Waalimu wa ujasiriamali wahitajika mwanza.

bereng

Senior Member
Feb 5, 2013
114
21
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Tuwafikie Tanzania inatoa nafasi za kazi ya ualimu wa ujasiriamali kwa watu wenye ujuzi wa kutengeneza bidhaa mbalimbali zenye viwango. Bidhaa hizo ni pamoja na:-
sabuni aina zote, manukato, mafuta ya kupaka ya mgando, shampoo, losheni, batiki, mishumaa, dawa za usafi, unga wa lishe, keki, wine aina mbalimbali, n.k

Tunahitaji pia watu wanaoweza kufundisha:- upambaji ktk sherehe, ushereheshaji, muziki, na sanaa ya maigizo.

Kama una ujuzi kati ya mambo yaliyotajwa hapo juu, tutumie maombi kupitia baruapepe: tuwafikiemwanza@gmail.com
Maombi kwa wakazi wa Mwanza yatapewa kipaumbele.
 
Unajua lakini maana ya Mjasiriamali? Inakuwaje mjasiriamali akaajiriwe? Hii inapatikana Bongo tu.
 
Na kama kweli mnataka kuwasaidia watu wapeleken wakasome kwa vitendo huko huko ila hii ya kusema mnaajiri walimu wakasiriamali ni kupotosha. Hakuna mwalimu mjasiriamali na mjasiriamali hawezi kuwa mfanya kazi ni lazima moja kati ya hizo ife.
 
Unajua lakini maana ya Mjasiriamali? Inakuwaje mjasiriamali akaajiriwe? Hii inapatikana Bongo tu.

Mkuu chashs huyu ni tapeli tu anawaibia watoto wa masikini inabidi MODS waamuke haya matapeli wasiyape airtime.
 
Back
Top Bottom