Waajiri migodini wanaowadhalilisha wafanyakazi kwa kuwapekua sehemu nyeti sasa kuchukuliwa hatua

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde amesema serikali itawachukulia hatua waajiri migodini wanaodhalilisha wafanyakazi kwa kuwapekua sehemu za siri. Mh. Mavunde ameyasema hayo leo wakati akijibu swali lililoulizwa na mbunge.

Picha ya Kusikitisha: Wafanyakazi wa Mgodi wa Almasi Mwadui
21.jpg

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde amesema Serikali itawachukulia hatua waajiri wa migodini wanaowadhalilisha wafanyakazi kwa kuwapekua hadi sehemu za siri, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Mavunde alikuwa akijibu swali bungeni mjini Dodoma leo kuhusu msimamo wa Serikali dhidi ya matukio ya udhalilishaji wa wafanyakazi maeneo ya migodini.

Naibu Waziri Mavunde amesema kumekuwa na matukio ya udhalilishaji kwa wafanyakazi yanayofanywa na waajiri zikiwamo baadhi ya kampuni za Wachina.

Amesema baadhi ya Wachina hao wamekuwa na tabia ya kusingizia kutojua Kiswahili kama sababu ya kutofahamu sheria za kazi nchini na kunyanyasa wafanyakazi wao.

Pia, amebainisha kuwa Serikali inatambua kutojua sheria si sababu ya kufanya kosa, hivyo imekuwa ikipokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu matukio ya udhalilishaji.

Ameahidi kuwafikisha katika vyombo vya sheria waajiri wanaoendelea kukiuka sheria za kazi nchini.

Credit: Mwananchi
 
Sitetei udhalikishaji huu lakini nilishamshudia mtu akikamatwa akiwa ameficha dhahabu ya hela nyingi Kwa kuivingirisha ndani ya condom na kuisokomeza sehemu ya haja kubwa...mambo ya namna hii ndo yanasababisha upekuzi unaodhalilisha watz tubadilike
 
Duh kumbe migodini kuna dili hivi, na suala la mchanga kusafirishwa nje mmelichukulia hatua gani? Au ndio mkuki kwa nguruwe kwa binadamu ni mchungu
 
Dili gani kupekuliwa hadi upenuni utadhani gaidi. Huu ni udhalilishaji na kinyume cha sheria za nchi.
 
Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde amesema serikali itawachukulia hatua waajiri migodini wanaodhalilisha wafanyakazi kwa kuwapekua sehemu za siri. Mh. Mavunde ameyasema hayo leo wakati akijibu swali lililoulizwa na mbunge.

Picha ya Kusikitisha: Wafanyakazi wa Mgodi wa Almasi Mwadui
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde amesema Serikali itawachukulia hatua waajiri wa migodini wanaowadhalilisha wafanyakazi kwa kuwapekua hadi sehemu za siri, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Mavunde alikuwa akijibu swali bungeni mjini Dodoma leo kuhusu msimamo wa Serikali dhidi ya matukio ya udhalilishaji wa wafanyakazi maeneo ya migodini.

Naibu Waziri Mavunde amesema kumekuwa na matukio ya udhalilishaji kwa wafanyakazi yanayofanywa na waajiri zikiwamo baadhi ya kampuni za Wachina.

Amesema baadhi ya Wachina hao wamekuwa na tabia ya kusingizia kutojua Kiswahili kama sababu ya kutofahamu sheria za kazi nchini na kunyanyasa wafanyakazi wao.

Pia, amebainisha kuwa Serikali inatambua kutojua sheria si sababu ya kufanya kosa, hivyo imekuwa ikipokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu matukio ya udhalilishaji.

Ameahidi kuwafikisha katika vyombo vya sheria waajiri wanaoendelea kukiuka sheria za kazi nchini.

Credit: Mwananchi
Hili hajalipatia ufumbuzi wafanyakazi wa buzwagi zaidi ya 1600 wamefukuzwa kazi kwa kigezo cha kufunga mgodi. Waziri kimya. Leo wanauza magari chakavu macho yamewatoka
 
Back
Top Bottom