Waalimu watishia kuing'oa CCM; Wasema hakuna maisha bora chini ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waalimu watishia kuing'oa CCM; Wasema hakuna maisha bora chini ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurzweil, Aug 6, 2012.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,895
  Likes Received: 4,748
  Trophy Points: 280
  na Abdallah Khamis | Tanzania Daima | Agosti 06, 2012  WAKATI walimu wakikubali kurejea kazini na kuendelea kutafakari amri ya mahakama, mkakati mzito unapangwa kuhakikisha hawakiungi mkono Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tangu kutolewa kwa kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba mgomo huo si sahihi na serikali yake haina uwezo kutimiza madai yao na kufuatiwa na uamuzi wa mahakama, walimu wamekuwa wakiangalia namna nyingine ya kuibana serikali.

  Mwishoni mwa wiki, walimu katika wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza, walikuwa na kikao kizito ambapo pamoja na mambo mengine, walipendekeza kuiangusha CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.

  Katika mkutano huo ulioitishwa na uongozi wa Chama cha Walimu (CWT) na kufanyika katika ukumbi wa Afro Berch mjini Nansio Ukerewe, baadhi ya walimu ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, waliwataka wenzao waungane kuing'oa CCM kwa madai kuwa serikali inayoiongoza imeshindwa kusimamia maslai yao.

  "Ndugu zangu walimu, walimu tusitarajie kupata maslai bora kama CCM itaendelea kushika dola. Hebu angalieni tangu tulipoanza mvutano na serikali chama hicho kimebaki kimya huku kikitambua matatizo makubwa yanayotukabili. Tuungane tufanye maamuzi magumu mwaka 2015," alisema mwalimu huyo.

  Huku akiungwa mkono na walimu wengi, mwalimu huyo bila kumung'unya maneno, alisema ingawa maadili ya utumishi wa umma yanazuia watumishi kushiliki siasa, lakini muda umefika kwa walimu kutumia ushawishi wao kuhakikisha mwaka 2015, CCM inang'oka madarakani.

  Mwalimu huyo alisema, walimu wakiamua kwa wingi wao wanaweza kwani ndio wanaotumika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa uchaguzi.

  Mwalimu mwingine aliungana na mwenzake kuishambulia CCM kwamba inalinda kundi dogo la wanasiasa wanaoneemeka na rasilimali za taifa huku Watanzania wengi wakikabiliwa na umaskini.

  Mwalimu huyo pia aliushambulia mfumo wa mahakama kwamba hauko huru kwenye kutoa maamuzi, akitolea mfano uamuzi wa kesi yao kuwa ulikuwa na mkono wa serikali.

  Kwa upande wake, Katibu wa CWT wilayani humo, John Kafimbi, alimlalamikia Rais Kikwete kuzungumzia kesi yao huku akijua fika kwamba suala hilo liko mahakamani.

  Aliwataka walimu wajipongeze kwani katika kipindi cha mgomo, wamedhihirisha kwamba wakiamu wanaweza kupigania haki zao.

  Jijini Dar es Salaam, Chama cha Wananchi (CUF), kimesema Rais Kikwete ameudanganya umma kwamba serikali inahitaji asilimia 75 ya bajeti yake kuboresha maslahi ya walimu tu wakati kiasi hicho ni kwa ajili ya watumishi wote.

  Mbali ya hilo, CUF imeitaka serikali kuacha kutumia mahakama kuzima madai ya msingi ya walimu bila kutafuta njia sahihi ya kutatua.


  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema katika mazungumzo yake na wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika Ikulu jijini Da es Salaam Agosti mosi, Rais Kikwete alichukulia madai ya walimu na kulinganisha na nyongeza ya wafanyakazi wote serikalini badala ya kuja na tamko la kushughulikia matataizo ya walimu.

  "Rais anaposema tutatumia asilimia 75 ya bajeti kama tukitekeleza madai ya walimu hawatendei haki Watanzania waliomsikiliza kwani alitumia takwimu za wafanyakazi wote serikalini kama wataongezewa mishahaya kwa kiwango hicho na kuyafanya ndiyo madai ya walimu," alisema Prof. Lipumba.

  Alisema, ingawa CUF haiamini kama migomo ya wafanyakazi ndio suluhu la matatizo, inaamini walimu wana madai ya msingi na ya haki yanayopaswa kushughulikiwa na kupewa kipaumbele.

  Mwenyekiti huyo wa CUF alimshangaa Rais Kikwete kushindwa kueleza mikakati ya kutekeleza madai ya walimu ili kuwanusuru na hali ngumu ya maisha.

  "Serikali isiyo na mipango kwa vyovyote vile haina uhalali wa kuwatumikia wakulima na wafanyakazi, na hali hiyo inaitia aibu serikali inayoamua kuwahadaa walimu kwa mambo yaliyo wazi," alisema Prof. Lipumba.

  Alisema kuna fursa nyingi ambazo serikali ya CCM imeshindwa kuzitumia na kama zingetumiwa ipasavyo, leo kusingekuwa na madai ya walimu wala wafanyakazi wa kada nyingine.

  "Kwa kweli elimu ya Tanzania itaendelea kuwa duni ikiwa mchezo huu wa kuwapiga danadana walimu utaendelea….vigogo wa CCM ambao watoto wao wanasoma katika shule za kimataifa na za kimombo, katu hawawezi kuwafikiria watoto wa maskini wasio na mbele wala nyuma," alisema Prof. Lipumba.

  Alibainisha kuwa lazima walimu watambue CCM haiko madarakani kutatua matatizo yao, hivyo ni vema wakaungana kuhakikisha chama hicho kinaondoka madarakani.

  Hivi karibuni Mahakama Kuu divisheni ya kazi ilisitisha mgomo wa walimu kwa madai kuwa ni batili.

  Mahakama hiyo iliamuru pande zote zinazotofautiana kurudi katika meza ya majadiliano kwa ajili ya kusaka suluhu.
   
 2. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Walimu sijui walifikiri nini. Kama Madaktari walishindwa, wao walidhania vipi wataweza? Kwa Serikali ya CCM labda wagome Wanajeshi.
   
 3. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hio ndio ccm wakati nchi inamatatizo rais ameenda kugawa ngombe na kuendeleza taarabu eti barabara ya mbugani itajengwa wanachi wasiwazikilize hao
  yaani ahadi ndio mtaji wao
   
 4. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,895
  Likes Received: 4,748
  Trophy Points: 280
  Ahsanteni kwa marekebisho.
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hao si walimu ni watu tu kama wewe ndo wenye mawzo hao, suala la hali ya uchumi wa nchi si la chama bali ni mabadiliko ya kiuchumi duniani kote.

  Kwa mtu mwenye mawazo finyu kama wewe anaweza kuamini kuwa matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi nyingi duniani kote yanasababishwa na vyama tawala vya nchi hizo, wakati hata nchi nyingine hazina mfumo wa nyama vya siasa.
   
 6. a

  afwe JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Walimu wamechelewa sana kujua kuwa tulipofikia, kwa sera za CCM maisha bora ni ndoto!
   
 7. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Sasa kwa maelezo haya nani mwenye finyu akili...
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kumbe ile Maisha Bora kwa kila Mtanzania ilikuwa haiwahusu waalimu, bado sijabaini kundi lipi hasa ndilo lililokuwa likilengwa.
   
 9. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,895
  Likes Received: 4,748
  Trophy Points: 280
  thatha Hivi aliyekwambia hii habari nimeandika mimi nani? Hapo umeonyesha kua wewe ndio unaakili finyu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndugai, nape, rizi, lowasa, etc
   
 11. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Na bado mkicheka na nyani(ccm) mtavuna mabua,siku zote mlikuwa wapi kulijua hili?Kumbe nyie ndio mnawalea hawa manyang'au?Afadhali amewaonyesha yeye ni wa shetani wa aina gani.....
   
 12. m

  mob JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  kwa hili la migomo ya madaktari,PPF,NSSF,LAPF na migomo ya walimu kupona kwa ccm inahitaji miujiza
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Ningewashangaa sana waalim wasingeyasema hayo.
   
 14. i

  iseesa JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa WAKOME. Hawa hawa waalimu ndio wanaoiba kura za wapinzani ili MAGAMBA washinde kwenye chaguzi. Sasa "kimenuka kwao" wanalalama.
   
 15. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wee mbwiga, hapo kwenye bold ndio kitu gani? Sasa nani ana mawazo finyu, wewe au mleta uzi? Mwenzio anajadili hali ya uchumi chini ya Chama cha Mabwepande, wewe unawaza nyama! Akili zingine bwana? Utadhani wewe si binadamu!
   
 16. GAMAH

  GAMAH Member

  #16
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ha ha ha nchi sasa kila mtu anajua kila mtu ataing'oa ccm kila mtu ana mamlaka
   
 17. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ukitaka kufanikiwa kumwangamiza adui vitani, sio vyema kuiweka mikakati yako ya jinsi yakumwangamiza, la sivyo unampa njia ya kujihami. Madaktari, Waalimu, wafanyakazi wa sekta zingine mlio chini ya Ndg. Mgaya pangeni mikakati yenu kwa siri ili muishtukize kuiangusha CCM kwa kuwadharau na kuwapuuza. Msitoe siri ya mikakati yenu kama kweli mna maanisha kuiangusha CCM 2015. 2015 mimi, na familia yangu 6, majirani 4 , marafiki 10 na wanakijiji wasiopungua 10 tumeapa kuiangusha CCM liwalo na liwe. Ombi kwa kila kila mwalimu, kila daktari, kila mfanyakazi kama angeweza kuwashawishi kuanzia sasa jumla ya watu wasiopungua 30, tunaweza kupata idadi isyopungua watu milioni 10,500,000 dhidi ya CCM. Hii inawezekana kuanzia sasa. Suala la kukutana wafanyakazi na kutangaza kutishia kuiangusha CCM 2015 halina tija maana hata 2010 tishio kama hilo lilikuwepo lakini halikufanikiwa. Hebu tutembee katika maneno yetu kama kweli tunahitaji mabadiliko ya kweli.
   
 18. M

  MTK JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  They can take a leaf from the 2002 Kenyan teachers election work book where by they used their substantial numbers to throw out KANU! of course by complementing the efforts of the Raila's, Muite's, Kibaki's and the other young turks who championed the reform agenda!

  Mwalimu Oluoch of CWT has kins and kith accross the border in kenya, they can come in handy for tutorials about the implementability of the action plan!

  Unfortunately our teachers have been too laid back for far too long! Wamesubiri sana "Mana" kutoka peponi but it has not been fourthcoming!!
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  06/08/2012

  walimu wakuu 10 wavuliwa madaraka kwa kuhamasisha mgomo  Walimu Wakuu 10 wa shule za msingi wilayani Tarime mkoani Mara, wamevuliwa madaraka yao hayo baada ya kubainika kufunga ofisi, kushindwa kulinda mali za shule na wanafunzi na kuhamasisha mgomo kwa walimu wenzao.

  Ofisa Elimu wilayani humo, Emanuel Johnson alikiri walimu hao kuvuliwa madaraka yao tangu Agosti mosi, mwaka huu na kwamba bado mchakato unaendelea wa kuwabaini walimu wengine waliohusika na mgomo huo, "Ni kweli tumewavua madaraka Walimu wakuu wa shule za msingi 10 tangu Agosti Mosi na tunaendelea na mchakato wa kuwabaini wengine waliohusika katika kushindwa kulinda mali za shule na wanafunzi na kufunga ofisi za umma na kuwezesha walimu kugoma kufundisha na kuathiri sekta ya elimu," alisema.

  Alimtaja mmoja wa Walimu Wakuu waliovuliwa madaraka kuwa ni Esther Magesa wa Shule ya Msingi Mturo ambaye alikamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbili na kuachiwa baada ya kudhaminiwa.

  Walimu wengine waliovuliwa madaraka wanatoka shule za msingi za Kwihanche, Reamagwe, Nkerege, Gibaso, Kitagutiti na Nyamwino. Walimu Wakuu wa shule mbili, za Nyankoni na Itiryo, walipewa onyo lakini endapo itabainika kuwa walihusika, na wao watavuliwa madaraka.

  Johnson alisema Polisi wilayani humo inamsaka Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Tarime, Matinde Magabe kwa tuhuma za kuchochea mgomo wa walimu, kutoa vitisho kwa walimu waliokataa kugoma na kusababisha uvunjivu wa amani katika baadhi ya shule.  Source: wavuti - wavuti
   
 20. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yaani mpaka leo haujaelewa ni kundi gani lililengwa,kama kusikia hausikii na kuona je? aliposema maisha bora kwa kila mtanzania ilikuwa ni kuzuga tu ukweli ilikuwa ni maisha bora kwa Mafisadi kwani si matokeo yameshaonekana na yanaendelea kuonekana!
   
Loading...