni baada ya Mfalme wa China kupiga marufuku nchini mwake uuzaji wa drugs ambao ulikuwa unafanywa na Uingereza. Ambapo awali China ilimwambia Uingereza iache kupitisha drugs na kuuza nchini mwake kutokea India, Uingereza ikakataa kusikia hilo shauri. Baada ya China kupiga marufuku Uingereza ikaivamia China na kuipiga.

Kipindi HK ipo chini ya Uingereza hizi vurugu zinazotokea leo hazikuwepo. Kwa sababu wakazi wa Hong Kong walikuwa ni daraja la chini na hawakuwa na uthubutu hata wa kuandamana kwa sababu risasi zilikuwa zinawahusu. Mkono wa utawala wa Uingereza ulikuwa kwa Hong Kong ulikuwa ni mkono wa chuma. Hata miaka ya 90 hii karibuni kabla ya Hong Kong kurudishwa tena kwa China bado Hong Kong wakazi wake walikuwa daraja la chini.

Miaka ya 1980 kuelekea 90 utawala wa Uingereza ukaanza kubadili mtaala wa elimu wa HongKong, kwamba HongKong ilikuwa inanyonywa na kutawaliwa kimabavu na China na Uingereza ikabidi izuie hiyo hali. Mfumo wa elimu uliyowekwa na utawala wa Uingereza ni wakazi wa HK wawachukie China bara. Na kwa hili amefanikiwa. Kwani vijana wa HK wanachukia China ya bara, wanachukia kuitwa Wachina na wanachukia lugha yao ya mandarin. Lugha wanayoipenda ni Kingereza.

Mwaka 1997 Hong Kong ilikuwa inatoa 20% ya GPD ya China. Kwa sasa inatoa 3% tu. Biashara za kimataifa wakazi wengi wa China bara walikuwa wanaenda kufanyia Hong Kong. Kwa hili, Hong Kong ikawa inachukua 50% yote ya biashara za kimataifa kutoka China bara. Kwa sasa imeshuka mpaka 12%. Stock market ya Hong Kong ilikuwa ni X 2 ya China bara. Miaka 15 iliyopita bandari ya Hong Kong ilikuwa ndiyo bandari kubwa(kama siyo miongoni) Duniani.

Lakini hizo fursa kwa sasa zimepungua sana. Sababu kuu ni kwamba miaka ya nyuma China bara ilikuwa masikini na Hong Kong ni tajiri. Lakini China bara ya sasa ni tajiri. Zile biashara zilizokuwa zinafanywa kwa kupitia Hong Kong sasa hivi zinafanywa bara. Stock market ya Hongkong imezidiwa kwa sana na miji kama Shenzhen na Shanghai. Hata bandari China bara hategemei tena ya HongKong. Bali ana bandari zake miji kama ya Shenghai, Shenzhen, nchi kama Singapore napo kuna bandari. Kwa hiyo ile faida kubwa waliyokuwa wanaipata Hong Kong imepotea kwa kukua kwa China bara na Dunia kwa ujumla.

Mwaka 1997 Hong Kong inarudishwa tena China bara kutoka utawala wa Uingereza hapa ndipo kitimtim kilianza. Hong Kong ameshajazwa sumu kwenye mfumo wake wa elimu na historia yao imepotezwa kwamba wao ni Wachina. Hiki ndicho Muingereza alichokifanya. Vijana wa Hong Kong wanaandamana wanasema wanataka Democracy lakini ni Democracy gani inaruhusu raia kuandamana wamevaa mask. Wanaweka vigingi kwenye barabara kuu za Hong Kong, wanaleta vurugu Subway na kuzuia zisiondoke, wanawapiga na kuwavamia raia wenye msimamo wa tofauti na wao, wanawapiga polisi na kuchoma majengo ya polisi. Hiyo haitoshi! Wana occupy airport.

Halafu wanasema wananyimwa uhuru! Nchi gani Duniani itakayoweza kukuachia kufanya hivyo(?) Na kwa nini wakikamatwa na polisi wakivuliwa mask zao hawataki sura zao zionekane wanainama chini? Wanaondamana wote hawataki kwenda kazini. Swali ni nani anaeyafadhili hayo maandamano? Halafu ajabu Hong Kong kuanzia maji, umeme ni mambo mengine wanategemea na vinafadhiliwa na China bara. Yani Xi Ping akikata hivyo Hong Kong inakuwa kijiji.

Hata hiyo sheria aliyotaka ipitishwe ni baada ya Hong Kongers wapenzi kwenda kula bata Taiwan. Kijana Chan akamuua mpenzi wake huko hotelini na kurudi HongKong. Uchunguzi baada ya kufanywa Taiwan ukaonekane ameuliwa na mpenzi wake ambaye alisharudi Hong Kong. Taiwan wakamhitaji huyo mhalifu kwa sababu uhalifu umetokea kwenye ardhi yake. Bahati mbaya Taiwan na Hong Kong hazikuingia mkataba wa kuhusu raia kama raia akifanya uhalifu anaweza akasafirishwa na kuchukuliwa hatua kwenye ardhi aliyofanyia uhalifu. Kwa hiyo, ushahidi upo, lakini kesi haiwezi kuamuliwa na Chan yupo huru mpaka sasa huko Hong Kong.

Gavana wa Hong Kong baada ya hilo tukio ndiyo akaleta amendments to Hong Kong extradition bill ili kukava hiyo hali kama iliyotokea. Wanaandamana! Sasa sijui wanaandamana nini.

Na Hong Kongers wasichogundua wanatumiwa kama karata tu na west kwa Mchina. Mchina naye haumizi kichwa shughuli zake anazihamisha anazipeleka miji yake mengine. Kama Hong Kong yenyewe inategemea baadhi ya mafungu ya pesa kutoka China bara kujiendesha, miaka 5 mbeleni HonKong itakuwa hali mbaya sana kiuchumi.

Na China bara inapaa kiuchumi,ambayo watu wanakandia chama chao wanasema cha kikomyunisti lakini kimewaondoa zaidi ya raia wake million 200 kwenye umasikini. Na uhuru raia wake wanao.
 
Vikwazo gani wewe? Sasa hivi atakaemwekea China vikwazo ataumia tu na yeye. Uchina anafanya biashara na dunia nzima kwa sasa
Unadhani Crimea ilikuwa kama Hongkong au unadhani Hongkong ni kama Crimea?
Pale hapahitaji nguvu watu washatumia wiki 14. China angependa tumia nguvu ila anaogopa vikwazo
 
kinachofanyika Hong kong tukizembea kitakuja tu kutokea na Tanzania.. ipo siku watu watalipwa hela waingie road waandamane kupigania haki za mashoga.
Screenshot hii comment utakuja kukumbuka.
Mkuu ni ngumu kuwalipa kila siku zaidi ya watu 2million.
 
Back
Top Bottom