Waajiri mmekuwa wabinafsi; kazi mnazotoa mnataka wenye 'experience' -- wahitimu wapya mnataka waajiriwe na nani? Serikali nayo ipo kimya

Mayunga234

JF-Expert Member
Feb 17, 2017
1,726
1,989
Kuanzia 2015 hadi Leo Asilimia kubwa ya waajiri wamekuwa wabinafsi mno wanataka kuajiri watu wenye Experience tu hawa waliomaliza Chuo wataajiriwa na nani.

Hata Nafasi za kujitolea kupata experience hamtaki kuwapa, graduate’s wamekuwa na hali mbaya sana mtaani wanakufa na msongo wa mawazo.

Walioajiwa wako busy kuwashauri waliomaliza Chuo wajiaajiri Ukiangalia Mtaji Hawana nyumbani hali ngumu
Huu Msemo wa kuwaambia waliomaliza chuo wajiajiri, wanachukulia kujiajiri ni issue simple sana.

Mtu ajiajiri vipi mtaji hana?
Wabunge nao ndo wamekuwa wabinafsi kabisa wanashindwa kuliangalia hili swala kwa upana zaidi.

Serikali inashindwa hata kutengeneza mazingira ya kuwakopesha waliomaliza Chuo hili wajiajiri kama imeshindwa kuwapa Ajira.

Hivi wabunge wanajadiligi nini bungeni kama vitu vya msingi hivi vinachukuliwa Poa, Mnawaambia watu wajiajiri na Mitaji hawana mnataka hawa Vijana Wajiajiri vipi kwa Mfano mnawaumiza sana hawa Vijana waliomaliza vyuo vikuu.

Mnataka kuajiri watu wenye experience ya miaka mitatu hadi kumi Huu ni ubinafsi wa kiwango cha juu kabisa means mnataka hizi kazi mpeane wenyewe kwa wenyewe

NGOs ndo zimekuwa hovyo kabisa Mnawanyima watu hata kazi za kujitolea na kuwaajiri pia hamtaki mnataka mtu mwenye experience ya 5 years na kuendelea hii inaumiza sana vijana

Mmekazana mjiajiri mjiajiri Ebu na nyie mnaosema hivyo acheni kazi then mkajiajiri Muone moto wake mnaongea simple tu lakini mnawaumiza sana hawa Vijana waliomaliza Chuo.
 
1-3 years experience fresh from school ndo anatakiwa aombe hizo kazi...ndo maana ya kuelimika
 
...ndio maana wenzetu wanaojielewa wana ruhusu wahitimu wao kufanya intern kwenye companies zao ili kuwapa uzoefu wahitimu hawa, na hili linaweza fanyika kwa utaratibu Mzuri tu kuwa kila Dec makampuni yaruhusu kuajili wahitimu for 90days ili wapate uzoefu wa kazi na wakalipwa fedha za kujikimu(kichele)
 
Shida siku hizi watu wanamaliza chuo wakiwa bado na utoto hivyo kupelekea hiyo hali unataka kwenda nayo mpaka kwenye ofis za watu ndio sababu wameona mkae mtaani KWANZA akili zikue
 
Mkuu embu na wewe anzisha biashara au ngo yako alafu uajiri hao wahitimu wapya uone jinsi wanavowaumiza hao waajiri wao.ITS not that SIMPLE to employ people who lack the skills,experience and discipline to work and make money for you.
 
...ndio maana wenzetu wanaojielewa wana ruhusu wahitimu wao kufanya intern kwenye companies zao ili kuwapa uzoefu wahitimu hawa, na hili linaweza fanyika kwa utaratibu Mzuri tu kuwa kila Dec makampuni yaruhusu kuajili wahitimu for 90days ili wapate uzoefu wa kazi na wakalipwa fedha za kujikimu(kichele)

Na huku wangefanya hivo ingewasaidia sana
Ila Serikali ipo kimya
 
Mkuu embu na wewe anzisha biashara au ngo yako alafu uajiri hao wahitimu wapya uone jinsi wanavowaumiza hao waajiri wao.ITS not that SIMPLE to employ people who lack the skills,experience and discipline to work and make money for you.

Mbona hiyo system haikuwepo before
Ubinafsi tuu
 
Unatoka chuo leo unataka ajira leo,kaa mtaani kwanza hata mwaka upate experience na kujua mambo ya mtaani yalivyo coz you spent most of your time schooling,kukaa mtaani kwa namna moja au nyingine kunaleta nidham ya pesa na kujielewa ukipewa kazi za watu unakua serious kidogo ...
Ushuhuda kidogo/Ushauri:
Kuna
kazi iliwahi tangazwa kwenye kampuni ya madini inataka mtu awe na experience 3 years but he applied na alikua fresh from school ila alipata moja ya nafasi hizo...Muda mwingine unajilipua tu una apply
 
Pole sana, hizo experience requirements huwa wanajisemea tu, kuna watu wanaajirwa na hawana experience yoyote...
 
Unatoka chuo leo unataka ajira leo,kaa mtaani kwanza hata mwaka upate experience na kujua mambo ya mtaani yalivyo coz you spent most of your time schooling,kukaa mtaani kwa namna moja au nyingine kunaleta nidham ya pesa na kujielewa ukipewa kazi za watu unakua serious kidogo ...
Ushuhuda kidogo/Ushauri:
Kuna
kazi iliwahi tangazwa kwenye kampuni ya madini inataka mtu awe na experience 3 years but he applied na alikua fresh from school ila alipata moja ya nafasi hizo...Muda mwingine unajilipua tu una apply

kukaa mtaan ndo mwanzo wa depression
 
Back
Top Bottom