Waandaaji wa Mashindano ya Urembo Nchini Tanzania wanavyowaibia Mabinti Zetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandaaji wa Mashindano ya Urembo Nchini Tanzania wanavyowaibia Mabinti Zetu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, Jun 26, 2009.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,559
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mrembo anajiandaa kwa sh 200,000 anaambulia 50,000 tu[/B


  ]Mchakato wa kutafuta warembo wanaowakilisha mikoa,vitongoji na vyuo ama upo katika hatua za mwisho na baadhi ya sehemu warembo wenyewe wamekwisha patikana.

  Mashindano hayo ambayo yalianza tena mwaka 1994 baada ya kupigwa marufuku na Serikali mwaka 1967 ambapo mrembo Theresa Shayo aliibuka kidedea.

  Mashindao hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ambapo uanzia katika ngazi za vitongoji hadi ngazi ya taifa ambapo mrembo wa Tanzania hupatikana.

  Ukitazama rekodi za mashindano hayo utagundua kuwa tangu mashindano hayo yaanze hakuna hata Mtanzania mmoja aliyewahi kutwaa taji la urembo wa dunia ,ingawa kuna mafaniko kadhaa yaliyopatikana kutokana na mashindano hayo.

  Inaelezwa na kutanagazwa na waandaaji kuwa washiriki wamekuwa wakipata zawadi mbalimbaki ikiwemo fedha taslimu,bidhaa na wengine kusomeshwa fani mbalimbali hasa za utalii na masuala ya hoteli.

  Jambo ambalo ni muhimu kujadili hapa ni je mashindano hayo yapo kwa ajili ya kuwasaidia wasichana hawa kimtazamo,kifikra,kielimu na suala la kujiamini au ni kwa ajili ya waandaaji kukusanya fedha kutoka kwa wadhamini na viingilio vya milangoni basi !.

  Ebu fikiria mchakato wa kukaa kwenye kambi takribani wiki mbili ambapo licha ya kwamba wanalipiwa malazi na chakula lakini wanajihudumia vitu vingine muhimu kama mawasiliano,mafuta ,vipodozi,nguo nk vitu ambavyo ni gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya sasa na upatikanaji wa vitu hivyo.

  Imeripotiwa hivi karibuni kuwa wasichana waliokuwa wakishiriki shindano la Umiss katika kitongoji cha Bagamoyo 2009 walijikuta wakitapeliwa baada ya kile kilichodaiwa ni zawadi kuyeyuka gafla ukumbini.

  Imeelezwa na vyombo vya habari kuwa washindi wa shindano hilo walitinga katika Ofisi za Kampuni ya Lino Interenational Agency Jijini Dar Es Salaam wakitaka mkurugenzi wa kampuni hiyo ambayo ndiyo waratibu wa shindano hilo washinikize mwandaaji wa shindano hilo kuwalipa zwadi zao.

  Hata hivyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Hashim Lundenga alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kapuni hiyo hausiki na suala la makubaliano ya washiriki hao na mwandaaji.

  “Kanuni zipo wazi ,kamati ya Miss Tanzania haiwajibiki kwa lolote na suala la zwadi za ngazi za chini yake,kwani hatujui waliahidiwa nini ,hilo litafanywa na muaandaaji mwenyewe na sisi tunafuatilia utekelezaji wake” Alisema Lundenga wakati akihojiwa na gazeti la Bingwa.
  Kwa ufupi ni kwamba washiriki hao tayari wametapeliwa na inawezekana hakuna atakayechukuliwa hatua zinazoweza kuwasadia washiriki bali kamati ya Miss Tanzania inaweza tu kuamua kuwanyima kibali za kuandaa mashindano hayo kwa miaka ijayo.

  Mbali na Bagamoyo ,imetangazwa kuwa Mshindi wa Miss Kigoma taambulia tu sh 250,000 .hivyo washiriki wengine wanaweza kuandoka na kifuta machozi cha sh 30,000 kila mmoja.

  Hivi hizi fedha wanazopata mabinti hawa zinakidhi haja ya ushiriki wa mashindano hayo au ni udhalilishaji wa mambinti zetu ambao kulingana na umri wa miaka 18 hadi 24 badi inawezekana wengi hawajui mipangilio ya maisha yao.

  Hii inatokana na uweli kwamba umri huo wanakuwa bado ni vijana ambao wengi wao wanakuwa ni wanafunzi ambao kimsingi hawajawaha na maamuzi sahii kuhusu nini watafanya katika maisha yao.

  Hivyo hii tabia ya kuwadhalilisha kwa kuonesha maungo yao mbele ya jamii na kulipwa ‘ujira’ wa sh 50,000 tu baada ya kutumia fedha nyingi za kujiandaa na kuwapotezea muda ni utapeli wa kiwango cha juu unaofanywa na waandaaji wa mashindano hayo.

  Hata hivyo hiyo ni tisa,kumi na tabia ya waandaaji wote karibu nchini Tanzania kuwa na mtindo wa kutoa kile wanachokiita ‘ofa’ ya kusomea fani ya masuala ya Hoteli na utalii.

  Hivi mambiti wote hawa wanataka kusomea fani hiyo,nani alisema kuwa wanaofaa kusomea fani hiyo ni warembo,je fani ya utalii na hoteli haina mahitaji ya mchepuo wa ufauru wa aina ya masomo ?.

  Ina maana hata washiriki wa urembo ambao wao wanafaa kuwa wana- mahesabu,wana-michezo au madaktari kulingana na taranta zao wakifauru kushiriki urembo na kushinda ni lazima wasomee fani hizo?.

  Hivi ni kwa nini mshindi asiulizwe fani anayotaka kusomea ili aweze kupata kile ambacho anapenda kutoka rohoni mwake au kutokana na taranta yake.

  Kulingana na michepuo ya masomo kati ya wanaowania mashindano hayo wamo wenye uwezo katika masomo ya sayansi ambao vipaji vyao labda ni kuwa madaktari au wana-mahesabu ambao wanaweza kuwa wahasibu nk.

  Licha ya kwamba wana sifa hizo na ndoto zao ni kusomea fani hizo lakini hapo hapo wanafaa kuwa warembo iweze kulazimishwa kusoma fani za utalii na huduma za hotelini ? ,Huu ni udhalilishaji.

  Soko la masomo hayo likoje kwa sasa kwani tumeshuhudia wasichana wengi wakisoma fani hizo na matokeo yao ni wachache wanaofanikiwa kupata ajira za uhakika katika sekta hiyo huku wengine wakijikuta wanafanya kazi za kuwadhalilisha ikiwemo kuuza pombe kwenye mabaa .
  Kazi hii kimtazamo wa mazingira yetu ya kitanzania hivi sasa ambapo watalii(wanaodhaniwa ni wastarabu) ni wa kuokoteza ,zinafganywa na watu ambao hawakusome fani husika na wananchi wengi wengi wanasema kama yeyote anayeweza kuvaa kimini,kufungua bia na kuwachekea walevi unaweza kufanya kazi hiyo.

  Inabidi tufike mahali watanzania tuelezane ukuiweli kwamba mashindao haya ni muhimu kwa wasichana hawa kuonesha vipaji vyao vya kujiamini,kujieleza nk lakini kile wanachopata ni sawa na bure .

  Pia kuna huii tabuia ya wasanii wanaotumbiza siku ya Mashindano ambao hulipwa zaidi ya mara kumi ya mshindi wa Kwanza,Hii ni aibu.

  Ni wajibu wa serikali kuingilia kati kuhakikisha mashindao haya yanakuwa na usimamizi unaostahili tofauti na sasa ambapo wasichana hawa wanaibiwa mchana kweupe na wezi(waandaaji) hawakamatwi.

  Ni ajabu Serikali kupitia idara ya Polisi kukimbizana na mwizi wa mayai ya sh 500 tena kwa kutumia bunduki zenye risasi,filimbi,magari nk huku matapeli hawa waandaaji wa mashindano ya urembo wakiachwa ‘wakiwachuna’ washiriki wa urembo.

  Ajabu ni kwamba siku warembo hawa wanapokuwa wakitapeliwa ,katika siku ya kutafuta yule ‘wanayemuita’ mrembo ukumbi mzima unalindwa na polisi au kwa lugha nyingine ni kwamba polisi wanawasaidia wezi kuimbia mambinti zetu.

  Kibaya zaidi hata baadhi ya viongozi wa serikali ndiyo wanakuwa wageni rasmi hali .

  Imeripotiwa na vyombo vya Habari wiki jana kuwa Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki dk diodorous kamala aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Kagera alilazimika kuongeza fedha kwa mshindi wa kwanza.

  Haikuelezwa kama aliongeza fedha hizo baada ya kusikia kiasi ambacho kilitanagzwa kwa mashindi wa kwanza kuwa ni kidogo au aliamua kutoa motisha lakini ukuweli ni kwamba hata yeye mwenyewe aliona soni ya kutoa zawadi kwa mashindi wa kwanza ambayo ni kiduchu.

  Nadhani tufike mahali tubadilike vinginevyo tutaendelea kuwalea waandaaji wakiendelea kuwaibia washiriki huku wao wakipata faida kibao kutoka kwa wadhamini kwani ni vigumu kupata wadhamini zaidi ya 14 huku mshindi wa kwanza akapata sh 250,000 ,achilia viingilio vya milangoni.Tumechoka wezi hawa wafikishwe mahakamani !.
   
 2. B

  Bw.Ukoko Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri we ujajua kuwa hiyo ni biashara na katika biashara kama hiyo kuna wanaokula na wanaoliwa.
  hilo ni suala la kawaida hapa Bongo ila ulichosema cha kushanagaza ni ile statment yako kuwa sifa kuu ya kuwa muhudumu wa baa ni kuchekea waqlevi,kuvaa vimini na kujua kufungua pombe hii si kweli bali wanaofanya hivyo ni kuidhalilisha taaluma ya uhudumu wa hoteli.

  chao
   
Loading...