Waalimu, Wingi wenu ni mtaji ktk siasa yetu utumieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waalimu, Wingi wenu ni mtaji ktk siasa yetu utumieni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Aug 3, 2012.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Maamuzi ya Mhakama juu ya mgomo wa waalimu una ishara mbili. Kwanza ni upuuzi wa mahakama zetu pili ni somo kwenu waalimu jinsi munavyotumika ktk siasa na baadaye kudhalaulika.

  Mahakama iliwahi kusikiliza na kuamua kuzuia mgomo wa waalimu siku ya jumapili. Iweje mahakama hiyo hiyo ikatae waalimu kupeleka notice ya mgomo ijumaa eti j-mosi iklikuwa ni siku ya mapumziko. Hizi ni mahakama kweli au ni mabaraza ya wahuni kutafuta muuza bangi?

  Ombi langu kuu ni kuwataka waalimu wafahamu umuhimu wao ktk siasa za nchi. Waalimu saidieni kuwaelimisha vijana walioko form 1 hadi 4 waelewe ubovu wa wanasiasa tulionao. Vijana hawa watakuwa na umri wa kupiga kura 2015.

  Huko vyuo vikuu inaeleweka maana siamini kama kuna muhadhili anayeweza kusifia utawala huu. Idadi hiyo yote kwa ujumla inatosha kabisa kutoa maamuzi ya chama gani kinastahili kutawala nchi hii.

  Waalimu mutanisikitisha kabisa kama serikali hii itawakumbuka siku chache kabla ya uchaguzi, nanyi musahau ubovu huu wa leo na kuanza kuwasifia kwa nyimbo.

  Mwalimu una nguvu za kutosha kisiasa. Chukuwa hatua.
   
Loading...