Waafrika wawajia juu wanaopendekeza chanjo ya COVID-19 kufanyiwa majaribio Afrika

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
15,189
20,157
Supastaa wa zamani wa Inter Milan na Chelsea, Samuel Eto'o amewatolea uvivu maprofesa nchini Ufaransa kufuatia matamshi yao yasiyofaa juu ya Afrika kipindi hiki ambacho ulimwengu unatafuta ufumbuzi dhidi ya kupambana na ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Hakuna dawa ambazo zinaweza kuzuia ugonjwa huu, lakini wanasayansi wamegundua chanjo ya BCG, inayotumika kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Kupitia kituo cha televisheni cha Ufaransa LCI, Profesa Jean-Paul Mira, mkuu wa kitengo cha huduma ya wagonjwa katika hospitali ya Cochin (Paris) na Profesa Camille Locht, mkurugenzi wa utafiti huko Inserm alipendekeza ufanisi wa chanjo hiyo inapaswa kufanyiwa majaribio Afrika.

Kauli hiyo, ilimchukiza Eto'o na kutumia mtandao wake wa kijamii kwa kuandika. "Afrika sio uwanja wako wa kucheza."

Nyota wa kimataifa wa Senagel, Demba Ba, alionekana kukerwa na msomi huyo kwa kuandika, "Karibu Magharibi, ambapo watu weupe wanajiamini kuwa bora zaidi kwamba ubaguzi wa rangi na ujasusi huwa kawaida. Wakati wa kuinuka."

Kiungo wa zamani wa Ufaransa na kiungo wa Inter Milan, Olivier Dacourt alionyesha msimamo wake katika Twitter.

"Je! Ni kweli wapo siriazi?" aliuliza.

Kuna watu wamekuwa wakikimbilia Ulaya ili wasaidiwe kisiasa lakini hivi ndivyo wazungu wanavyotuchukulia

-----

Tuwe na ujasiri wa kuwaambia “ Afrika sio shamba la majaribio...

NA MOHAMMED ABDULRAHMAN

Kizaazaa, taharuki, hofu na majina mengine mengi ndiyo unayoyasikia yakitumiwa kuelezea hali inayojikuta dunia wakati huu kuhusiana na janga la virusi vya Corona au COVID-19. Ugonjwa huu ulianzia China tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini sasa hali ni mbaya zaidi Italia, Uhispania na Marekani baada ya hapo kabla Iran na Korea Kusini kuwa nchi zilizofuata baada ya China.

Hadi hivi karibuni bara la Afrika halikuwa limethirika kiasi cha kutia wasiwasi, lakini sasa Corona imeshaingia katika nchi kadhaa na kuanza kusambaa nchi za jirani. Wataalamu wanasema umetokana na watu walioingia kama watalii au raia waliorudi nyumbanio kutoka mataifa ambayo yameathirika. Vyovyote iwavyo, Corona limegeuka janga la dunia.

Tahadhari kubwa inachukuliwa na hasa kwa sababu ya idadi kubwa ya vifo katika baadhi ya nchi nilizozitaja kama Italia na Uhispania na Marekani ambako maelfu wamepoteza maisha.
Miongoni mwa hatu za kinga zinazochukuliwa na kuwataka watu wafuate muongozo uliotangazwa na serikali zao, ambazo baadhi zimeweka utaratibu wa watu kubakia ndani majumbani mwao , wakitoka tu pale inapolazimika.

Kuna nchi nyengine hatua hizo ni kama za hiyari kwa sababu watu kwa sababu mbali mbali wamelazimika kutoka kutafuta njia za kuweza kukidhi maisha yao ambayo tangu hapo ni magumu yakitegemea kipato cha siku ili angalau kuweza kupata mlo mmoja kwa familia. Mazingira ya aina hiyo yako zaidi katika nchi zetu za Kiafrika. Lakini kwa wa Ulaya sana sana wanaokiuka utaratibu uliotangazwa hufanya hivyo zaidi kwa kutojali zaidi ingawa mwamko kuhusu kitisho hiki cha Corona ni kama kwengineko.

Kuna wanasiasa na wataalamu ambao kila kukicha wanazungumzia janga la Corona na jitihada za kuhakikisha vifaa mbali mbali vinapatikana kwa ajili ya idadi ya walioambukizwa na wagonjwa inayozidi kuongezeka na mahospitali yaliofurika. Sambamba na hayo ni jinsi madaktari na wauguzi wanavyojitolea usiku na mchana , wengine wakiwa wahanga wa janga hili na kuathirika wakiwa makazini. Wengi wamepoteza maisha.

Miongoni mwa juhudi zinazoendelea ni kutafuta tiba ya virusi vya Corona. Hata hivyo tiba kwa gharama ya nani?

Hivi majuzi katika mjadala kwenye stesheni moja ya televisheni ya Ufaransa, madaktari wawili maarufu wa Ufaransa Jean-Paul Mira na Camille Locht walisababisha mjadala mkubwa mitandaoni walipopendekeza majaribio ya chanjo mpya yafanywe Afrika. Hoja yao eti kwasababu waafrika hawana vifaa na dawa za kutosha.
Mira alipotoa matamshi hayo akaungwa mkono na daktari mwenzake Locht aliyesema, “ Kwa hakika tutalizingatia vilivyo pendekezo lako.”

Hapana shaka yoyote ni matamshi ya kibaguzi na hoja yao isiyo na mantiki hata kidogo , ilioibua maswali kadhaa. Kwanini majaribio yasianzie kwanza kule ambako hali kwa sasasa ni mbaya bila kiasi na ukiliweka kando hilo kwanini yasiwe majaribio ya wakati mmoja duniani kote kwa kuzingatia hili ni janga lililoukumba ulimwengu kwa jumla ?

Miongoni mwa waafrika wa kwanza kukemea matamshi hayo ni wachezaji nyota wa kandanda wa zamani Didier Drogba kutoka Cote d´Ivoire na Samuel Etoo wa Cameroon, na Msenegal Demba Ba. Wote waliyakosoa vikali matamshi hayo kuwa ni ya kibaguzi na kusikitishwa na mtazamo wa waulaya wenye misingi ya kibaguzi kwamba Afrika ni maabara ya majaribio ya kitabibu.

Ba aliandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba bara zima la Afrika kuanzia Kaskazini hadi Kusini lilikuwa na maambukizi ya watu 6,700 na Ufaransa pekee karibu 60,000, hivyo Ufaransa kingekua kituo bora kwanza, cha majaribio yoyote yatakayofanywa

Kama kawaida wengine tukisubiri viongozi wetu watakuwa na msimamo gani kuhusu kadhia hiyo ninayoiita ya dharau, ubaguzi , unyanyasaji na kulitusi bara la Afrika. Nikitarajia Umoja wa Afrika ungezungumza , lakini haikuwa hivyo. Pamoja na hayo sikushangaa hata kidogo,kwani moja huo umezidi kuwa dhaifu. Bado kuna hali fulani ya baadhi ya watendaji wakuu katika Halmashauri kuu ya Umoja huo kuyatii zaidi mataifa yaliotutawala . Rais wa Halmashauri kuu Moussa Faki Mahamat ni kutoka Chad na aliwahi kuwa Waziri mkuu na waziri wa mambo ya nchi za nje.

Historia ya kisiasa ya Chad inafahamika sawa na nchi kadhaa zilizokuwa makoloni ya Ufaransa barani Afrika. Nilikaa nikatafakari na mwishowe sikushangaa tena , kwa sababu yaliomfika aliyekuwa Balozi wa Umoja wa Afrika mjini Washington Dk.Arikana Chimbori-Quao. Bibi Chimbori aliondolewa katika wadhifa wake, alipodiriki kuikosoa Ufaransa inavyoendeleza aina ya ukoloni mambo leo katika baadhi ya nchi ilizozitawala Afrika, ambapo nchi 14 zinawajibika bado kwa Ufaransa chini ya mkataba unaozishurutisha kuweka 85 asilimia ya pato lao la akiba ya kigeni kwenye benki kuu ya Ufaransa.

Inasemekana Ufaransa ilikuwa na mkono wake katika uamuzi wa Mahamat ambaye nchi yake Chad imo katika orodha hiyo.
Ufaransa ina kituo kikubwa cha wanajeshi mjini Ndjamena na mara kadhaa imemnusuru Rais wa sasa Idris Deby dhidi ya waasi , ambao waliwahi hata kukaribia Ikulu kabla ya kukandamizwa kwa msaada wa ndege za kijeshi za Ufaransa. Dola hilo mkoloni wa zamani limekuwa na mkono wake katika misukosuko ya Chad tangu baada ya kuangushwa Rais wake wa kwanza Francois Tombalbaye na migogoro ya wa tawala waliofuata Jenerali Felix Malloum, Goukuni Wedei, na Hissene Habre.

Kwa muda mrefu kumekuweko na minon´gono na tetesi kwamba maamuzi ya Umoja wa Afrika huwa yanajulikana Paris na miji mengine mikuu ya magharibi hata kabla ya waafrika kuyajua au hata kabla ya tamko la mwisho kutolewa.

Lakini tukitathmini kadhii ya madaktari hao wa kifaransa si Umoja wa Afrika peke yake tunaopaswa kuukosoa , viongozi wetu pia wamekuwa kimya kama walivyo kuwa kimya bara hilo na waafrika walipotukanwa na Rais Donald Trump wa Marekani.

Msimamo wa viongozi tuliokuwa nao miaka mingi ya nyuma, wa ujasiri na kujiamini ( ingawa sio wote ) hauko tena. Wakati ule angalau Afrika ikizungumza kwa sauti moja na kusikika licha ya tafauti za kinadharia na ushawishi wa wakoloni wa zamani kwa baadhi ya nchi. Miongoni mwa masuala ambako ulionekana msimamo wa pamoja ni mapambano dhidi ya ukoloni, Ian Smith kujitangazia uhuru na utawala wa wazungu wachache nchini Rhodesia 1965 na utawala wa kibaguzi Afrika Kusini.

Afrika ilikuwa na sauti iliosikika katika Umoja wa Afrika , Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote
( Non-Aligned Movement ) na hata katika Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Kisa hiki cha chanjo ya majaribio ya Corona sio cha kwanza. Kulikuwa na majaribio ya chanjo ya Polio na Ebola . Afrika pia imegeuzwa jaa la zana za vifaa vibovu vya elektroniki visivyotumika tena Ulaya , Taka za sumu na nguo zilizotumiwa ( mitumba) ambazo awali zikipelekwa kama misaada lakini sasa zimekuwa biashara.

Umewadia wakati wa kusimama kidete kuilinda utu wetu na kuwakumbusha madaktari Mari , Locht na wote wenye fikra kama za kwao kwamba,”Afrika sio Shamba la Majaribio, bali bara linalostahili heshima kama Ulaya.”
Nasi pia tujiulize nani hasa wa kulaumiwa na kwasababu gani kuna udhaifu miongoni mwa mataifa yetu na vyombo vya kulisimamia na kulizungumza bara hili, ukiwemo Umoja wa Afrika ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eto+o na Drogba hawakuelewa majadiliano, wanapiga kelele bure.
Chanjo kipya kipo, kabla za kuruhusiwa rasmi kinahitaji majaribio. Hapo ni kawaida kuwateua watu kadhaa, wengine wanapewa chanjo, wengine hawapewi, baadaye matakokeo yanalinganishwa je tofauti ilikuwa namna gani..., je kuna hasara au matokeo mabaya.
Hao madaktari walisema majarobio yanaanza Ulaya na Australia, walipendekeza kuteua kundi la jaribio pia Afrika, kwa sababu ya hali tofauti ya huduma za afya kulingana na Ulaya na Australia.

Soma hapa BBC France racism row over Africa testing comments
 
Hivi Hawa Etoo na huyu mwenziwe wao ndio wamekua wasemaji wa waafrica?

Waafrica ni watu wa ajabu sana, Hatuna mchango wowote kwenye maendeleo ya ulimwengu halafa tunang'ang'ania lazima tupewe heshima sawa. Nikama vile wanawake wanaodai usawa wakati ni tegemezi tu.

Tuache kulalamika.
 
Eto+o na Drogba hawakuelewa majadiliano, wanapiga kelele bure.
Chanjo kipya kipo, kabla za kuruhusiwa rasmi kinahitaji majaribio. Hapo ni kawaida kuwateua watu kadhaa, wengine wanapewa chanjo, wengine hawapewi, baadaye matakokeo yanalinganishwa je tofauti ilikuwa namna gani..., je kuna hasara au matokeo mabaya.
Hao madaktari walisema majarobio yanaanza Ulaya na Australia, walipendekeza kuteua kundi la jaribio pia Afrika, kwa sababu ya hali tofauti ya huduma za afya kulingana na Ulaya na Australia.

Soma hapa BBC France racism row over Africa testing comments
Tambueni ya kwamba kuna mtego ktk hili na tunapaswa kuikataa hiyo chanjo,labda kwa mtu asiyekua mchunguzi wa kina juu ya ugonjwa husika na ugumu wa miili ya waafrika

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Tambueni ya kwamba kuna mtego ktk hili na tunapaswa kuikataa hiyo chanjo,labda kwa mtu asiyekua mchunguzi wa kina juu ya ugonjwa husika na ugumu wa miili ya waafrika

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
Sawa ukatae tu chanjo, wasalimie wazimu au hao utakapokutana nao...
 
Ni bora majaribio ya chanjo yaanzie huko huko kwenye chanzo Cha huo ugonjwa,sidhani kama sisi Afrika tatizo la corona ni kubwa mpaka ifikie hatua kwamba chanjo ifanyiwe majaribu huku.wao wapambane tu na hali zao
 
Hivi Hawa Etoo na huyu mwenziwe wao ndio wamekua wasemaji wa waafrica?

Waafrica ni watu wa ajabu sana, Hatuna mchango wowote kwenye maendeleo ya ulimwengu halafa tunang'ang'ania lazima tupewe heshima sawa. Nikama vile wanawake wanaodai usawa wakati ni tegemezi tu.

Tuache kulalamika.
We ndo hauna mchango wowote Duniani.
Unahisi bila walivyotufanya na wanavyoendelea kutufanya Waafrika hao unaowaabudu wangefika hapo walipo?
Kama wako vizuri sana kwenye uvumbuzi wa chanjo waanze kujijaribia huko wenyewe waliokumbwa na madhara zaidi yetu.
 
Madaktari ufaransa wanataka kuja ku test dawa zao za corona kwa waafrika. Wachezaji maarufu wakiafrika waja juu.

=====
Didier Drogba criticizes proposal to have corovanirus vaccine tested in Africa

- Africans express anger over French some comments on using the continent as an experiment for the test of vaccine for the COVID-19

- Some footballers from the continent have dismissed the proposal by the doctors saying Africans are not human guinea pigs

- The players are Christian Atsu, Didier Drogba and Samuel Eto'o Fils


There is outrage among the black population in France and the world after two doctors on live television pushed for Africa to be the first place where coronavirus treatments are tested.

Some world-class footballers from Africa including former Chelsea cult hero Didier Drogba have also expressed their anger and condemned the suggestion made by the French doctors.

Christian Atsu, Didier Drogba and Samuel Eto'o Fils have all lashed out the doctors, saying Africa will not be used for the experiment of the treatment of a potential cure for the deadly coronavirus.

In a Clip that is fast going viral, one of the doctors Jean-Paul Mira seemed to suggest the vaccines should be tested in Africa where he believes there “are no treatment and masks”.

He went on to liken the situation to testing out AIDS vaccines on commercial ladies of the night.

If I can be provocative, shouldn’t we do this study in Africa, where there are no masks, no treatment, no resuscitation, a bit like it has been done in some studies in AIDS, where among prostitutes, we try things, because they are exposed, and they don’t protect themselves, what do you think?” Mira said
The other doctor also named Dr. Camille Locht joined the conversation supporting his view and assertion.

Drogba was visibly the most irritated public figure by the comments on Friday, April 3 as he took to Twitter to fault them for what he viewed as blatant racism.

“I would like to vividly denounce those demeaning, false and most of all deeply racist words,” Drogba tweeted.

Some social media users have also expressed their disgust over the development with many calling on African leaders to protect its people .

On his part, Eto'o referred to the doctors as "assassins".

Insem issued a response to the back clash saying the doctors' words were completely misunderstood.

“If there is indeed a reflection around a deployment in Africa, it would be done in parallel with these. Africa must not be forgotten or excluded from research because the pandemic is global." a statement from insem said.
Africa is currently the continent least affected by the virus, although the numbers are steadily increasing by the day.

South Africa has the most cases reported with at least 1462 persons affected by the COVID-19, but with only five deaths confirmed.

In Kenya, the disease claimed the life of another patient on Friday, April 3, bringing the total number of casualties to four while the cases rose to 122.

The vaccine in question is a form of BCG, which is primarily administered to babies to prevent tuberculosis.

“If there is indeed a reflection around a deployment in Africa, it would be done in parallel with these. Africa must not be forgotten or excluded from research because the pandemic is global." Insem added in the statement.

Scientists have noted that countries which administer BCG have reported fairly fewer casualties from the coronavirus.

Source:TUKO
 
Back
Top Bottom