Waajiriwa wengi mtakufa masikini sana. Hivi mnaishije?

Sham777

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
334
836
Habari zenu naomba niwape mrejesho. Baada ya kukaa kwa shemeji yangu kwa zaidi ya miaka Mitatu na kupitia changamoto nyingi nimefanikiwa kupata kazi katika kampuni ya Wachina tunauza na kusambaza Solar System. Ni jambo la heri sana kwangu maana nime fight kwa mda mrefu sana bila ya kupata kazi na umri wangu tayari ni mkubwa ivyo kukaa kwa chini ya mtu ni mtihani sana..

Kutokana na kuchoka kukaa kwa mtu na kuwa tegemezi, kukosa Privacy na mambo kibao ambayo siwezi yataja, siku nilivyo nipigiwa simu niende nikasaini barua ya mkataba wa kazi wala sikufikilia mara mbili. Mkataba ni kufanya kazi Chini ya iyo kampuni ndani ya miaka Miwili na Mshara wangu ni 270,000/= ( laki mbili na sabini tu) na makubaliano yetu kuwa mshara utapanda endapo kampuni ikianza kuingiza faida sababu hii ni kampuni mpya na imeanza kipindi kibay cha anguko la kiuchumi kutokana na Hawa CVD Virus.

Nimefanya kazi mwezi mmoja nikitokea Nyumban (kwa shemeji) mbaka nilipo pata mshara wangu wa kwanza na kuaga na kuondoka kwa aman kwa Shemeji nikiwa na iman sasa naenda kuishi maisha yangu yatakayo kuwa na furaha, uhuru, privacy na aman ila mambo ni tofauti sana na nilivyo tarajia.

Nilipo pata mshahara wangu kitu cha kwanza nilitafuta chumba nikafanikiwa kupata chumba na sebule ambayo nalipia elfu 60,000/= kwa mwezi na nimelipia miezi mitatu jumla 220,000 pamoja na malipo ya dalali. nikafanya shopping ya nguo za kuvaa kazini sababu ya nguo nilizo kua nazo zilikuwa ni kuu kuu kidogo jumla ikani cost 40,000/=. Pia kutokana nilikuwa na kaakiba kangu nikafanikiwa kununua tuvitu tudogo twa kunirahishia maisha kwangu ila maisha yamekuwa magumu mara mia zaidi.

Lengo la huu uzi ni kuwauliza wenzangu mnaishi vip ambao mmeajiriwa na mishahara yanu aizidi laki 4 na wengine mnaishi kabisa na familia zenu na mnasomesha, je kuna ujanja ujanja mwingine huwa mnatumia ili angalau kuwe na wepesi wa maisha. Binafsi kwa huu mshahara sizani kama nitadumu hata miezi sita sababu kuu nimeona nitakuwa nafanyia kazi tumbo tu na hakuna nitakacho save kwa ajiri ya future, na hivi karibuni natarajia kuitwa baba na ndio sababu nimechukua chumba na sebule sijachukua single room.

Nahitaji sana ushauri wenu ili angalau na mim niishi maisha ya kawaida sababu nina mahitaji mengi sana ya kununua kwa mshahara wa mwezi huu sizani kama nitaweza. Nashukuru pia siku ninayo ondoka kwa shemeji kuna vitu niliazimwa kwa ajili ya kuanzia life kama godoro na vitu vingine ambavyo natakiwa nirudishe pindi nitakapo nunua vya kwangu.

NB:
Kwa wale wabobezi wa Lugha mtanisamehe bure mim sio mwandishi mzuri na pia sio mwongeaji mzuri wa Lugha ya kiswahili. Nachanganya sana L na R pia H na A kutokana na mazingira niliyo kulia na kuishi...
 
Hongera sana kwa kuanza kuyajua maisha kiuhalisia..Mwanzo siku zote huwa mgumu.Usikate tamaa,,Muandae mama kijacho aje kuwa mjasiliamali ili muweze kuendesha maisha kwa unafuu..Mungu akujaalie
Asante sana kwa ushauri wako.. Nitafanya ivyo lazima nimuandalie mazingira mazuri ya ujasiliamali asije kuwa tegemezi..
 
Duh! Mkuu nikupe hongera sana! Ila nakushauri kama una mtu wa kufungulia ata Ofisi ukipokea mshahara wa mwezi fungua ofisi hata ya kuuza vitafunwa boss. Life ni gumu mno watu tunalipeleka kibishi mno

Lakini ushauri wa Mwisho usiache kazi kama ofisi yako haijasimama vzr man. Mungu akutangulie
 
Yaani kwenye title yako ututukane kwamba tulioajiriwa ni wazembe wa kufikiri hivyo tutakufa masikini na pu*mb zetu mbili😠😡 halafu unatuomba ushauri tukupe maujanja ya kutoboa na hii mishahara yet yetu midogo. Pumbav huna adabu. Nina mbinu nyingi ila sikupi. Nautakoma maana sasa hivi hata kubeti Hakuna.
 
Wacha wenge kijana utalost mapema sana. Huo mshahara wa 270 wewe binafsi haukutoshi, unatuuliza ufanye nini, kabla hujapata jibu unawaza kuwa na familia!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wenge mkuu haya mambo huwa yanatokea .. Mim pia napenda sana ningekuwa mwenyewe nichukue ata single room ya 15k
 
Mnaosema kachukua CHUMBA cha ghali sidhani kama mpo Sahihi.

Kuna vyumba ni bei rahisi ila changamoto zake ndio zinakuja kufidia cost kubwa baadae

_Location

Huwez acha chumba cha karibu kisa ghali uende kulipia chumba cha mbali na eneo la kazi cost utazozipata za nauli,muda,usumbufu utajilaumu zaid


_Usalama
.unachukua chumba cha elf 10.. unadhan kitakuwa na hali gani?

Essential service
Umeme na maji.. chumba unakuta elf 15.. maji unachota mtaa wa 5 hukoo unabebelea mandoo,umeme hakuna.. unaenda kuomba kwa jirani au unalipia kila siku uchajiwe simu vibandani..

Ukiwa na chumba kam hiki hata kununua vitu ni ngumu sana maana ushajizoesha maisha ya kifukara tu



Ushauri wangu:

Hata uwe unalipwa laki mojaa jitahid UKAE sehem nzuri. Ina faida nyingi Maisha ndio hay haya... Ya nini ukae bandani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pambana sana hiyo pesa ni ndogo kwa mahitaji yako haswa kama unaishi mikoa ambayo maisha yako juu utapata tabu sana
Mkuu ubaya wa hii kazi ninayo fanya haina kujiongeza na pia inakula sana muda ivyo nikitoka Job siku inakuwa imeisha tayari.. Nipo Dar..
 
Mnaosema kachukua CHUMBA cha ghali sidhani kama mpo Sahihi.

Kuna vyumba ni bei rahisi ila changamoto zake ndio zinakuja kufidia cost kubwa baadae

_Location

Huwez acha chumba cha karibu kisa ghali uende kulipia chumba cha mbali na eneo la kazi cost utazozipata za nauli,muda,usumbufu utajilaumu zaid


_Usalama
.unachukua chumba cha elf 10.. unadhan kitakuwa na hali gani?

Essential service
Umeme na maji.. chumba unakuta elf 15.. maji unachota mtaa wa 5 hukoo unabebelea mandoo,umeme hakuna.. unaenda kuomba kwa jirani au unalipia kila siku uchajiwe simu vibandani..

Ukiwa na chumba kam hiki hata kununua vitu ni ngumu sana maana ushajizoesha maisha ya kifukara tu



Ushauri wangu:

Hata uwe unalipwa laki mojaa jitahid UKAE sehem nzuri. Ina faida nyingi Maisha ndio hay haya... Ya nini ukae bandani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana kaka.. Umeongea jambo la maana sana najua kila mtu atajifunza kupitia hii comment.
 
Nimekosa ajira za serikal,nimepewa mradi wa familia niusimamie na kunasiku huwa natoa pesa za matumizi kwa siku tunatumia elfu 20-30 kwa familia ya watu 5,nawawazia walioajiriwa kwa mishahara ya laki 4 wanaishije
 
Back
Top Bottom