Waafrika/watanzania fungukeni macho na akili pia

Shadya

Member
Sep 14, 2011
87
37
Jamani wandugu hivi mshatafakari haya ya mmarekani kwa undani zaidi? Hivi ni hawa mataifa ya europ kwa nini hawakumpiga mugabe? Ulishajiuliza kwa sababu nchi yake haina dili. Na kwa nini wamemuuwa gaddafi? Kwa sababu nchi yake ni dili na miela yao yao waliyogarimu kwenye vita itarudi muda mchache na mara dufu ya hela walizotumia. Na je kwa nini wao wana vyama viwili? Ni kwa sababu wanaweza kuvicontrol na wanvicontrol vizuri tu. Je? Umeshawahi kujiuliza kwa nini sisi wametuletea vyama vingi? Hawa viumbe wametuanzia mbali ili tuanze kujichukia na kujichanganya wenyewe na tumalizane kama walivyotumia kwa watu wa gaddafi, na wakafanikiwa kumuuwa. Tuwe macho watanzania nchi yetu ni dili kwa hawa watu wanatutumia ili watumalize. Amka usitumike.
 
Back
Top Bottom